Ikulu Yaita Waandishi Wa Habari kuwaonesha Hati Ya Muungano

Ikulu Yaita Waandishi Wa Habari kuwaonesha Hati Ya Muungano

Naomba nikuulize maswali yafuatayo:-
1. Kuna hati ngapi za Muungano?
2. Kama hii ni halali je zile zilizowasilishwa hapo Mwanzo zikiwa na Saini za Nyerere na Msekwa tu na saini zenyewe feki ni nani alizipeleka kule?
3. Na Lengo la Mpelekaji wa hizo za awali lilikuwa nini?
4. Je msukumo huo wa kuionyesha hati hiyo na kuipeleka Bungeni umetokana na nini? (Jibu ni TUNDU LISSU)

Tambua kuwa kama hiki kilichoonyeshwa ni sahihi hapa ndipo CCM walipoingia CHOO CHA KIKE kwani waliyokuwa wakiyaficha katika hati hiyo yatabainika hadharani na ukweli utajulikana.

Samwel Sitta ameahidi kila mjumbe wa BMK atapata nakala, pia Katibu mkuu kiongozi kasema wataweka nakala kwenye Makumbusho ya taifa. Nadhani hapo hakuna kitakachofichwa.
 
Naomba nikuulize maswali yafuatayo:-
1. Kuna hati ngapi za Muungano?
2. Kama hii ni halali je zile zilizowasilishwa hapo Mwanzo zikiwa na Saini za Nyerere na Msekwa tu na saini zenyewe feki ni nani alizipeleka kule?
3. Na Lengo la Mpelekaji wa hizo za awali lilikuwa nini?
4. Je msukumo huo wa kuionyesha hati hiyo na kuipeleka Bungeni umetokana na nini? (Jibu ni TUNDU LISSU)

Tambua kuwa kama hiki kilichoonyeshwa ni sahihi hapa ndipo CCM walipoingia CHOO CHA KIKE kwani waliyokuwa wakiyaficha katika hati hiyo yatabainika hadharani na ukweli utajulikana.

Umenena vyema! Kina Lisu wasingaliweza kujua ipo au la Bali Kwa kudhihirishiwa na wenye kukimbilia I, yaani serikali. Ni rahisi kuainisha haukuwepo Kwa ishara za kusitasita Kwa serikali, Mara iko UN, Dar nk, tena Kwa Bahati mbaya wakatoa hio feki. Hakuna Aibu ila serikali ijilaumu Kwa kujifedhehesha mbele ya watu wake
 
Lisu utakumbukwa daima umewafanya ccm na ikulu kutoa hati ya muungano wewe no mwanaume..

Lisssssuuuuuu, huyu jamaa ana ulinzi gani, tukimkuta mabwe pande nani wa kumlaumu. Ee mungu weka mkono wako
 
walioiomba hati siyo waandishi wa habari, ni wabunge wa bunge la katiba tunatakaka ipelekwe huko na wala sii hizi sarakasi.

Hahahahaha kuna watu wamem corner Lissu akomalie hati ili siku ikitolewa avuliwe nguo. I hope hili litakuwa fundisho kwa vizabizavina wote popote walipo duniani.
 
Tundu Lissu anahoja nzuri sana.Tatizo ni kusema kuwa HATI hiyo haipo...nahisi kuna namna ya utunzaji wa Vitu muhimu na kuna utaratibu wa kuvitoa...Siyo kila kitu kukiweka weka hovyo tu. Pili kama hiyo hati ni Original huoni kuwa Tundu Lissu na kundi lake watakuwa wameaibika? Kwa jinsi tulivyo mpa sifa leo halafu ije onekana tumetoa sifa kipumbavu aisee itaniuma sana.

Kiongozi, Hati hakuna, subiri uone hii movie itakavyoelekea kuzimu.
 
Hivi uhalali wa mkataba wowote unategemea uwepo wa nyaraka za mkataba huo hasa kama pande zote zinakubaliana kuwa mkataba ulisainiwa na ushahidi wa watu kusaini na yaliyomo mwenye hiyo hati yanajulikana?

Yea, kuna mikataba ambayo lazima kuwe na nyaraka hata kama pande zote zinakubaliana kuwa mkataba ulisainiwa na ushahidi wa watu kusaini na yaliyomo mwenye hiyo hati yanajulikana.

Kwa mfano, mikataba mingi inayohusiana na transactions za ardhi must be put in writing, otherwise they will be void an unenforceable.

Suala linakuja kuwa ni lazima makubaliano ya nchi mbili zilizoungana yawekwe kwenye maandishi?

Lakini hata kama kweli hati ya muungano ipo, kwa nini inakuwa ya siri hivyo?

What is so "secret" kwenye hiyo hati ya muunguno kupelekea kufichwa hivyo?
 
si utani umenena matawi ila nina wasiwasi na kamchezo kanakoendelea.
 
ilipotakiwa kwenye bunge la katiba walisema haiwez kusafirishwa maan ipo moja tu na inaweza ikapotea njian na ushahid kupotea ss leo mbn imekua rahisi kwa waandish wa habari kuluko kule kweny macho ya wqtanzania wengi na kweny umuhim zaid ya huku? achen ubabaishaji bwana!!!
 
nahisi kuna namna ya utunzaji wa Vitu muhimu na kuna utaratibu wa kuvitoa...Siyo kila kitu kukiweka weka hovyo tu.

Right. Hizo hati ziko ngapi na huwa zinahifadhiwa wapi?

Maana Karume alishadai kuwa pamoja na kukaa Ikulu ya Zanzibar kwa miaka 10 hajawahi kuiona hiyo hati.
 
Ni halali kabisa Tz kubaki kama ilivyo kama wasomi na wapiga kura wake ndo wanaweza kutoa mawazo kama wewe.ni mawazo ya kipumba..fu kabisa.

Mkuu kabla ya kunisulubu ni bora ukarejea kusoma bandiko langu! Ukiona linaukweli mwingi ndani yake basi usisite kuniomba radhi! Nashukuru wengi wameanza kuona ukweli; HATI na sahihi za waasisi si muhimu kwa sasa kwani Muungano upo na umedumu kwa miaka 50! Muhimu hapa ni kutatua kero za muungano aidha kwa kukubaliana muundo wa serikali 1, 2, 3 na si kupoteza muda kung'ang'ania HATI na Sahihi za waasisi wakati picha za kuchanganya udongo, picha za kutiliana sahihi zipo! Tunatakiwa tu deal na Mapungufu yaliyoko kwenye muungano kwa kuyaondoa kama si kuboresha Muungano wetu...
 
hii picha itaisha tu sijui kwanini tunababaishwa hii ni hati ya ngapi
 
Safi sana Ikulu kwa kukata mzizi wa fitina.

Kwa sasa kelele za hati ya muungano zimekatwa. Tuendelee na mijadala ya msingi yenye maslahi kwa taifa.

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania itadumu ingawa ina maadui wengi. Pamoja tutashinda.

We need to go one step further. kama hati imepatikana, je baraza la wawakilishi lilishiriki kuijadili na kuiptisha km bunge la JMT lilivyofanya?
 
Tundu Lissu anahoja nzuri sana.Tatizo ni kusema kuwa HATI hiyo haipo...nahisi kuna namna ya utunzaji wa Vitu muhimu na kuna utaratibu wa kuvitoa...Siyo kila kitu kukiweka weka hovyo tu. Pili kama hiyo hati ni Original huoni kuwa Tundu Lissu na kundi lake watakuwa wameaibika? Kwa jinsi tulivyo mpa sifa leo halafu ije onekana tumetoa sifa kipumbavu aisee itaniuma sana.
hawajaaibika,kwanini hiyo hati hawataki kuionyesha mwanzoni??
 
Back
Top Bottom