Mkuu naunga mkono hoja yako kwa 100%... Kama kuishi na mwanamke kwa miaka 2 inatambulika kisheria kuwa ni ndoa halali iweje watu walioishi zaidi ya miaka 50 wamezaliana, wameendesha mambo yao pamoja, wamekabiliana na changamoto mbalimbali kwa umoja wao IWEJE leo tuseme eti Muungano ni batili kwakuwa eti cheti hakipo! Makubaliano au muungano ni zaidi karatasi yenye maandishi ya watu wawili! Muungano huu Unawakilisha Muungano wa Jamii ya watu wa Znz na Watu wa bara na umedumu kwa nusu karne mpaka sasa! Ukiangalia kwa undani utagundua kuwa pande zote mbili yaani CCM na UKAWA wote wako bias ile mbaya! Mifumo wanayopendekeza yanajikita kwenye political gain zaidi! CCM wajua kuwa ndani ya mfumo wa dola mbili wataendelea kutawala milele daima, UKAWA wanajua kuwa ndani ya dola tatu CCM itakosa nguvu na kuachia ngazi! Kama kweli wote wangekuwa na dhamira ya kweli ninauhakika leo hii Tanzania Ingekuwa Moja chini ya Serikali Moja yenye kuendeshwa kwa mfumo wa Majimbo kama zilivyo nchi za wenzetu..