Ila biashara nyingine Sinza zinachekesha sana

Ila biashara nyingine Sinza zinachekesha sana

Kuliko kukurupuka kufanya biashara kwa kuiga bora uweke benki kwenye usalama. Siku zote ukipata fedha za mkupuo, ni vizuri ukazituliza kwanza sehemu kama benki wakati ukifikiri cha kufanya. Na siku ukiamua kufanya biashara ni vizuri uanze na mtaji kidogo sana ili upate uzoefu kwanza.
amna mfanya biahara anae ogopa kupoteza ela na aka fanikiwa hio biashara haikufai kama kijana
 
Naomba nimtumie rafiki yangu kama kidubwasha cha mfano.

Aliuza kiwanja cha urithi kule Nanjilinji, akauza na nyumba aliyopewa pale Mburahati. Akanunua mzigo wa friji na Tv za Sumsung za kutosha, pesa iliyobaki akakodi fremu Sinza, akaajiri kadadaa kamsaidia kuingiza maokoto

Baada ya miezi mitatu kupita, alikafukuza, kisha akamtaka mkewe asimamie maokoto. Mwezi mmoja tena, nilishangaa sana kumkuta yeye mwenyewe golini. Wiki mbili tena nikawa napita mchana namkuta yeye akiwa ameuchapa tu huku udenda ukimmwagika mchana kweupe, siku si nyingi mbeleni nikawa nawakuta yeye na mkewe wameuchapa huku wanakoroma fofofo

Biashara kubwa kubwa zinahitaji connections, social media sponsoring, location nzuri ya fremu, ukarimu wa muuzaji, uhitaji wa bidhaa na mtazamo juu ya hadhi ya watu unaokwenda kuwauzia. Inafikia hatua mpaka msosi wa mchana hupigi ilihali una friji la Boss la 2mil dukani, inachekesha sana. Wateja hawaonekani dukani, basi achukue hata mafuta ya manabii, wapii, au amtafute mshana jr wapande kilingeni, wapi! Inasikitisha sana

Mara mia angewaza hata kufungua duka la nafaka kwa kweli. Ni hayo tu
We koma
 
Usimseme bali Mshauri afanye sponsoring mitandaoni na aweke mzigo kwa ajili hiyo.

Acheze zaidi na mitandao mingineyo. Asisahau kuwa anaweka updates mara kwa mara na kila siku WhatsApp. Watu mtaji.
 
amna mfanya biahara anae ogopa kupoteza ela na aka fanikiwa hio biashara haikufai kama kijana
Sijasema mfanyabiashara aogope risk, nimesema achukuwe tahadhari. Kuna tofauti kati ya kuwa makini na kuogopa. Hata kwenye vita kuna wakati majeshi huweza kurudi nyuma siyo kwamba wanaogopa ila wanachukuwa tahadhari.
 
Back
Top Bottom