Katika mavitu yamenipita kushoto ni bongo movie. Yaani hawa ni vituko tu. Hata kuiga tu wameshindwa.
Hapo ujue mwisho wa hiyo movie huyo mfungwa lazima atakuwa tajiri. Halafu lazima ndio mtunzi huyo huyo,na ni director huyo huyo,na editer mwenyewe na staring mwenyewe. Na movie ametunga wiki hii mwezi ujao iko hewani.
Wakajifunze Nigeria,wale jamaa wako serious sana na kazi zao. Hawa kujishow tu ndio kazi yao. Sasa mfungwa hawataki kumuondolea uhalisia,wanamuacha na heleni na nywele zake na ndevu. Bongo movie ni vituko.
Na siku hizi baada ya kuona wamechemsha kwenye movie za maisha halisia yanayoonekana,wamegeukia movie za uchawi tu ksbb vitu vya kwenye uchawi sio halisia ni vya kubuni tu atakavyo,na kudanganya sana. Wanawapata tu wanawake na watoto,lakini hawawezi kuwapata wenye uelewa.