Ila kutapeliwa kunauma wakuu

Ila kutapeliwa kunauma wakuu

Mikoa tofauti kabisaaa, kipindi hicho kwanza alikimbia akavuka boda akaitelekeza familia yake. Japo sikuwa namuona lakini hasira lazima iwepo, imagine unakula msoto afu kuna lijinga limekusababishia, hapo nabaki kumlaani tu, f**k. Zile hasira hazielezeki. Kimsingi ningemkamata kwa kipindi kile aiseee ingekuwa ni habari nyingine kabisa.

Vina muda basi, alirudi nikapewa taarifa na sikuhangaika nae tena maana tayari muda uliniponya na angalau nilikuwa nimebarikiwa kupata zaidi ya nilivyovipoteza na yeye ameharibikiwa zaidi sasa nilikuwa na amani.
Unaonekana ni tu wa dini sana mkuu,.

Ndio maana wanasemaga Muda huponya,. Mwacha tu aendelee kuhenyeka
 
Pole sana.
Mimi jamani mtu akianza tu kunitapeli namshtukia hapo hapo, huo uchawi wa aina hiyo usinipate kwa kweli
 
Huu mwaka umekua wa hovyo mapema mnoo aisee,

Habari zenu kwanza wakuu

Mwenzenu jana nimetapeliwa, na nikiri tu kuwaambia uchawi upo wakuu, Ilikua jana kuna hela nilipatiwa nikamlipie dogo Ada, Nimeenda bank( NMB)nimelipa, ile wakati natoka nikawa naelekea ile njia ya sokoni ili nikapite vile NBC then Mtaa wa zanzibar nichukue baadhi ya vitu halafu nirudi Nyumbani.. Asa wakati natembea mbele yangu kulikua na Gari Hillux ( sijui ndio hilohilo jina, ila ni haya wanatembeleaga sana wakandarasi sikufanikiwa kukariri plate number zake) Limeandikwa St. Joseph ila sikuweza kumalizia ni St Joseph nini maana kuna mtu alikua ameegemea pale kwenye Maandishi..

Napita akaniita kwa majina yangu matatu kabisa, Dada Lee habari?,, nikaitikia salama za kwako?, akanijibu tu safi za masiku nikamwambia salama nikawa nataka kuendelea kuondoka sikuwaza kwasabu nilijua huenda mteja niliwahi kumuhudumia kunijua majina yangu sio kesi,. Kabla sijafika mbali akaniita tena Akaniambia nashida mara moja naomba nisaidie nikamuuliza shida gani?,. Akasema yuko na sister mle ndani na kweli alishusha kioo ni mama mmoja hivi kavaa mavazi yale ya masista,.
Akaniambia mwanangu nina shida naomba nisaidie,. Nilikua natoa hela pale Atm bahati mbaya nimekosea pin mara3, Kadi Yangu imemezwa nasiwezi kwenda ndani kutoa sina kitambulisho,, sasa nataka uende kuna mtu nimeongea nae akahamishie hela kwenye account yako halafu utoe unipatie,,. ( Kwanza kwa maelezo kama hayo wakuu mtu mwenye akili timamu anaona kabisa hayana mashiko, kwanza kutoa hela kwenye Account yako na kitambulisho wapi na wapi?, alijuaje nina NMB account?, na kwanini asimtume yule kijana??,,. )

Basi dada enu ndo nlikua nisharogwa nahisi nikasema sawa,. Nipe namba ya huyo mtu akasema ukienda tu atakuona akachukua karatasi akaandika kiasi Tsh. 1.5m na akaomba nimtajie namba yangu ya Account nikamtajia basi nikaingia ndani, Mwenzenu nikiri tu sikua naelewa chochote mpaka wakati huo😥 ,. Nikaenda moja kwa moja nimejaza slip ya kutoa hizo hela na ni Account namba yangu niliandika,. Nimekaa foleni mpaka nimefika dirishani yule dada ananiambia mbona Acount yako haina hilo salio dada?,. Kiukweli sikua na hiyo hela ila akili yangu ilikua inaniambia kuna hela zinaingia so itakuwa ipo,. Nikamwambia yule dada basi tutoe kwanza hiyo iliyokuwepo nikarudi kujaza slip upya nikatoa laki6 na 15,. Nikarudi kule nje nikamwambia yule sista bado hawajaingiza ipo ileile yangu akaniambia nipe hiyo kwanza sisi tumwahi mgojwa wewe kaa dakika tano nenda tena watakua washahamishia hela kwako na sisi tunakuja mda sio mrefu,. Si nikakubali nimekaa weeee Pale nje sokoni kila nikienda ndani naambiwa hakuna salio..

Baadae sana ndio napata wazo hawa watakua washanitapeli maana hawakunipa hata namba yao, na Namba yao ya Account wala chochote ile karatasi waliandika tu kiasi na namba yangu ya account niliyowatajia ( Aisee jamani nimelia jana tena sanaaa),. Nikawafata wale walinzi nikawaambia nikawaelekeza na walikokua wamepark gari wanasema kule mbali sana Cctv camera haziwezi zinaonyesha kitu ( Ni kule karibu na mlango wa kuingilia soko kuu kwa mbele kidogo kama unataka Ukunje kona uende NBC),. Polisi nako ndio vilevile jana hamna hata cha maana nilijibiwa,. Na sijui ile gari ilikua ni ya St. Joseph University, St. Joseph Primary school, Hospital au ni nini??.

Nachoshukuru ni kwamba nilifanikiwa tu kulipa Ada ya dogo maana Bila hivyo walahi mzee angenikata kichwa au yeye afe kwa Pressure,.

Ila kuna watu ni wakatili sana, mlaaniwe nyie wakujiita watumishi wa Mungu halafu kumbe ni wezi,. For real wamenitia Umasikini maana ndio ilikua hela yangu ya mwisho. Mwaka ushakua wa Hovyo huu,. Tuwe makini jamani matapeli bado wapo na ninahisi wanatumia uchawi maana sio bure🤔😭
Mm kamwe siwezi kukutana ghafla barabaran na stranger alafu aongelee hela na nimsikilize.
Mara nyingi namkataa sitaki mazoea hayo
 
Kati ya banki ambazo ukienda unatakiwa uwe makini basi ni NMB. Matapeli wengi wanajichanganya ndani ya bank na wengine wanakuwa nje. Kuna dada mmoja mwaka Jana alitapeliwa mil 15 ndan ya bank. Wakat yupo ndan ya bank alifuatwa na mtu ambae hamjui ila wakajikuta wanaongea kama vile wanafahamiana.
Akili ilipokuja kuka sawa yule dada anajikuta hana hela amebaki na fomu ya kudeposit, ndo anakumbuka kumbe wakati wanaongea alimkabidhi yule jamaa hela yote.
Ee Mungu wangu🤔
 
Pole sana na kuibiwa. Mwenyezi Mungu atawalipa hao wezi na wewe atakufariji kwa namna usiyoijua.

Ya laiti ungesema kuwa aliyokutapeli ni mtu aliyevaa kanzu na mwanamke kavaa babui na gari lao limeandikwa maneno ya kiarabu ... basi humu watu wala wasingejadili kuhusu utapeli au kuibiwa bali wangejadili uislamu na kusema waislamu ni wachawi au washirikina.

Lakini kwa sababu wahusika wametoka kanisani na gari lao la St Joseph na mavazi ya mwanamke ni ya sista basi watu wanajadili kuhusu kutapeliwa kwako na wala hawajadili kabisa kuhusu ukristo wao au kanisa.
ASante mkuu,.
Ila sentensi ya mwisho imeniwazisha kidogo
 
Mitaa yangu kabisa hiyo.

Kuna classmate wangu walimtapeli kwa style hiyo kule Peramiho. Kuna madawa wanatumia kukupumbaza.

Usiruhusu kuongea sana na sura ngeni mabarabarani humu. Mambo ni mengi.
Kwakweli,. Nawaza hivi ndio nilikua sina akili wakati hadi najaza fomu mle ndani ya kutoa hela na kuwafata tena kuwapa.

Huenda kweli wanatumia madawa
 
Pole sana.
Mimi jamani mtu akianza tu kunitapeli namshtukia hapo hapo, huo uchawi wa aina hiyo usinipate kwa kweli
Usikupate tu mkuu, maana kwa jinsi wanaongea na wewe huwezi kujua hata kama wanakutapeli akili sijui ilikuwa wapi maskini
 
Kuhusu hilo duka la hao watawa nafikiri ni la vitabu kama nilivyosema lakini kama ukikuta ni tofauti basi we ingia tu usijali itakuwa nimenote tofauti maana nishawahi kufika hapo niliona kama vitabu vile. Nimekupanga mapema usije kufika hapo ukajikuta unalitafuta sana. Ok good luck to you!
 
Unaonekana ni tu wa dini sana mkuu,.

Ndio maana wanasemaga Muda huponya,. Mwacha tu aendelee kuhenyeka
Hapana hata sio mtu wa dini, sema tu by nature nipo hivyo pia maisha yanatufundisha. Ila upande wa pili pia niko brutal sana pia, huwa sitabirikagi.
 
Kuhusu hilo duka la hao watawa nafikiri ni la vitabu kama nilivyosema lakini kama ukikuta ni tofauti basi we ingia tu usijali itakuwa nimenote tofauti maana nishawahi kufika hapo niliona kama vitabu vile. Nimekupanga mapema usije kufika hapo ukajikuta unalitafuta sana. Ok good luck to you!
Thanks
 
Back
Top Bottom