Ila kutapeliwa kunauma wakuu

Ila kutapeliwa kunauma wakuu

Pole Sana.


Ulivyoona St Joseph na Sister .

Yawezekana huyo kavaa tu vazi Ila sio sister then mambo ya hela ni very sensitive kumruhusu mtu afanye alichofanya inafikirisha sana.

Pole Sana kwenye mambo ya hela unabidi kuwa makini Sana trust no body even ur self.
Binafsi hela yangu kuichukua labda unitolee bastola au unipige roba ya mbao ila kwa utapeli hakuna huo uchawi wakuniingia ili unitapeli.Yaani huu ubahiri nilio nao sijui grade,stage au level gani maana ukiniambia tu nikupe hela hata buku tu wakati tumekutana njiani labda uwe kiwete ila ukiwa viungo vyako vimekamilika kwanza mwili lazima ufe ganzi halafu ntaanza kuvimba balaa.So kunitapeli kuanzia elfu 2 tu reaction ya mwili wangu kutokana na ubahili nilionao automatically huo uchawi wa kutapelia watu unakufa kabla hata haujaniingia
 
Dawa rahisi kabisa ya kudhibiti utapeli wa aina hiyo, ni hii hapa;
Ukiwa mjini, ukitoka tu benki, au ukiwa katika mishe zako! Jitahidi uwe busy tu na mambo yako! Na usikubali kamwe kumsikiliza mtu anayekuita au kukusimamisha ili akuambie shida yake.

Na kwa ule utapeli wa kwenye simu, na wenyewe ni hivyo hivyo! Usikubali kumsikiliza mtu. Wewe mwambie kwa ufupi tu uko busy, na kama atakuambia eti kuna hela sijui imetumwa kimakosa kwenye simu yako; mjibu tu kirahisi apige simu huduma kwa wateja ili arejeshewe hiyo pesa yake! Maana hilo silo jukumu lako.
Na wala usikubali akiguse sehemu yoyote ya mwili.
 
Mimi nilipata mteja wa mpesa akaniambia anatoa 40K nikamwambia toa, akaomba namba ya wakala nikamtajia, akataja jina nikasema correct, si nikahesabu hela nikampa! kuangalia meseji iliyoingia sio!! alafu jamaa ameshaondoka aah acha kabisa.
We mzembe sana mkuu, nimefanya sana uwakala wa benki na simu sijawahi tapeliwa kwa namna yayote.

Kosa kubwa ambalo nimewahi kulifanya, nilimnunulia umeme mtu wa 20000 badala ya 2000 na hii ni kutokana na uwingi wa wateja na haraka. Lakini hata hivyo sikumpa ile receipt yenye 20k nika correct muamala nikampa wqke wa 2k ile 20k ikawa hasara kwangu.

Sent from my SM-A042F using JamiiForums mobile app
 
Huu mwaka umekua wa hovyo mapema mnoo aisee,

Habari zenu kwanza wakuu

Mwenzenu jana nimetapeliwa, na nikiri tu kuwaambia uchawi upo wakuu, Ilikua jana kuna hela nilipatiwa nikamlipie dogo Ada, Nimeenda bank( NMB)nimelipa, ile wakati natoka nikawa naelekea ile njia ya sokoni ili nikapite vile NBC then Mtaa wa zanzibar nichukue baadhi ya vitu halafu nirudi Nyumbani.. Asa wakati natembea mbele yangu kulikua na Gari Hillux ( sijui ndio hilohilo jina, ila ni haya wanatembeleaga sana wakandarasi sikufanikiwa kukariri plate number zake) Limeandikwa St. Joseph ila sikuweza kumalizia ni St Joseph nini maana kuna mtu alikua ameegemea pale kwenye Maandishi..

Napita akaniita kwa majina yangu matatu kabisa, Dada Lee habari?,, nikaitikia salama za kwako?, akanijibu tu safi za masiku nikamwambia salama nikawa nataka kuendelea kuondoka sikuwaza kwasabu nilijua huenda mteja niliwahi kumuhudumia kunijua majina yangu sio kesi,. Kabla sijafika mbali akaniita tena Akaniambia nashida mara moja naomba nisaidie nikamuuliza shida gani?,. Akasema yuko na sister mle ndani na kweli alishusha kioo ni mama mmoja hivi kavaa mavazi yale ya masista,.
Akaniambia mwanangu nina shida naomba nisaidie,. Nilikua natoa hela pale Atm bahati mbaya nimekosea pin mara3, Kadi Yangu imemezwa nasiwezi kwenda ndani kutoa sina kitambulisho,, sasa nataka uende kuna mtu nimeongea nae akahamishie hela kwenye account yako halafu utoe unipatie,,. ( Kwanza kwa maelezo kama hayo wakuu mtu mwenye akili timamu anaona kabisa hayana mashiko, kwanza kutoa hela kwenye Account yako na kitambulisho wapi na wapi?, alijuaje nina NMB account?, na kwanini asimtume yule kijana??,,. )

Basi dada enu ndo nlikua nisharogwa nahisi nikasema sawa,. Nipe namba ya huyo mtu akasema ukienda tu atakuona akachukua karatasi akaandika kiasi Tsh. 1.5m na akaomba nimtajie namba yangu ya Account nikamtajia basi nikaingia ndani, Mwenzenu nikiri tu sikua naelewa chochote mpaka wakati huo😥 ,. Nikaenda moja kwa moja nimejaza slip ya kutoa hizo hela na ni Account namba yangu niliandika,. Nimekaa foleni mpaka nimefika dirishani yule dada ananiambia mbona Acount yako haina hilo salio dada?,. Kiukweli sikua na hiyo hela ila akili yangu ilikua inaniambia kuna hela zinaingia so itakuwa ipo,. Nikamwambia yule dada basi tutoe kwanza hiyo iliyokuwepo nikarudi kujaza slip upya nikatoa laki6 na 15,. Nikarudi kule nje nikamwambia yule sista bado hawajaingiza ipo ileile yangu akaniambia nipe hiyo kwanza sisi tumwahi mgojwa wewe kaa dakika tano nenda tena watakua washahamishia hela kwako na sisi tunakuja mda sio mrefu,. Si nikakubali nimekaa weeee Pale nje sokoni kila nikienda ndani naambiwa hakuna salio..

Baadae sana ndio napata wazo hawa watakua washanitapeli maana hawakunipa hata namba yao, na Namba yao ya Account wala chochote ile karatasi waliandika tu kiasi na namba yangu ya account niliyowatajia ( Aisee jamani nimelia jana tena sanaaa),. Nikawafata wale walinzi nikawaambia nikawaelekeza na walikokua wamepark gari wanasema kule mbali sana Cctv camera haziwezi zinaonyesha kitu ( Ni kule karibu na mlango wa kuingilia soko kuu kwa mbele kidogo kama unataka Ukunje kona uende NBC),. Polisi nako ndio vilevile jana hamna hata cha maana nilijibiwa,. Na sijui ile gari ilikua ni ya St. Joseph University, St. Joseph Primary school, Hospital au ni nini??.

Nachoshukuru ni kwamba nilifanikiwa tu kulipa Ada ya dogo maana Bila hivyo walahi mzee angenikata kichwa au yeye afe kwa Pressure,.

Ila kuna watu ni wakatili sana, mlaaniwe nyie wakujiita watumishi wa Mungu halafu kumbe ni wezi,. For real wamenitia Umasikini maana ndio ilikua hela yangu ya mwisho. Mwaka ushakua wa Hovyo huu,. Tuwe makini jamani matapeli bado wapo na ninahisi wanatumia uchawi maana sio bure🤔😭
Pole sana dear
 
Yalinikuta mim mwaka ulioisha Bora umeisha nilitapelewa yaan sijawah kusajil line halaf niwape na sim sijui walinipa dawa wale watu nikajikuta had nataja passwords za mpesa kwenye Ile line kahela kangu ka mtaji[emoji24][emoji24][emoji24][emoji24] kakaenda walaaniwe jaman walaaniwe hawana huruma Hawa watu
 
bahati nzuri namba yako inayoishia 74 tunayo mkuu..

tutakufikia
Nini kujua namba? Hata ujue chumba ninacholala hakuna mpuuzi anayeweza kunitapeli,kuna mpuuzi mmoja walikuwa na ofisi ya kuzugia victoria pale green acres kona ya kuingia mwananyamala ni tapeli balaa . Basi alivyoniona kwa sura yangu ya upole akajua hili fala ngoja nilitapeli,ila kilichomkuta atasimulia wajukuu zake
 
Daaa ndio maana nakuwaga mkorofi nikisemeshwa na mtu nisie mjua. sijibu kitu maana nasikia ukijibu umenasa.
 
Daaa ndio maana nakuwaga mkorofi nikisemeshwa na mtu nisie mjua. sijibu kitu maana nasikia ukijibu umenasa.
Tatizo mimi waliniita majina yangu yote matatu,. Sijui waliyajuaje jamani😥
 
Back
Top Bottom