Ila kutapeliwa kunauma wakuu

hakuna uchawi wala nini ni ujinga na tamaa tu ulijua utapata chochote ukifanikisha
 
Nimekuamini kooooote, ila pale ulipotoa pesa bila kuomba statement kama 1.5mil. imeingia, na kama haitoshi, ukaambiwa kabisa pesa hiyo hamna.., hapo nimegoma kuamini..
RUdia kusoma vizuri mkuu,. Ningejuaje kama niko na na laki6 na 15 bila kuambiwa na kupewa statement?,. Na nilirudia kujaza Bps upya

Anyways lishapita🙌🙌
 
Bora hata ingekua wameniahidi chochote kitu😄😄🙌
 
Ndio maana Mimi Nina njia zangu za kufanya pindi tu nikikutana na watu nisiowaelewa basi kama wana Nia mbaya hawawezi kufanya kitu, sisi tuna nguvu ndani yetu.
Huwa unafanyaje mkuu,. Tujuze kwa faida ya wote basi mkuu
 
Basi mimi hao watu wanaotumia hayo mambo walishanishindwa,

Mimi ipo hivi, Nkikutana na watu wa aina hiyo baada ya salamu fupi ( majibu yangu huwa ni mafupi kwa mtu ambae simfahamu )

Akileta hoja au jambo lake ( special case kama alichofanyiwa huyu mtoa mada ) huwa sijibu kitu kwanza, Nitakuangalia kwenye macho yako direct bila kukwepesha kwa zaidi hata sec 30, Baada ya hapo huwa wanatetemeka wenyewe na wanaondoka kwa aibu sanaa wengine hata kukimbia
 
Kutapeliwa huwa ni ujinga tu, na pia kinachonipa hasira zaidi ni watu kuamini kuwa ni uchawi.
Utapeli wa papo kwa papo kweli wajinga ndio utapeliwa ila Upo utapeli wa mikakati huo ndio mbaya zaidi, Hata wewe huwezi kuruka hata kidogo
Na unatapeliwa kisha kesho yake unakutana na huyo huyo tapeli na atakununulia vinywaji na kula nyama choma kwa wingi alafu anakutapeli kwa mara nyingine

Yani anahakikisha kakumaliza hela zote hata za kumfuatilia na mwisho unaweza kukaa hata ndani na muhanga ni wewe

Kiufupi mambo ni mengi sana hapa Duniani, aina hii ya utapeli ni mbaya sana

Mimi naishi kwenye maisha ya tahadhari na umakini mkubwa kama jasusi kwa sasa hivi.
 
Kuna mpuuzi mmoja eti alikuwa ananipa dili la biashara ya madini sasa nikimuangalia usoni kapauka balaa hala kachomekea nikiangalia viatu soli zimelika upande mmoja.Nilitaka kucheka ila nikamkaushia coz sisi wanaume utafutaji wetu ni jasho na damu.Mpuuzi mwingine eti aliniomba nimuazime simu eti amfahamishe mwenyeji wake amefika hakujua kwamba nna code zake tayari
 
Haha😂,. Kwamba anauza madini halafu mwenyewe kapauka
 
Dah!,pole mkuu,wale hata sijui inakuwaje mtu unajikuta unahisi hapa SI salama,ila Kuna roho inakuambia,angalia uone mwisho wao nishawahi tapeliwa kijinga buguruni pale,nilijicheka sana,wiki ilopita nimetapeliwa na kijana wa tigo ila jiji la dar bhana,matapeli Wana moto wao wa ziada wanaturudisha nyuma sana dah!.
 
Mtu afanye nini ili hizo dawa za kutafuniwa zisimpumbaze hadi kutapeliwa?
 
Yan nimekumbuka maongezi yangu mimi na wewe hivi karibuni katika uzi fulani hivi,kwamba kuna mtu alikosea shilingi laki mbili akatuma katika namba yako kimakosa,halafu wewe ukahamishia katika namba yako ya halotel

Na ukasema siku hizi huna huruma kabisa kwakuwa ushatapeliwa sana,je huenda hela ya watu ndio imerudi na ziada juu?

Pole sana kpnz
 
Sasa doktori umeongea point muhimu sana,sasa usipojiamini mwenyewe si ndo utatapeliwa kabisa
 
RUdia kusoma vizuri mkuu,. Ningejuaje kama niko na na laki6 na 15 bila kuambiwa na kupewa statement?,. Na nilirudia kujaza Bps upya

Anyways lishapita🙌🙌
Akaunti inakuwaje na laki 6 kama kuna 1.5mil. imeingia? Hiyo ndio point yangu iliyoganya nigome kukuamini
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…