Ila Tundu Lissu Kiboko; nimekumbuka hii

Mbowe ndio anashikiria msimamo wa Lissu?

Kama Lissu alikubaliana na Mbowe kuhusu Lowassa maana yake hana msimamo kama wanasiasa wengine.

Unless kama una tafsiri yako nyingine kuhusu msimamo.

Kipindi kile Lisu Hakuwa na Cheo alichonacho sasa hivi, walikuwepo kina Slaa na mbowe

Lisu alikuwa mpiga Debe na Mwanasheria wa CHADEMA
 
Wengine wote hatuwajui lkn magu sio shujaa na mjinga kafa kwa COVID
 
😀😀😀😀

Unataka nimtetee?

Hapo wakulaumiwa ni Mbowe ndio maana Mimi simuamini Sana mbowe lakini kwenye Siasa za upinzani Lisu anamsimamo wa kiwango cha juu.
Hata Lissu ana la kujibu katika hilo! So Mbowe akiamua chochote kile yeye anafuata blindly??? Then hana msimamo!! Slaa alikuwa karibu zaidi na Mbowe kuliko Lissu lakini still alisimamia msimamo wake na akajitoa, matokeo yake akaambuliwa kutukanwa na hao akina Lissu na watu wake na kumuita mzee wa kula mihogo!! Wanasema mtu mzima akikosea huchutama, August 2015 CDM (Wote, not only Mbowe) walifanya kosa kubwa sana ambalo litawafuata kwa miaka mingi ijayo
 
Kipindi kile Lisu Hakuwa na Cheo alichonacho sasa hivi, walikuwepo kina Slaa na mbowe

Lisu alikuwa mpiga Debe na Mwanasheria wa CHADEMA
Kwahiyo hicho cheo alichonacho sasa hivi ndicho kimemfanya kuwa na msimamo,

Kwamba ukiwa mpiga debe na mwanasheria hutakiwi kuwa na msimamo ???
 
Wewe na familia yako hamuwezi kuona ushujaa wake
 
Hayo yangewezekana kwa jeshi dhaifu kama la Congo au Mozambique, sio hapa JMT. Hata angekuwa na wanajeshi waliofuzu 10000, asingeweza kuchukua chochote, na hakuna mtu angeongea hayo 'mengine' kama ulivyosema. Sio rahisi hivyo.
 
Lowasa sahivi yupo wapi? CHADEMA ni malaika wao hawakosei? poor
 
Msimamo wa Lisu upo kiwango cha juu Sana ni vile watu wengi hawajui.

Ukitaka ujue msimamo wa mtu mtishie Uhai au kugusa kitu nyeti chake ndio utaelewa Lisu anamsimamo au Hana.
 
Hizi sasa ni ramli za mchana kweupe, Tundu Lisu hakushambuliwa kwa sababu za kisiasa, kuna biashara nyuma ya pazia iliyomtokea puani. Haya huwakuta wengi tu sema yeye anajificha kwenye kivuli cha siasa, kama kesi ya Mbowe tu na matukio yake ya kigaidi.

Haya ni mawazo nitakayobaki nayo kipindi wengine wakimpa cheo cha ushujaa dalali wa mabeberu aliyetaka kudalalia nchi yetu kwa mgongo wa elimu ya sheria.
 
Hayo yangewezekana kwa jeshi dhaifu kama la Congo au Mozambique, sio hapa JMT. Hata angekuwa na wanajeshi waliofuzu 10000, asingeweza kuchukua chochote, na hakuna mtu angeongea hayo 'mengine' kama ulivyosema. Sio rahisi hivyo.

Mkuu unacheza na watu wenye msimamo mkali au huwajui vizuri.

Hata wawe Buku nyie muwe milioni kazi mnayo nakuhakikishia. Vinginevyo huelewi maana ya msimamo mkali.

Mtu mwenye msimamo mkali yupo tayari kufa Kwa kile anachokiamini akipewa Mafunzo ya kijeshi na akiwa na silaha huoni ni hatari tupu hiyo.

Usidhani kila anayeenda jeshini au aliyevitani ni jasiri😀😀😀 wengine ni kulazimishwa tuu.
 
Mwendazake ninaweza kumuamini Kwa mengi tuu.

Ila hapa nazungumzia msimamo wa Lisu sijasema namuamini Lisu au Lisu aaminiwe.

Nazungumzia ujasiri wake wengi hatuna.

Sasa ujasiri kwenye nini hiyo ni mada nyingine
Mada yako ni ngumu kidogo mtu kufunguka kwa uwazi maana kwa aliyopitia Lissu yataka moyo, ila kuna mikanganyiko mingi sana jinsi tukio lenyewe lilivyotokea na hadi leo hii kipi kinaendelea kuhusu tukio hilo!! Ishu kubwa zaidi ni jitihada zinazofanyika kumficha shahidi namba moja (Dereva) ambaye naamini kwa utawala uliopo sasa angeweza kurudi na asidhurike
 
Mpuuzi wewe, kwanini mlificha CCTV kamera na mkatoa askari pale eneo la viongozi?
 
Dereva angekufa uchunguzi usingefanyika?
 
Lowasa sahivi yupo wapi? CHADEMA ni malaika wao hawakosei? poor
Hamna asiyekosea, ishu inakuja pale mkosaji anaposhupaza shingo kwamba alikuwa right! Haijalishi Lowasa yupo wapi kwa sasa, ila uamuzi wa August 2015 ulikuwa ni uamuzi wa hovyo zaidi kupata kutokea katika historia ya vyama vingi nchi hii
 
Lakini si yupo CCM?
 
Dereva angekufa uchunguzi usingefanyika?
Umesema ANGE..., as long as yupo hai anaweza kurahisha uchunguzi, ya nini kuhangaika wakati mtu ambaye alishuhudia tukio live yupo na anarushwa rushwa tu sehemu mbalimbali? Ishu ilikuwa angekuja kipindi cha mwendazake usalama wake ungekuwa hatarini, then why asije sasa amwage kila kitu hadharani?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…