Ila walimu wa shule za Serikali wanajiaibisha sana

Fungua kanisa uanze kutapeli watu
 
Hawapo creativity siyo,huko mashuleni sijui kuna shida gani siku hizi!!!!?
Shida kubwa hawakubali kujifunza mambo mapya .

Kwakuwa walimu hapa Tanzania unaweza kufikiri wanazaliwa na mama mmoja jinsi akili zao zilivyo.

Kuna uncle wangu ni mwalimu anawakopesha hela walimu wenzake Kadi za bank na vitambulisho wanaweka kwake Kama dhamana yaani hela ikiingia yeye ndo anaenda ATM kuchukua hela anayowadai

Na wanajisifu kuwa wanakula maisha .
 
Kama mshahara wako ni chini ya 1.5M usininue hata IST yenye Cc 1490 utakua unajididimiza kiuchumi maana gari ya kutembelea tu inaongeza gharama ya maisha, matumizi yake kwa mwezi itengee Tsh 300,000/=
 
Naomba kujifunza yafuatayo:
anawakopesha kwa muda gani na riba ya asilimia ngapi?
kama wanaacha kitambulisho & ATM CARD kama dhamana, vp wakienda bank wakaripoti kua wamepoteza kadi na wakapewa kadi zingne, hapo si unakua umepoteza hela zako?

au yeye anatumia mbinu gani kuwabana?
 
Kazi wamefanya wao, mchoko wamepata wao. Wanapofurahia unataka kuwazodoa. Binadamu tumekuwaje lakini?
 
Hivi watanzania nyie tumewakosea nini sie walimu kila siku ni kutusimanga tu mnakera πŸ˜†πŸ˜†πŸ˜†
 
Kama umewazidi waalimu lakini ulipitia kwa hao walimu basi wewe ni komando.

Kuna generation tatu
1.Golden generation
2.Silver generation
3.Bronze Generation

Ukiwa mtafiti utajua kila set-up ya binadamu ina strength and weakness zake.
In Tanzaniakuna mgawanyo mbaya wa resources ndo maana Kuna gap kubwa sana la malipo..Na bado unacholipwa ni kuendeleza xircle ya chini.

Ukiwa kwenye group moja Kuna vikwazo vikubwa sana kupanda group la juu sababu watu Wana banana na kilichopo ili usipande.

Wachimbaji wa madini ni wengi sana migodini lakini wanapata madini kwa wingi ni wale wenye vifaa vya kisasa na wenye connection za matajiri wa kuwatoa Giza na kuwapaisha juu.

Ukiona watu wanafanya vacation ni Matokeo ya serving lakini huyo mwalimu unaomcheka alipoanza kazi alikutana na changamoto ya kukosa sehemu ya kuishi akaamua kujenga kwa mkopo,hii ni stutas quo,akijenga atalipa mkopo huo kwa miaka mitano tayari watoto wake watahitaji elimi.bora huku wakiwa na uwezo mdogo kutokana na make up.

Waafrika hatujui kufanya mapinduzi ya generations,unakuta mzazi anamuacha mtoto bila kumpa codes za maisha sababu ya migogoro ya familia,huenda ni Matokeo ya umaskini lakini wenzetu wahindi wanapeana codes,waarabu wanapeana connection za biashara za malori sisi Swahili people tunapigana majungu sana.

Ukianzisha biashara mtu wa kwanza kukuponda ni yule unaeshinda nae kwenye mzunguko wako(Circle).
Sisi waswahili hatuna muda wa kutafuta circle vizuri sababu sisi ni daraja la matajiri niliowataja hapo juu. In fact mpaka mwafrika anafikia level ya Silver lazima apate mentor mahili ili aweze kumpa koneksheni ya kazi na vitu vingine vya kufanya apande hapo juu.

Swala la imani nalo linakuwa kikwazo sababu hizi dini ni mapokeo tokea nje.

Tunahitaji mifumo ya familia ambayo haitaingiliana na fitna na CHUKI za kiafrik,Kuna midume inafanya kafara ngumu kuwezesha kupanda daraja la Silva lakini Matokeo yanatokea hayana mwendelezo sababu ile Silva imepanda kwa njia isiyo sahihi hivyo watoto wote wanaokuja hapo wanakuwa very allogant hawana vinasaba vya gold gen,hawana muunganiko wa incestor wa mwendelezo as result wakizubaa wanakuwa walevi,malaya,hatimaye wanarudi kwenye Bronzi.

Unaweza jitahidi kufanya mazuri lakini nyuma yako huna mwongozaji hatimaye unadondokea kwemye circle ya maskini Tena sababu waswahili tunapenda matako ya wanawake na sio genetical make up.

Ukiwa makini ukipata mafanikio sababu ya CHUKI hakuna mtu atakuongoza kwenye ndoa unadondokea.kwa aduai yako bila wewe kujua mzunguko unaanza upya.

Usimcheke mtu kila mtu anashida kwa kila maisha.
 
Umeandika mambo mengi points tu.
 
Pesa yao we unataka waitoe kwa utaratibu gani? Achana nao fanya mengine
 
Hakika, ndio maana nimesema tusiwalaumu ila tuwahurumie tu.
 
Mishahara yao ni midogo sana mkuu,
Basic salary ni 887000 kwa Sasa kwa degree,

Take home ni 587000,,, yani wanachukua salary sawa na wataalam wa Afya ngazi ya certificate walio soma college miaka miwili 😁😁😁
 
Wewe ni nurse!
Wewe ni nini mbaya na wewe kwani unakereka nini?! Hujui hawana marupirupi.ubuyu mmekomaa wasiuze,twishen hamtaki wafundishe Sasa wafanye ni i
 
[emoji1787][emoji1787][emoji1787] mkuu umetia chumvi sana. Laki moja?
 
Insightful.

Tatizo la mtoa mada anadhani yeye ni bora kuliko wengine, Ni fikra zake binafsi.

Ukweli ni kuwa hakuna Binadamu ambaye ni bora kuliko mwingine, Sote Tuna mwanzo mmoja na mwisho mmoja.
Hakuna haja ya kumdharau/kumheshimu mwingine kwasababu ya shughuli anayofanya.

Muhimu ni Kuheshimu & kushukuru kwa ulicho nacho, Kuheshimu wengine na Kutiana moyo.
 
Ndio mshahara anaotegemea, afanyeje? Auze chaki na madaftari ya shule? Hana marupurupu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…