Mimi ningeshangaa km angeongelea suala la mishahara na madaraja au mikopo ya elimu ya juu masuala ambayo ni ya kundi fulani katika nchi. Nchi hii ina zaidi ya watu 45 million, wengi wakiwa wakulima, wafanyabiashara wa chini na kati, sasa uanze kuongezea minority utakuwa Rais wa namna gani.
CCM wanatatibu kampeni na kunakuwa na ujumbe kwa kila eneo la kampeni akiongela kilichofanyika hapo, atakachofanya na anayo fanya kwa Taifa. Si jamaa yule kila mahali ni RISASI, madaraja, mikopo audience ni wafanyakazi na wanafunzi ukiongea mara moja ujumbe umefika huhitaji kwenda kuwaambia watu wa Bahi, kiteto na Shinyanga kwa wafugaji na wakulima.
Halafu wagombea waache porojo nani kasema madaraja hayapandi, nani kasema hakuna mikopo ya elimu ya juu? Km serikali imeweza ku subsidies gharama za elimu kwa elimu msingi awali hadi kidato cha nne I nawezaje kushindwa kwa mikopo elimu ya juu?. Watanzania wa leo sio vilaza kwamba ukibwabwaja tu watawaamini, tafuteni kura kwa Sera makini si kutaka huruma ya watumishi wa Umma na wanafunzi.
Kwa taarifa yenu kundi mnalohangaika nalo ni dogo na wala halijawatuma, nyie ndo mnawatia gundu tu. Mnajifanya kusahau kuwa nchi hii bado inategemea kilimo na huko vijijini bado zana ni duni, teknolojia ya usindikaji ni ndogo au hamna, masoko ni tabu na zaidi kwa nchi yenye mito, maziwa, mabonde, na mvua nzuri bado tu nategemea kilimo cha kuangalia mawingu kisicho na tiba.
Nchi yenye mapori, majani n. k bado wafugaji wanachunga badala ya kufunga kisasa au hajui hata nchi km Namibia ambayo ni jangwa inatuzidi kwa kusafirishwa nje matunda na nyama wao wamewezaje? Jamaa yule si alitembea sana vipi mbona sioni alicholeta kutushawishi namna ya kuboresha maisha ya anataka wampe dhamana.?. WINO UMEISHA NINGEENDELEA.