Ile hali ya kupenda mwanamke kupitiliza, ni akili ya kawaida au ni kulogwa?

Ile hali ya kupenda mwanamke kupitiliza, ni akili ya kawaida au ni kulogwa?

Mkuu huyo ni wakuachana naye mara moja, utaumia kama mwezi mmoja, ila utakua umejikomboa kutoka kwenye utumwa wa mapenzi, lazima uweze kuhimili mapenzi. Kuna kabinti nilikuwa na ki-date few months ago nilikua naelekea huko, nimesitisha mapenzi mazima. Utimamu wa akili kwanza
Cha ajabu, kwa sasa akirudi na kukwambia muendelee kuwa wapenzi kuna uwezekano mkubwa usikatae.
 
Kuna kumpenda mtu ile moyo unakuambia kabisa huyu ndiyo utawezana naye,unakimbia na kususa kwa sababu ya nyenendo zake mbovu ila moyo unasuta tu…”we rudi tu mama kwa usalama wako”

Watu wanachinjana huko,ila huyu jamaa sijui Kama ana muda hata wa kukasirika🙌🏾
Anaweza kuwa na nyendo mbovu, lakini bado unamng'ang'ania
 
Niliwahi kuongea na kiongozi Wa kiroho akasema mambo mengi lakini moja ni mtu huyo mnakua mnaendana katika vitu vingi kama sio vyote. Pia roho zinakua zimeridhiana hivyo kuwatenganisha ni ngumu.

Kipendacho roho hula nyama mbichi
Mbaya zaidi wa namna hii, wanakuwa ni wagharama, na uko tayari utoe mpaka senti ya mwisho.
 
Hii hali nilishakutana nayo miaka ya nyuma, unajikuta unampenda mtu kupitiliza, kuliko yeye anavyokupenda.

Na hii inatokea baada ya kuonja tunda lake, unajikuta muda wote unatamani awe karibu yako, umpigie pigie simu; wakati mwingine yeye asikupe ushirikiano lakini utatumia nguvu ata ya hela ili awe karibu tu.

Unataka kumuacha, baada ya muda unamrudia tena; wakati huohuo kuna wadada wengine wanakutafuta wewe unakuwa unawaona hawana cha maana.

Sasa najiuliza, hii ni akili ya kawaida au ni kulogwa?​
Hiyo ni hali ya kutokuwa na ukomavu wa kihisia
  • Unakuwa hauko tayali kupoteza kitu unacho kipenda.
  • Na pia hauko tayali kukubaliana na hali au kukubali maumivu.
 
Hiyo ni hali ya kutokuwa na ukomavu wa kihisia
  • Unakuwa hauko tayali kupoteza kitu unacho kipenda.
  • Na pia hauko tayali kukubaliana na hali au kukubali maumivu.
Uko sahihi, kupoteza unachokipenda ni mtihani mgumu.
 
Hii ni tabia ya kike! Mwanaume ukishakula tunda shobo huwa zinapungua kwahiyo JITATHIMINI KIJANA! Yani uache ku focus na kutafuta hela unahangaika kuwa karibu na mwanamke shenzi kabisa!
 
Ata kama ni ombaomba utajititimua umgharamie tu
Attachments tu sio kitu kingine hakuna uchawi na wala hujarogwa ni ile hali unakua unampenda mtu the way alivyo tu hii hua inatokea kwa kila mtu na sababu ni yeye kukuonyesha upendo then baadae anapokua na machaguo mengi anaanza kujiengua na kukuona wewe sio type yake hapo ndipo unapoanza kutapatapa kwamba mboni mwanzoni ni yeye ndiye alienionyesha unanipenda? Unapofikia hatua hio unaanza kuwehuka ni km umeachwa kwenye mataa hivi halafu ushaachwa na bus la asubuhi kodisha tax au bodaboda ulikimbilie kituo kinachofuata kuna hotel litasimama hapo hotelini
 
Hii hali nilishakutana nayo miaka ya nyuma, unajikuta unampenda mtu kupitiliza, kuliko yeye anavyokupenda.

Na hii inatokea baada ya kuonja tunda lake, unajikuta muda wote unatamani awe karibu yako, umpigie pigie simu; wakati mwingine yeye asikupe ushirikiano lakini utatumia nguvu ata ya hela ili awe karibu tu.

Unataka kumuacha, baada ya muda unamrudia tena; wakati huohuo kuna wadada wengine wanakutafuta wewe unakuwa unawaona hawana cha maana.

Sasa najiuliza, hii ni akili ya kawaida au ni kulogwa?​
Ni moja ya changamoto ya afya ya akili, inahitaji matibabu kama magonjwa mengine ya akili.
 
Hii hali nilishakutana nayo miaka ya nyuma, unajikuta unampenda mtu kupitiliza, kuliko yeye anavyokupenda.

Na hii inatokea baada ya kuonja tunda lake, unajikuta muda wote unatamani awe karibu yako, umpigie pigie simu; wakati mwingine yeye asikupe ushirikiano lakini utatumia nguvu ata ya hela ili awe karibu tu.

Unataka kumuacha, baada ya muda unamrudia tena; wakati huohuo kuna wadada wengine wanakutafuta wewe unakuwa unawaona hawana cha maana.

Sasa najiuliza, hii ni akili ya kawaida au ni kulogwa?​
Hii ni Hali ya kawaida kabisaa kwa Kijana wa umri wa miaka 27 kushuka chini mpaka miaka 14. Umri huo kijana anakuwa anatawaliwa sana hisia sana zile za ndani, na kuna wakati ktk umri huo anaweza kuwa anatafsiri kuwa hili ndiyo jukumu lake kuu hapa duniani. Hizo hisia huwa zinaenda zinashuka kadri majukumu yanavyoongezeka na kupigwa matukio. Baadae matukio yakizidi utaanza kuonja ladha zingine, na baada ya hapo unakuwa sugu na hiyo inaanzia miaka 28 na kuendelea.
 
Back
Top Bottom