Ile hali ya kupenda mwanamke kupitiliza, ni akili ya kawaida au ni kulogwa?

Ile hali ya kupenda mwanamke kupitiliza, ni akili ya kawaida au ni kulogwa?

Hii hali nilishakutana nayo miaka ya nyuma, unajikuta unampenda mtu kupitiliza, kuliko yeye anavyokupenda.

Na hii inatokea baada ya kuonja tunda lake, unajikuta muda wote unatamani awe karibu yako, umpigie pigie simu; wakati mwingine yeye asikupe ushirikiano lakini utatumia nguvu ata ya hela ili awe karibu tu.

Unataka kumuacha, baada ya muda unamrudia tena; wakati huohuo kuna wadada wengine wanakutafuta wewe unakuwa unawaona hawana cha maana.

Sasa najiuliza, hii ni akili ya kawaida au ni kulogwa?​
ki-lugha chetu hii hali inaitwa infatuation!
 
😹😹😹 Na mnaboa afu unakuta jitu limekuganda wewe hulipendi basi kero tupu..!!

Kuna moja mpaka nikatupa line nipumzike maana kuliblock ilikua haitoshi na hanielewi..!!
 
Hiyo hua ni hali ya kawaiada kama ukitanguliza hisia mbele halafu akili ukaziweka kwenye mfuko wa shati.
 
Ukiona watu mpaka wanaonga mali na vyeo, ujue hii dunia ina mengi.
Hilo ni tatizo la akili Love Obsessive Disorder kwanini ulazimishe mtu kukupenda?? Nyie ndo wale mnakuja kupiga wanawake Magobore kisa kujifanya mnajua kupenda sana na kujali🚮
 
Penzi la kwanza kabisa ndio huwatokea hali hiyo watu wengi,wataalamu wa mambo ya kisaikolojia na biolojia wanasema penzi la kwanza kabisa ndio penzi la kweli/lenye hisia ya kweli ambayo hua ni deep,na huwezi kumsahau hiyo mpenzi wako,

Ila mkiachana,unakua na roho ngumu sana,hakuna Mwanamke/Mwanaume mwingine atakaye kubabaisha tena au kumbabaikia na kuforce love.
 
Kuna maumbo ukiyaona unaweza kulia kama mtoto mdogo
 
Back
Top Bottom