Ile hali ya kupenda mwanamke kupitiliza, ni akili ya kawaida au ni kulogwa?

Cha ajabu, kwa sasa akirudi na kukwambia muendelee kuwa wapenzi kuna uwezekano mkubwa usikatae.
 
Anaweza kuwa na nyendo mbovu, lakini bado unamng'ang'ania
 
Niliwahi kuongea na kiongozi Wa kiroho akasema mambo mengi lakini moja ni mtu huyo mnakua mnaendana katika vitu vingi kama sio vyote. Pia roho zinakua zimeridhiana hivyo kuwatenganisha ni ngumu.

Kipendacho roho hula nyama mbichi
Mbaya zaidi wa namna hii, wanakuwa ni wagharama, na uko tayari utoe mpaka senti ya mwisho.
 
Hiyo ni hali ya kutokuwa na ukomavu wa kihisia
  • Unakuwa hauko tayali kupoteza kitu unacho kipenda.
  • Na pia hauko tayali kukubaliana na hali au kukubali maumivu.
 
Kwa namna nilivyochomoka sidhani kama atanitafuta, nilitumiwa WhatsApp msg 1078 na sikuzisoma, nilifuta zote. na nikala block, Mapambano yanaendelea
Itakuhitaji uwe na moyo wa chuma
 
Hiyo ni hali ya kutokuwa na ukomavu wa kihisia
  • Unakuwa hauko tayali kupoteza kitu unacho kipenda.
  • Na pia hauko tayali kukubaliana na hali au kukubali maumivu.
Uko sahihi, kupoteza unachokipenda ni mtihani mgumu.
 
Hii ni tabia ya kike! Mwanaume ukishakula tunda shobo huwa zinapungua kwahiyo JITATHIMINI KIJANA! Yani uache ku focus na kutafuta hela unahangaika kuwa karibu na mwanamke shenzi kabisa!
 
Ata kama ni ombaomba utajititimua umgharamie tu
Attachments tu sio kitu kingine hakuna uchawi na wala hujarogwa ni ile hali unakua unampenda mtu the way alivyo tu hii hua inatokea kwa kila mtu na sababu ni yeye kukuonyesha upendo then baadae anapokua na machaguo mengi anaanza kujiengua na kukuona wewe sio type yake hapo ndipo unapoanza kutapatapa kwamba mboni mwanzoni ni yeye ndiye alienionyesha unanipenda? Unapofikia hatua hio unaanza kuwehuka ni km umeachwa kwenye mataa hivi halafu ushaachwa na bus la asubuhi kodisha tax au bodaboda ulikimbilie kituo kinachofuata kuna hotel litasimama hapo hotelini
 
Ni moja ya changamoto ya afya ya akili, inahitaji matibabu kama magonjwa mengine ya akili.
 
Hii ni Hali ya kawaida kabisaa kwa Kijana wa umri wa miaka 27 kushuka chini mpaka miaka 14. Umri huo kijana anakuwa anatawaliwa sana hisia sana zile za ndani, na kuna wakati ktk umri huo anaweza kuwa anatafsiri kuwa hili ndiyo jukumu lake kuu hapa duniani. Hizo hisia huwa zinaenda zinashuka kadri majukumu yanavyoongezeka na kupigwa matukio. Baadae matukio yakizidi utaanza kuonja ladha zingine, na baada ya hapo unakuwa sugu na hiyo inaanzia miaka 28 na kuendelea.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…