Ile pisi ni kali imenifanya mpaka niunde business card

Ile pisi ni kali imenifanya mpaka niunde business card

OKW BOBAN SUNZU

Platinum Member
Joined
Aug 24, 2011
Posts
53,868
Reaction score
121,001
Mpaka sasa najiuliza hivi ni mimi kweli nimefikia hatua ya kupelekwa puta na pisi.

Wakuu nipo Mwanza kuna pisi moja matata rangi nyeupe imenipiga ganzi nikienda kupata huduma kwenye moja ya taasisi za fedha hapa Mwanza.

Mara ya kwanza nimeenda pale hakukuwa na foleni kubwa kwa hiyo nikapata muda wa kupiga stori mbili tatu lakini kuomba namba nikaona soo kubwa (roho huuma sana nikiomba namba halafu ninyimwe). Lakini roho ilinisumbua sana,imeogopa kuomba namba halafu tena imeumia kukosa namba.

Ikabidi nikae kikao kujadili nini kifanyike. Nikapata wazo la kutengeneza business card itakuwa rahisi kumuachia. Nikaingia stationary wakanipa pieces 100. Siku hiyo hiyo nikatinga tena kwa pisi, iko pale counter inawaka hatari.

Kama kawaida nikaipa muamala wangu na stori mbili tatu,bahati nzuri ilikuwa inanikumbuka. Wakati inanipa docs nisaini nikaiachia business card.

Mimi: Madam sorry naomba nikuachie na business card yangu.
Pisi: Asante, lakini sasa nitaifanyia kazi gani,ya kazi gani (ikaweka pembeni yake)
Mimi: Baki nayo tu kuna contacts hapo
Pisi: Sawa ila siwezi kukupigia (ikanirudishia fomu za miamala)
Mimi: (Nikajifanya sijasikia,nikaaga).

Mpaka sasa yamepita masaa mengi pisi haijapiga wala sms. Wewe bidada kama upo humu najua unanipata. Niokoe kijana wa watu. Usipofanya hivyo kesho ntarudi tena
 
Ahiiiiiiiiiii bhaghoooooshaaaaaa[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]..wew kijana hao wadada wametrainiwa kuwa humble for each customers bila kujaji, sasa wew umechekewa kidogo tu ushaamishia akili uko down[emoji23][emoji23], sasa unazan we wakwanza kupga nae story?[emoji23][emoji23] kuna wenzako hapo pia wamekuja tangu asubh na wengine jana wakaacha mpka hela ya mboga( notii noti nyekundu 400k)[emoji23][emoji23] na bado hawajatafutwa wengine wameblockiwa, sasa wew mkono mtupu nan akukumbuke[emoji23][emoji23][emoji23] inauma hee?? mke wa mtu uyooo jombaa tena kibwana chake ni choka mbaya hakina hata ishuu yoyote mjini hapa zaid ya kuvaa vinjunga mjini,na kulamba lips[emoji23][emoji23][emoji23].....acha tamaa
 
Hahahaha!.

Benki? Sehemu ambayo mtu huweza kuona salio lako bila tatizo. Ameshachungulia, akaona wewe bado.

Kuna pisi niliizimikia. Alikuwa teller PREMIER LOUNGE. Akanihudumia, nikamuomba aniangalizie salio, akaniandikia akanipa. Nikamuachia ya maji. Alinitafuta mwenyewe.

Achana na mambo ya business Card. Hiyo utawapa wanawake wajanja wanaojiweza. Hawa ambao bado wanapata 600k, wewe muombe account number.

Dumbukiza kama 200k. Namba atakupa mwenyewe.

Mengine mtamalizana mnavyojuana.
 
Nilishawahi fukuzia Pisi moja benki flan nikatafuta mbinu ya kuipata nikakosa nikaumiza kichwa Sana.
Nikaja na mbinu moja nikawa nachukua hela toka NMB napeleka huko alipokua yeye... mda mwingine nachukua kwa mawakala napeleka pale kwa siku nikawa naenda pale Kama Mara kumi ...siku mbili zilitosha kupata namba mpka kesho nachakata tu na mtoto kanizalia ...!
 
Nilishawahi fukuzia Pisi moja benki flan nikatafuta mbinu ya kuipata nikakosa nikaumiza kichwa Sana.
Nikaja na mbinu moja nikawa nachukua hela toka NMB napeleka huko alipokua yeye... mda mwingine nachukua kwa mawakala napeleka pale kwa siku nikawa naenda pale Kama Mara kumi ...siku mbili zilitosha kupata namba mpka kesho nachakata tu na mtoto kanizalia ...!
😂😂😂 kuna watu mna moyo
 
Back
Top Bottom