Ili kuchochea uboreshaji wa viwanja LIGI KUU wadau mbali mbali wa soka waandae maandamano ya "viti" na "magunia" kwenye kila mechi.

Ili kuchochea uboreshaji wa viwanja LIGI KUU wadau mbali mbali wa soka waandae maandamano ya "viti" na "magunia" kwenye kila mechi.

OMOYOGWANE

JF-Expert Member
Joined
Dec 30, 2016
Posts
4,701
Reaction score
11,920
Habari wakuu,

Mpira wetu umepiga hatua mbili mbele, ila viwanja vyetu vimepiga hatua mbili nyuma.

Leo hii Feitoto anachuana na Aziz ki kuchukua kiatu cha mfungaji bora, kipa Rey Matampi anapambana na Diara kuwania tuzo ya golikipa bora, wakati huo Simba akipambana na Azam kupigania nafasi ya pili, costal ikichuana vikali na KMC kuwania nafasi ya nne, wakati huo timu zingine zikifungana point na zingine zikipishana point chache.

Ligi yetu ya NBC PL inatizamwa na nchi zote za afrika mashariki kupitia vinga'muzi vya Azam, haya ni maendeleo makubwa.

Ila sasa viwanja ndio vinazidi kuchakaa,

Uwanja wa Meja Isamulyo hauna viti, uwanja wa CCM liti hauna viti, uwanja wa sokoine mbovu, uwanja wa Tabora mbovu, uwanja wa Geita mbovu, uwanja wa kirumba umepitwa na wakati. Ule wa arusha umejaa matuta

Kama uchumi wetu ni mbovu basi ndio tukose hata pa kukaa uwanjani, yaani tusimame tu? Mpira ni burudani Bodi na TFF mturuhusu tuingie na viti vyetu au mabenchi uwanjani.

Tuingie na magunia matupu ya kuhifadhia mpunga ktk kila kiwanja chenye eneo bovu la kuchezea (pitch) kama ishara ya kutaka mabadiriko.
0d1d2d98dd010a10e6b7c5b1ca99b39f.jpg


Maandamano ya viti na magunia yawe kama chachu ya kushinikiza uboreshaji wa miundombinu ya uwanjani.

Tuwaamshe TFF na bodi maana wamelala sana wamelala sana.

Hii iwafikie wadau wote wa soka nchini.
 
Hivyo viwanja ni vya ccm lakini Kila mara vimekuwa vikihamasishwa na kukarabatiwa na serikali huu ni wizi wa mchana kweupe
Vifungiwe mechi zichezwe kwenye viwanja vichache vyenye unafuu
!.chamazi
2.mkapa
3.uhuru (iboreshwe zaidi)
4.Namungo
5.Kaitaba(iboreshwe)
6.Manyara (KIWANJA kipo Cha binafsi.)
 
Back
Top Bottom