Uchaguzi 2020 Ili kuondoa kelele za kutotendewa haki, nawashauri CHADEMA na ACT wekeni Mawakala kila Kituo ili kujiridhisha, Uchaguzi Mkuu ni huru na wa haki

Kaka Mayala sio bure utakuwa ushasamehewa ile kodi uliyokuwa unadaiwa sio kwa kujipendekeza huku. Uchaguzi huru na haki sio kuhesabu kura ni mchakato wote mpaka kuisha kwa uchaguzi, mbona ujaongolea figusi za tume kwa wagombea waliowaengua kwa mizengwe?
 
Angalieni nyomi kama hii, kama wote hawa ni wapiga kura, then ushauri wa bandiko hili ni muhimu sana, this time hatutaki kelele, za watu kuibiwa kura!.
P
 
Huu mjadala unaendelea kwenye group fulani la WhatsApp, na mimi naendelea kusisitiza

Shemeji @⁨paul sarwatt james⁩, kwanza naheshimu mawazo yako. CCM is the only party that has the capacity and the capability kuweka mawakala kila kituo.
Ballot boxes are transparent, na zinakuja sealed no one can temper, kura zinapigwa kituoni na zinahesabiwa kituoni na matokeo ya vituo vyote yanabandikwa vituoni, hivyo hakuna wizi wowote wa kura vituoni!.

Kama kunafanyika wizi au mchezo mchafu wa bao la mkono ni kupitia vote rigging, ambapo mabox yenye kura, yanapelekwa kwenye tallying centres.

Kama kura zote za vituoni zimebandikwa vituoni, hakuna kosa lolote kwa vyama kufanya an independent tallying kwa kutumia tuu wanachama wao kila kituo, wawe na simu janja. Una downloads scanner program, hivyo huhitaji kuwa na mawakala, unahitaji kuwa na wanachama wenye simu janja, kazi yao ni ku piga picha matokeo ya kila kituo kwa scanner ya simu janja na kuyatuma kwenye independent tallying centre ya Chadema, ACT Wazalendo.

Kama there is nothing to hide, hakuna ubaya wowote kwa vyama kufanya independent tallying, kosa ni kutangaza matokeo. Hiyo independent tallying inafanywa bila kutangaza matokeo.

Chedema wakiwa na kanzi data ya matokeo ya vituo vyote nchi nzima, ambayo ndio NEC wanayo, NEC wakitangaza matokeo tofauti kwa kuongeza kura za bao la mkono, then, the opposition will have a very strong case to argue.

This time around, ushindi wa kishindo kwa CCM is very clear and clean na hatutaki kelele, hivyo nimeshauri
Ili kuondoa kelele za kutotendewa haki, nawashauri CHADEMA na ACT wekeni Mawakala kila Kituo ili kujiridhisha, Uchaguzi Mkuu ni Huru na wa Haki
P
 
Naona mkuu umeamua tu kujitoa ufahamu
1. 2015 UKAWA walikua na Tallying centers mbili nini kilitokea? THRDC/LHRC? One of them, walikua na joint task force ya waangalizi wa uchaguzi walikua wana tally pia matokeo. Wote tunafahamu taasisi zote mbili zilivamiwa zikapokwa laptops na hard drives na mpka napoongea hazikuwahi rudishwa then unasema tallying inasaidia?
2. Kafulila alifanya tallying ila what happened? Kaambiwa nenda mahakamani kma huajridhika and the rest was history. Hiyo pia ilimkuta wenje,Bungo and Naftali. Maalim pia alikua mpka na Nyaraka ila out of the blues uchaguzi ukafutwa ila kura za muungano kwa zenji hazikufutwa!! Coincidence?
3. Kuhusu mawakala haina faida kma masanduku yataongezwa mfano kule mbagala na kinondoni watu ilibidi wavamie ofisi watishie kuchoma masanduku ndio matokeo yakatangazwa then unasema tallying? Kule kwa Mtolea uchaguzi wa marudio wakiona wizi umegoma wakawatoa mawakala wote wa upinzani nje then unasema wakiwemo tu ni automatic credibility ya uchaguzi? Je nani analimiy movement za ndani ya jengo? Ulinzi wa kura? Fomu kuwa altered?

Bora ungeshauri CCTV zifungwe vituo vyote vya majumuisho na kila fomu iwe scanned itumwe kwenye website ya tume kila mtu aone na kuepuka watu kulia faulo. Ama uchaguzi usimamiwe na wawakilishi kutoka AU watakaokua neutral ama kura zihesabiwe za wazi kabisa kituo kwa kituo ila sio kelele za mawakala bado hazisolve kitu maana uchaguzi ni process sio event hivyo mpaka kura zinaanza kuhesabiwa kuna rafu 100 zishachezwa kinachobaki ni kukamilisha tu utaratibu.
 
Pascal acha kuzuga watanzania hao mawakala mtawanyima viapo. R.I.P Dada akwilina
Pia Kanuni ya uchaguzi inasema kuwa wasimamizi wa vituo vya kupigia kura hawalazimiki kuwapa mawakala wa vyama nakala za matokeo ya vituo vyao. Unajua tafsiri yake? Kwa msingi huo, independent tallying inawezekanaje? Kwa simu janja itakuwa sio official. Lakini suppose tunagundua kuwa JPM kashindwa which is likely, twaweza kufanyaje? Mahakamani sheria imekataza. Je atakubali? Tume yake itakubali kutangaza mshindi? Kama majibu ni hasha, nini kitatokea? Mwenyezi Mungu tunusuru!!!
 
Kama kura zinapigwa kituoni, kuhesabiwa kituoni, na matokeo yote hadi ya urais kubandikwa ubaoni hapo hapo kituoni, hizo kura za maruhani, wataziingizia wapi?, huku kila kituo kuna mawakala wa vyama?.
P
Wakubali basi kuwapa nawakala official coppies ili kuwe na independent tallying. Kutokufanya hivyo kikanuni ndio mpenyo wa kura za maruhani.
 
Kutumia phrase kama hii sio busara na sio lugha ya kiungwana kabisa! Kelele inamaanisha kinachopiganiwa hakuna mantiki! This in incorrect kabisa! Usifikiri CCM watabaki daima dawamu kwenye madaraja, chochote ninaweza kutokea dakika yoyote
Mwamba umepotea wapi rudi jamvini. Umeaunga juhudi mkono kimya?
 
Hawana rasilimali watu wala rasilimali fedha
Nilishuhudia wakala wa chadema wakati wa maboresho ya daftari la wapiga kura akiwa ni mwana ccm kindaki ndaki
Kuiondoa ccm sio kazi rahisi
 
Paschal alijijengea heshima sana amekuja kuharibu sijui kwanini? hana mvuto tena
 
Nimesoma tu title ya post yako na kuidisqualify. Kimsingi Post yako imelenga kupotezea watanzania muda wao.

Unachanganya Uchaguzi na Kupiga Kura. Wakati Post inaongelea Uchaguzi Huru nanwa Haki, maelezo ya ndani yanaongelea nini kifanywe Siku ya Kupiga Kura.

Mayalla sote tunaamini wewe ni mwandishi mzoefu. Na unajua Uchaguzi ni Mchakato (process) na sio tu kupiga Kura (event). Unaposema Uchaguzi Huru na wa Haki wakati Hadi sasa hiyo Haki na Huru hatuvioni unamaanisha nini?? Au unatufanya wajinga?

Upigaji Kura ni kitendo kinachohitimisha Tu Mchakato wa Uchaguzi. Tukukumbushe kuwa, tunapoongelea Uchaguzi Huru na Wa Haki, fahamu tunaongelea mchakato mzima na sio tu kitendo cha kupiga Kura.

So far hadi sasa kinachoendelea sio cha Uchaguzi Huru na wa Haki. Wewe unajua Kwanini sio Huru na Haki. Wagombea wengi wa Upinzani wameenguliwa, wamenyimwa Uhuru na Haki yao kugombea. Ila umekaa kimya Kwa vile unalinda maslahi yako na ya familia yako. Kimsingi umeamua kuisaliti nchi yako Kwavile unapata Maslahi fulani. Ila kwa kivumbi kinachoendelea kutimshwa na TL, wasaliti mjipange.
 
Mkuu nzotangai , karibu, mitaa hii
Uchaguzi 2020 - Ili kuondoa kelele za kutotendewa haki, nawashauri CHADEMA na ACT wekeni Mawakala kila Kituo ili kujiridhisha, Uchaguzi Mkuu ni huru na wa haki
hapa nimezizungumza hoja zako, kura zinapigiwa kituoni, zinahesabiwa kituoni na matokeo, yanabandikwa kituoni, huo wizi wa kura unauzungumzia, unafanyikia wapi?!.
P
 
We jamaa akili zako uliziachaga sokoni hauko sawa kichwani
 
We jamaa akili zako uliziachaga sokoni hauko sawa kichwani
Mkuu yomboo , kiukweli kupitia post yako hii, nikajikuta nalisoma upya bandiko hili, ili isije kuwa ni kweli siko sawa kichwani, kwasababu hata wale vichaa, wanaotembea utupu, wanawashangaa watu wanaovaa nguo, wanaficha nini!.

Hivyo nimelipitia bandiko hili mwanzo mwisho, sijaona popote ambapo siko sawa!. Kwavile kila mtu has the right to his/her own opinion, nayaheshimu mawazo yako, ila ingenisaidia sana naa kuwasaidia wasomaji wetu humu, kwa kushea your views ni nini hakiko sawa.
P
 
Wewe ni MPUMBAVU wa hali ya juu. Na WAPUMBAVU kama wewe Nchini kwetu ni tatizo kubwa sana.

 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…