Ili kuongeza fursa za kusoma Post Graduate, Je wagombea urais mtairudisha AIMS?

Ili kuongeza fursa za kusoma Post Graduate, Je wagombea urais mtairudisha AIMS?

Prof Janabi wa JF

Senior Member
Joined
Jul 7, 2023
Posts
189
Reaction score
490
Ili kuboresha elimu Africa washirika mbalimbali wanatoa hela zao kufadhili masomo ya wanafunzi wa post graduate wa hesabu kwa taasisi inayojulikana kama African Institute of Mathematical Sciences (AIMS). Chuo hiki kiko nchi mbalimbali kikichukua wanafunzi wa hesabu na engineering na kuwasomesha bure kwa ngazi ya Masters na PhD, na uzuri wa PhD zao nyingi ni joint PhD unaanza kusoma nchi ya Africa kisha unamalizia Marekani.

Kwa sasa nafahamu kwamba AIMS iko Rwanda, Ghana na baadhi ya nchi za Africa. Tanzania, AIMS ilikuja mwaka 2017, kwa taarifa nilizonazo ni kuwa UDSM iliogopa kwamba watu wataenda zaidi AIMS na kuiacha UDSM hali iliyofanya chuo hiki kifungwe.

Hata hivyo, nafasi za AIMS ni very competitive na sio kila mtu atapata, na kuacha nchi nyingine ziwe na chuo hiki huku sisi tukiwa hatuna taasisi hii muhimu ya kufua wanasayansi tunaathiri elimu yetu.

Kwa kuwa huu ni mwaka wa uchaguzi, nawauliza wagombea wa urais kama wako na nia yoyote ya kurudisha chuo hiki ili watoto wa kitanzania waweze kusoma nasi tukawa na wanasansi wa kutosha.

Nategemea majibu kwenye kampeni zenu,

1757915321136.png
 
na kuacha nchi nyingine ziwe na chuo hiki huku sisi tukiwa hatuna taasisi hii muhimu ya kufua wanasayansi tunaathiri elimu yetu.
AIMS haina tofauti na TECU, nawaona waliosoma shahada za uzamili AIMS wakiendesha bodaboda na kulima nyanya.

Elimu inayotolewa Afrika inamtenga msomi na fursa zinazomzunguka.
 
AIMS haina tofauti na TECU, nawaona waliosoma shahada za uzamili AIMS wakiendesha bodaboda na kulima nyanya.

Elimu inayotolewa Afrika inamtenga msomi na fursa zinazomzunguka.
Kuendesha bodaboda sio ishu, na hiyo sio kwa maana kuwa elimu yao haina maana, bali matumizi ya wanasayansi nchini bado ni ya kusuasua. Kumbuka AIMS wanaanzia Masters
 
Back
Top Bottom