Ili kupunguza hasara, ATCL ifute safari kuelekea vituo visivyo na abiria, hasa Chato

Ni wazi kwamba ndege ya ATCL inayokwenda Chato huwa inaenda tupu, bila abiria

Abiria pekee ni mama Janeth Magufuli na watoto wake au Kalemani.

Nashauri ruti hii ifutwe kwa maslahi ya taifa.
Aahaaaa
 
Tunawajua waajiriwa wa January Makamba humu JamiiForums ukiwemo wewe chiembe
IMG-20230410-WA0012.jpg
 
chiembe
Na wenzako someni hii kutoka kwa mwana JamiiForums mwenzenu ambae nimemnukuu hapa chini.

"Tumeona mpaka gazeti la mwananchi wameingia kwenye upuuzi wa kuandika habari zisizo na ukweli wowote kuhusu Chato, hospital ya Kanda ya Chato imekuwa msaada mkubwa Kwa wananchi wa Kanda ya ziwa, uwanja wa ndege Chato umeendelea kufanikiwa kwani ndege za shirika la ATCL zimeendelea kutua mara tatu Kwa wiki tofauti na hapo mwanzo zilikuwa zinatua mara mbili tu Kwa wiki.

Shirika la Hifadhi za Taifa (Tanapa) imeiteuwa Hifadhi ya Burigi-Chato kuwa miongoni mwa hifadhi mbili nchini zitakazoendeleza kuhifadhi faru weupe ambao ni adimu zaidi nchini.

Kupelekwa kwa faru weupe katika hifadhi hiyo ambayo ni ya tano kwa ukubwa kati ya hifadhi 22 zilizopo. Hivyo kutaifanya kuwa miongoni mwa hifadhi zenye sifa ya kuwa na wanyama wakubwa watano.

Kwa mujibu wa Kamishna msaidizi wa uhifadhi, Jonny Nyamhanga ambaye pia ni msimamizi wa Hifadhi ya Taifa ya Burigi Chato amesema wanyama wengine wakubwa wanaopatikana katika hifadhi hiyo ni pamoja na tembo, nyati, simba na chui.

Akizungumza ofisini kwake na waandishi wa habari leo Desemba 02, 2022, Nyamhanga amesema uwepo wa faru katika hifadhi hiyo itakuwa kichocheo cha kuongeza wageni na kwamba watalii watapata fursa ya kumbatiza faru kwa kumpa jina ambalo atalilipia kwa kipindi fulani.

Nyamhanga amesema mbali na utalii wa wanyama wa nchi kavu pia watalii wanaweza kufanya utalii wa majini na kuona wanyama kama kiboko pamoja na kuvua samaki kwa ndoano na kwamba hifadhi hiyo inaupekee wa kuwa na maziwa matano ndani ya hifadhi.

“Hifadhi hii pamoja na uchanga wake lakini wanyama wanaongezeka kwa kasi zamani waliokuwa wakiwindwa, sasa wameanza kuamini kuwa wako salama hawajifichi kama mlivyotembelea na kujionea wenyewe ongezeko kubwa la wanyama. Pia vivutio kama mti mmoja mkubwa ambao ukiwa kwenye eneo hilo unaweza kuwatazama wanyama wote kwa wakati mmoja,” amesema Nyamhanga.

Aidha hifadhi hiyo inapakana na nchi tatu za Afrika Mashariki ambazo ni Rwanda, Burundi na Uganda na kwamba uwepo wa eneo la mipaka ya nchi tatu ni fursa nyingine inayoweza kuingiza watalii na kuongeza pato la Taifa.

Akizungumzia watalii wanaoingia katika hifadhi hiyo, Nyamhanga amesema idadi inaendelea kuongezeka siku kwa siku. Mwitikio wa wazawa uko chini na kuitaka jamii kubadilika na kuona hifadhi ni mali yao na wanapaswa kuwa mstari wa mbele kuzitembelea na kuona rasilimali zilizopo.

Consolata Evarest miongoni mwa wanahabari waliotembelea hifadhi hiyo amesema kutokana na ongezeko la wanyama ndani ya hifadhi ni wakati sasa wa makampuni ya utalii kutangaza hifadhi hiyo kwa kupeleka wageni kwa wingi.

“Tumezoea kuona magari mengi kwenye hifadhi nyingine kwa kuwa hii ni hifadhi changa na haijazoeleka ninaimani kampuni za utalii zitatembelea na kuona wanyama walivyo wengi,” amesema Evarest.

“Kujionea maziwa haya matano pamoja na eneo la mpaka wa nchi tatu, hivyo kwa sababu hizo ni rahisi kumtoa mgeni Rwanda na kuja Burigi anapita kwenda Serengeti kisha ataenda hifadhi zilizoko kaskazini,” amesema Evarest.

MWANANCHI"
 
Ni wazi kwamba ndege ya ATCL inayokwenda Chato huwa inaenda tupu, bila abiria

Abiria pekee ni mama Janeth Magufuli na watoto wake au Kalemani.

Nashauri ruti hii ifutwe kwa maslahi ya taifa.
Ungesema ifute safari za chato. Mkuu inaelekea wewe ndege unaziona angani tu hata haujawahi kuiona imetua, mara zote nimepita mwanza kupitia chato pale tulikuwa tunashusha abiria sio chini ya 20 hadi 30 na kubeba kwa idadi hiyo hiyo. Sasa umefanya utafiti gani sijui hadi upendekeze kufutwa ruti ya mwanza kupitia chato in short hakuna safari ya dar chato bali ni mwanza via chato distance ya dakika 15 ndo inakufanya utoe mapovu kiasi hicho
 
Nyumbu wanateseka sana na Chato
 
Unajua gharama za kupandisha ndege angani -take off, na kuishusha? Kwa yale madege makubwa makubwa? Unalirusha na kulishusha kwa Kila dakika tano? Halafu hivyo vinauli vya Chato mwanza ndio vifidie mafuta hayo? Haiwezekani, hiyo ruti ifutwe
 
Ni wazi kwamba ndege ya ATCL inayokwenda Chato huwa inaenda tupu, bila abiria

Abiria pekee ni mama Janeth Magufuli na watoto wake au Kalemani.

Nashauri ruti hii ifutwe kwa maslahi ya taifa.
Kwanza unao utaalam hata wa biashara au na wewe umeona uandike tu .

ATCL (na mashirika yote ya ndege) inao wataalam ambao hufanya upembuzi yakinifu wa kitaalan kabla ya kuanzisha route. Pili route/biashara inapoanzishwa sio lazima itengeneze faida papo hapo wakati mwingine wataalqm wana foresee kuwa baada ya muda fulani trend itaanza kubadilika na kuanza kupunguza hasara hatimaye kuleta faida kanili.

Ni vizuri mtu atoe ushauri kwa, jambo ambalo ana weledi nalo.

Hata hii ripoti ya CAG wengi wameichukulia kama dini vile wakati kuna naeneo inawezekana kabisa amekomoa asiowapenda kwani naye ni binadamu.

Nb: Binafsi ripoti ya CAG kuna wizi mkubwa ameubainisha na ni kweli umefanyika lakini pia inawezekana kuna ufisadi mwingine ameufunika hakuutaja.. pia kuna maamuzi amedai kulitia hasara taifa lakini si kweli kuwa ni hasara bali ni mtazamo wake

Siku zote mtu akitaka kuchambua jambo aweke chuki/ mahaba pembeni halafu aepuke kusoma kama kasuku.
 
Kaeni pale tuwasokote, mmeiba sana
 
Back
Top Bottom