JOHNGERVAS
JF-Expert Member
- Mar 22, 2016
- 1,011
- 1,681
ILI KUWA NA FAMILIA IMARA NA VIONGOZI BORA WA BAADAE TANZANIA IFUNDISHE SOMO LA “UTAIFA” KUANZIA DARASA LA AWALI ILI KULINDA TAMADUNI ZETU NA KUJENGA JAMII YENYE MAADILI MEMA.
SHULE AU DAY CARE ZA MITAANI PIA ZISHIRIKISHWE MAANA WATOTO WANASHINDA HUKO.
Kabla sijaanza anaomba nitoe Maana ya UTAIFA, Utaifa ni jumla ya mambo yote ya kiutamaduni, kiuchumi au kisiasa yanayowaunganisha watu kama nchi moja. Kwa hali hiyo, udugu na ujamaa huweza kuzaa utaifa na uzalendo.
Kwa mujibu pia wa Mtandao wa Wikpedia inaeleza kwamba Utaifa ni itikadi ya mtu kupenda taifa lake kupita kiasi, hata kudharau watu wa mataifa mengine. Hivyo ni tofauti na uzalendo unaomfanya mtu apende nchi yake kwa kutambua mema mengi aliyopata kutoka kwake
Suala la Mmmonyoko wa maadili na Ukosefu wa maadili ni Janga kubwa sana kwa taifa letu na linaweza kuwa na madhara makubwa sana huko baadae kama Halitatafutiwa ufumbuzi wa Kudumu kwa haraka, Na suala hili linachochewa sana na kuziacha tamaduni zetu na kukumbatia Tamaduni za mataifa Mengine na kudharau tamaduni zetu wenyewe
Imefika hatua sasa huko mtaani watoto hawaheshimu kabisa wakubwa, hawaheshimu wazazi hivi hawa watakuja kuwa wazazi wa iana gani huko baadae? Au watakuja kuwa viongozi wa aina gani?
Watoto wanafanyaiana vitendo vya kikatili wao kwa wao, tena vinavyohusisha Vitendo vya ulawiti na ubakaji.
Tanzania yenye makabila zaidi ya Mia moja Ishirini yote yamekuwa na Tamaduni tofauti tofauti na Miiko tofauti lengo ikiwa ni Kutengeneza jamii ya watu waliostaarabika.
Lakini pia Tanzania ina Tamaduni zake ambazo zinaitambulisha Tanzania na utamaduni huo unalinda maadili ya kitanzania na kuimairisha udugu n.k
BAADA YA UTANGULI HUO SASA TWENDE KWENYE HOJA YANGU
Somo la Utaifa ni muhimu sana kwa kizazi hiki na haliepukiki ili tuweze kuwa na Taifa la watu waliostaarabika watu wenye maadili mema, hivyo inapaswa watoto wafundishwe tangu wakiwa wadogo ili waweze kujitambua, kutokana na pilika pilika nyingi za wazazi kujitafutia Maisha hivyo hawana Muda kabisa na watoto wao wato wanaachiwa wasaidizi wa ndani au wanawapeleaka shule (day care) mapema
Kutokana na hali hiyo wazazi huamua kuwapeleka watoto wao kwenye vituo vya Kulelea watoto DAY CARE ambapo huko huenda kujifunza mambo mbalimbali Lakini zaidi elimu Ya kawaida KUSOMA, KUANDIKA NA KUHESABU huku eneo muhimu la utaifana maadili likisahaulika
Watoto hawa wasipoandaliwa vizuri kuwa na maadili mema, kuipenda Nchi yao, upendo na kudumisha Udugu huko baadae tutakuja kuwa na kizazi cha hovyo sana na viongozi wasiokuwa na maadili.
Viongozi wanapokosa maadili hawataogopa kuiba Kodi za wananchi, hawatawaheshimu wananchi (wateja wao), hawataheshimu ofisi za Umma, hawataogopa Rushwa, hawataogopa kumfanyie mtu yeyote ukatili n.k na matokeo yake taifa litapoteza Mwelekeo.
Matendo yote maovu yanayofanywa na Viongozi wa umma,viongozi wa Dini na watu wote wenye mamalaka ni matokeo ya Ukosefu wa maadili, malezi bora, Ambavyo vyote hivyo hubebwa na kukosekana kwa Kitu kinachoitwa UTAIFA
NAMNA GANI UTEKELEZAJI WAKE UTAFANYIKA?
Suluhisho la hayo yote ni Kuwa na njia sahihi za Kuwaandaa watoto hawa wadogo kwanza wajitambue kwa kufundishwa UTAIFA. Somo hili liwekewe Mkazo liwe ni somo la Lazima kabla hata haajaanza kufundishwa Elimu hi ya kawaida ya Kuhesabu, kuandika na Kusoma yaani ianze Darasa la awali.
KWA NAMNA GANI?
Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum kwa Kushirikiana na Wizara ya Elimu na teknolojia Kuandaa Muongozo maalumu wa Ufundishaji wa Somo hilo kwa shule zote pamoja na Vituo vya shule za kulea watoto DAY CARE kwa sababu watoto wengi kwa takwimu ambazo sio Rasmi asilimia 80% ya watoto wanaoishi mijini wanasoma kwenye hivyo vituo hivyo itasaidia kuwafikia watoto hao.
Somo hilo pia liwe la lazima kwenye Shule za awali au chekechea pamoja na Shule za Jumapili na madrasa liwe ni somo la lazima huko kwa kufuata Muongozo ambao utatolewa na wizara hizo mbili nilizozitaja hapo Juu.
Somo hilo lizingatie zaidi kuwafundisha au kuwalea watoto Kwa kufuata misingi na tamaduni za kitanzania wajivunie utanzania wao, wajivunie utamaduni wao, waishi kwa kufuata mila na desturi za kitanzania, na kufundishwa tabia njema kumheshimu kila mmoja kwenye jamii, kupendana na masuala mengine yanayohiana na hayo.
Tatu, somo hilo pia linaweza kuendelea kufundishwa katika shule za msingi na sekondari kwa Jinsi itakavyofaa
KAMA WAZO HILI LITAZINGATIWA NA KUFANYIWA KAZI, Ni matumaini yangu kuwa Baada ya miaka ishirini (20) tunaweza kuwa angalau na kizazi chenye mwelekeo unaofaa tofauti na kupunguza Kwa kiwango kikubwa mmonyoko wa Maadili katika jamii kwa sababu kwa sasa hali ni mbaya watoto hawajui kusalimia wala kuwaheshimu wakubwa, Vipi hawa wakija kuwa viongozi huko baadae hali itakauje?
MWISHO;
Somo hili liende sambamba na kuwajengea uwezo wa kutoa taarifa kuhusiana na matukio ya Ukatili yanayoendelea ikiwemo Ubakaji kwa wasichana na Ulawiti kwa wa kiume.
Bila kusahau matumizi sahihi ya mitandao ya Kijamii kwa sababu hata wakilelewa vizuri mitandao ya kijamii inaweza kuwaathiri kwa kiasi kikubwa Hivyo ni lazima pia wajue matumizi sahihi ya mitandao ya kijamii.
Watoto wenye maadili na malezi bora ni wazazi Bora na viongozi bora kwa kizazi kijacho.
Serikali pia kwa kushirikiana na wadau wengine waandae Program mbalimbali za mafunzo kwa Vijana wenye Umri wa kuanzia miaka 15 Na kuendelea, mafunzo hayo yawe Endelevu kwa ajili ya Maslahi mapana ya nchi yetu
TANZANIA NI YETU SOTE
Andiko hili limeandikwa na Yohane Gervas Massawe
Email gervasyohane@gmail.com
Instagram @drsalekaa

Upvote
6