Ili Magufuli aibadilishe Tanzania, ni lazima awe Rais kwa zaidi ya miaka kumi

Ili Magufuli aibadilishe Tanzania, ni lazima awe Rais kwa zaidi ya miaka kumi

Maswali mazuri sana Mkuu. Leo hii, Marekani au hata South Afrika, anaweza kuingia Mkwere na bado nchi isitetereke, kwa sababu imeshajenga momentum/resilience ya ku-absorb ukwere wowote utakaoletwa na raisi Mkwere kwa kipindi cha miaka minane ya uraisi kikatiba. Hicho ndicho ningependa Magufuli aifanyie Tanzania - kumpa nafasi ya kujenga momentum au resilience ya Tanzania kiuchumi na kidesturi (culture) katika uwajibikaji. Na hicho pia ndicho kilifanyika katika nchi kama South Korea na Singapore. Hazikubadilika kwa viongozi kukaa miaka minane au kumi ya kikatiba. Ila sasa zina momentum/resilience ya kutosha kuweka utaratibu wa miaka nane au kumi, na kuhimiri ukwere wowote utakaotokea katika kipindi hicho.

Hivi unajua Tanzania kuna wakati watu walikuwa wanaenda ofisini kupiga soga, kunywa chai na kupiga simu ya ofisi na kurudi nyumbani? I believe Magufuli ana silka ya kubadili hii culture mbovu sana ambayo tuliipata katika awamu moja tu ya kikatiba ya miaka 10. Na tunaongelea zaidi ya miaka kumi kwa kuwa ni rahisi kujenga culture mbaya katika miaka kumi kuliko kuiondoa katika miaka kumi.
Sina tatizo na mawazo yako mkuu lakini tatizo langu ni moja na Magufuli pamoja na mazuri yake ni mtu ambaye anapenda kuchagua upande wa kuegemea kwa kusema hivyo sihitaji kusema Tanzania ina makabila mangapi, dini za aina ngapi, wasio kubaliana na mitazamo yake na upinzani unazidi kukua kwa kasi ya ajabu nk
sidhani kama pamoja na hayo yote niliyo yataja yatatuvusha salama kwa aina ya uongozi Magufuli

Hivi kuna kipindi watu walikuwa wawajibikaji kama wakati wa Nyerere? Kwa maana hiyo hili la Magufuli kurudisha nidhamu ya utendaji na uwajibikaji sio ndio pekee litatuoa hapa tulipo kwenda kwa kina Malaysia..

Kwa mfano kulikuwa na sababu gani ya msingi kujenga uwanja wa ndege chato kama jambo la kwanza baada ya yeye kuingia madarakani?
Kwanini wasinge panua uwanja wa Mwanza kwa kuongeza runway ama KIA ama kufunga mataa ya kuongezea ndege kwenye viwanja vidogo?

Turudi kwenye elimu shule hizi nini iliua misingi yake Ilboru, Tabora boys /girls, Mzumbe, Kibaha, Moshi/Tanga/Arusha/ Tech, Msalato, Kilakala, Old Moshi Nk
kifupi ni kwa sababu hatuna sera za elimu mpaka leo kama taifa. Akiingia Mungai sijui chemistry na Physics liwe Somo moja sawa tu.. Haya sijui Shukuru kawambwa watoto wamefeli ili serikali isihaibike basi tu standardize matokeo ndio hizo BRN mwishowe watoto wanaingia kidato cha kwanza kusoma na kuandika hawajui...
Hayo yote hayahitaji manguvu kuya shughilikia ama sijui umimi wa kusema mimi ni Raisi sipangiwi fomu nilichokuwa mwenyewe nk...

Kwa kusema hayo mkuu bado naona kiza kinene hata akipewa miaka 100
Historia ni Somo zuri mkuu kuna kina Mugabe very intelligent and committed aimeshia kuifanyia nini Zimbabwe?

Museveni yupo madarakani miaka mingapi Uganda kuna nini?

Kenya hapo viongozi wao wanakaa muda gani? Mbona wao wanazidi kupiga hatua?.
 
Mkuu, ni kweli, lakini hilo linawezekana katika nchi iliyoendelea tayari. Nchi kama Norway it does not matter nani anakuwa raisi kwa kuwa raisi anaingia pale kwa ajili ya kusimamia, sio kuendeleza nchi.

Katika nchi changa kama Tanzania, ili nchi iendelee, unahitaji kufanya strategic planning. Strategic planning haiwezi kuwa ya miaka mitano au kumi. Inakuwa ya kuanzia miaka 15 hadi 50. Sasa ikiwa raisi anajua kuwa atakuwa na miaka 10 tu, thinking yake inakuwa confined kwenye timeframe ya miaka 10 - atafanya nini katika kipindi cha miaka 10. Sasa mambo ya kufanya katika miaka 10 mara nyingi sio mambo ya kuleta maendeleo ya muda mrefu au ya kudumu sana. In fact, mara nyingi lead up time za project au mikakati mikubwa ya maendeleo ni kuanzia miaka 5 hadi 20.

Kwa mfano, leo Magufuli anaweza hata kuja na development strategy ya miaka 20, akaja mtu mwingine kama raisi baada ya miaka 5 au 10 akaifutilia mbali na akataka iwepo ya kwake. Mind you, huyo mtu sio lazima abadilishe development strategy ya Magufuli kwa sababu anatoka upinzani, anaweza kuwa wa kutoka CCM pia. Vipao mbele vya maendeleo vya Magufuli sio vipao mbele vya Kassim Majaliwa, au hata Mwigulu Nchemba. Hizi ilani za vyama vya siasa si mali kitu - mara nyingi zina mambo madogo madogo sana ambayo hayana impact kubwa kwa uchumi.

Na of course, upande wa pili ni raisi kuwa na muda wa kutosha kujenga culture na descipline ya uwajibikaji katika nchi, kama nilivyosema hapo juu, kuua tabia kama za watu kwenda ofisini kupiga soga, kuiba stationery za ofisi, kutoa photocopy na kuprint document binafsi au kama biashara, kunywa chai ya ofisi na kupiga simu binafsi kwa gharama za serikali. Watanzania ndipo tulifikia hapo. Watu walikuwa wanaenda, na bado wanaenda, ofisini sana sana kufanya hayo, na wanalipwa mishahara.

Mhu! ngoja nitasoma baadaye, labda naweza kuelewa vizuri.
 
Naunga mkono hoja na hili na mimi pia niliwahi kulizungumzia na nikapendekeza tumpe angalau vipindi 4 vya miaka mitano mitano na kusiwe na uchaguzi wa rais ili kubana matumizi.

Kwa Kasi hii ya Magufuli, kuna haja Kufanya Uchaguzi wa Rais 2020?
Nilisema hivi


Pascal
Huna hoja ila una vioja Pascal Majanga, ivi muna khofu ya nn kuhusu uchaguzi ikiwa huyu muheshimiwa anafanya vizuri? Kwa nn asiweke fair ground Kwa vyama vyote wananchi wakaamua maisha yao?Pascal Majanga hebu jaribu kuipotezea njaa kidogo na kuwa Neutral, itendee haki akili yako, usijaribu kutetea jambo ambalo nyuma ya kichogo akili inakusuta.
 
Ukisikia Rais wa nchi anasema hawezi kusafiri kwa sababu akisafiri huku nyuma watu watapiga dili maana yake hiyo nchi haina mifumo ya utawala bora.
Kwa nchi yenye mifumo bora ya utawala mifumo mahsusi ndio inayotawala nchi.
Ninachomuomba Mheshimiwa Rais atusaidie kuweka mifumo ya utawala bora ambayo hata akitokea mrithi wake akawa kichaa kama Trump asiweze kufanya lolote atakalo nje ya mifumo iliyowekwa.
 
Ili awe kiongozi zaidi ya miaka hiyo.msisahau kumtafute Mungu Mwenyezi mfunge naye mikataba wa kumfanya aishi..akiwa na siha njema ..atawale limitless kama mugabe

Unapoona mtu kapewa bia kumi..za raundi ya tano.tano mbili amekunywa..hata ya tatu hajafungua ...anaalazimisha aletewe kreti kwa mkupuo huku anaonekana tayari kashalewa basi utachukulia ni sehemu ya ulevi wa hii pombe...iitwayo MADARAKA
 
Huwa najitahidi kuongea ukweli, japo mara nyingine watu wananikasirikia. Nakumbuka mapema sana, kabla hata jina Bulldozer halijajulikana kitaifa na kimataifa, nilisema humu JF Magufuli ni mchapa kazi sana, lakini labda ningependelea awe na nafasi ya Waziri Mkuu badala ya Raisi, kwa sababu anafanya kazi kama bulldozer, nikimaanisha alihitaji mtu ambaye sio "impulsive" kumwongoza, kama ilivyokuwa kwa Nyerere na Sokoine. Baadaye nilishangaa kuona jina Bulldozer limemnasa Magufuli.

Sasa nitawaambia jambo jingine. Tanzania tumegawanyika kwa sasa, pro na against Magufuli. Huko nyuma nilisema pia Tanzania ilikuwa imefikia pabaya sana na hivyo labda ilikuwa vema na wakati muafaka kupata kiongozi wa namna ya Magufuli, angalau kwa miaka kumi. Lakini sasa najua kwamba miaka kumi haitatosha. Najua hii ni kauli ya kuleta hasira, lakini ndio ukweli wenyewe.

Hakuna Raisi duniani anaweza kuibadilisha nchi toka alipoikuta Magufuli kwa kipindi cha miaka kumi tu. Na hatari ya miaka kumi ni kwamba raisi atakayefuata anaweza kuharibu mazuri yote yaliyofanywa, kwa sababu yale mazuri yanakuwa hayajaota mizizi sawasawa (established sustainable systems). Na hiyo ni ukweli wa-kishule (academic truth) kwamba ili nchi iendelee inahitaji mipango ya muda mrefu isimamiwe na mtu ambaye yuko committed kuisimamia (committed leadership to implement strategic national development plans). Hakuna mpango wa muda mrefu wa kuiendeleza nchi utakaotekelezwa chini ya miaka kumi. Huo ndio ukweli wenyewe.

Ukiangalia historia ya mataifa yaliyoendelea haraka chini ya viongozi wao maarufu, utaona kwamba mafanikio ya nchi hizo hayakuletwa na viongozi waliobadilisha hizo nchi katika kipindi cha miaka kumi tu. Mifano mizuri ni Singapore, Malaysia na hata Rwanda. Singapore kwa mfano, kuna wakati fulani kiongozi wao alilalamikiwa, na hata kukasirikiwa kwa maamuzi magumu aliyofanya, lakini angalia alipoifikisha Singapore, toka taifa masikini sana. Ilimchukua miaka zaidi ya kumi kufanikisha hilo. Malaysia ni hivyo hivyo na Rwanda ndiko wanakoelekea.

Huwezi kuilinganisha Tanzania na nchi kama Marekani, ambao tayari wana "established systems" ambazo hazihitaji raisi mzuri kukaa madarakani zaidi ya miaka nane. Na mie ni wa kwanza kukubali kwamba ukiweka utarataibu wa kutokuwa na kikomo cha uraisi kabla hujampata Raisi mzalendo kama Nyerere au Magufuli, hatari ni kwamba unaweza kumpa nafasi raisi fisadi au mbovu akaharibu sana nchi. Mifano ya nchi za namna hiyo ipo mingi imetuzunguka.

Lakini sasa tunajua Magufuli ni mtu wa namna gani. Yapo ambayo sikubaliani na Raisi Magufuli, na hata kumkasirikia mara nyingine. Lakini ni mengi zaidi ninayokubaliana naye, hasa katika kukabiliana na ufisadi na kuleta nidhamu ya uwajibikaji. Watanzania tulilala sana, tulifikia uozo mbaya sana. Niliwahi kuwaambia kuna mke wa raisi alimfokea kiongozi wa bandari kwa kukataa kuyatoa makontainer yake bila kuyalipia kodi. Aliitwa ikulu (na mke) na akaishia kuyatoa bila kupenda.

Na ukweli unabakia, kwamba, kama kweli Tanzania tunahitaji mabadiliko ya kutumia rasilimali zetu tuwe kama Singapore au Malaysia, basi mtu kama Magufuli anahitaji kuwa madarakani kwa zaidi ya miaka kumi. Najua hii ni lugha Watanzania wengi, na hasa vyama vya upinzani, hawawezi kuifurahia, lakini huo ndio ukweli. Baada ya hiyo miaka labda ishirini ya Magufuli, basi tunaweza kurudi tena kwenye uraisi wa kipindi cha miaka kumi au hata nane. Tutakuwa tayari tuna "established system" huenda hata kwa kiwango cha Singapore. Kama ikibidi vyama vya upinzani kuungana na CCM kwa sasa ili kufanikisha hilo basi na iwe hivyo.

NB: Naomba niweke wazi kwamba thread hii nimeiweka katika context ya strategic national development, na sio ushabiki wa kisiasa. Nimetukanwa sana humu kwa kumkosoa Magufuli, na bado msimamo wangu ni kwamba kuna mazuri sana anayofanya Magufuli, na pia yapo mabaya sana anayofanya. Mie siko CCM wala upinzani. I just call a spade - spade.
Hapa unaonesha kuwa kwa miaka 10 atafeli,sasa inamaana ahadi alizotoa ni za uongo?Aache maneno atekeleze ahadi zake
 
Pole aumini katika mtu na sio taasisi imara, swala la kuongeza muda ni hatari sana kuliko ufikiliavyo. Linaweza likabadili kabisa mfumo wa political stability!!!!! tusipime kina cha bahari kwa mguu.
 
FB_IMG_1499055654409.jpg
 
hatuwezi kuendelea kwa kunyamazisha mawazo ya watu wengine na kumtazama mtu mmoja. kila mtu ana mchango wake katika maendeleo hivo kila mtu apewe nafasi.
We kweli mburura, maana ya rais in mini? Unavyosema kila MTU asikilizwe inamaana watu wote in marais? Watanzania tunaongea sana pia mipango in mingi mno Ila utekelezaji no hafifu ndo maana tunang'ang'ania kila MTU asikilizwe ili tuishie kupanga tu na maneno mengi mwisho wa siku tunabaki hapohapo na mipango yetu. Anachofanya magufuli no sahihi kwa watu wenye nia ya taiga kusonga mbele ila kwa wazembe na mafisadi kama wewe wataona wananyanyaswa na hafai.
 
Huwa najitahidi kuongea ukweli, japo mara nyingine watu wananikasirikia. Nakumbuka mapema sana, kabla hata jina Bulldozer halijajulikana kitaifa na kimataifa, nilisema humu JF Magufuli ni mchapa kazi sana, lakini labda ningependelea awe na nafasi ya Waziri Mkuu badala ya Raisi, kwa sababu anafanya kazi kama bulldozer, nikimaanisha alihitaji mtu ambaye sio "impulsive" kumwongoza, kama ilivyokuwa kwa Nyerere na Sokoine. Baadaye nilishangaa kuona jina Bulldozer limemnasa Magufuli.

Sasa nitawaambia jambo jingine. Tanzania tumegawanyika kwa sasa, pro na against Magufuli. Huko nyuma nilisema pia Tanzania ilikuwa imefikia pabaya sana na hivyo labda ilikuwa vema na wakati muafaka kupata kiongozi wa namna ya Magufuli, angalau kwa miaka kumi. Lakini sasa najua kwamba miaka kumi haitatosha. Najua hii ni kauli ya kuleta hasira, lakini ndio ukweli wenyewe.

Hakuna Raisi duniani anaweza kuibadilisha nchi toka alipoikuta Magufuli kwa kipindi cha miaka kumi tu. Na hatari ya miaka kumi ni kwamba raisi atakayefuata anaweza kuharibu mazuri yote yaliyofanywa, kwa sababu yale mazuri yanakuwa hayajaota mizizi sawasawa (established sustainable systems). Na hiyo ni ukweli wa-kishule (academic truth) kwamba ili nchi iendelee inahitaji mipango ya muda mrefu isimamiwe na mtu ambaye yuko committed kuisimamia (committed leadership to implement strategic national development plans). Hakuna mpango wa muda mrefu wa kuiendeleza nchi utakaotekelezwa chini ya miaka kumi. Huo ndio ukweli wenyewe.

Ukiangalia historia ya mataifa yaliyoendelea haraka chini ya viongozi wao maarufu, utaona kwamba mafanikio ya nchi hizo hayakuletwa na viongozi waliobadilisha hizo nchi katika kipindi cha miaka kumi tu. Mifano mizuri ni Singapore, Malaysia na hata Rwanda. Singapore kwa mfano, kuna wakati fulani kiongozi wao alilalamikiwa, na hata kukasirikiwa kwa maamuzi magumu aliyofanya, lakini angalia alipoifikisha Singapore, toka taifa masikini sana. Ilimchukua miaka zaidi ya kumi kufanikisha hilo. Malaysia ni hivyo hivyo na Rwanda ndiko wanakoelekea.

Huwezi kuilinganisha Tanzania na nchi kama Marekani, ambao tayari wana "established systems" ambazo hazihitaji raisi mzuri kukaa madarakani zaidi ya miaka nane. Na mie ni wa kwanza kukubali kwamba ukiweka utarataibu wa kutokuwa na kikomo cha uraisi kabla hujampata Raisi mzalendo kama Nyerere au Magufuli, hatari ni kwamba unaweza kumpa nafasi raisi fisadi au mbovu akaharibu sana nchi. Mifano ya nchi za namna hiyo ipo mingi imetuzunguka.

Lakini sasa tunajua Magufuli ni mtu wa namna gani. Yapo ambayo sikubaliani na Raisi Magufuli, na hata kumkasirikia mara nyingine. Lakini ni mengi zaidi ninayokubaliana naye, hasa katika kukabiliana na ufisadi na kuleta nidhamu ya uwajibikaji. Watanzania tulilala sana, tulifikia uozo mbaya sana. Niliwahi kuwaambia kuna mke wa raisi alimfokea kiongozi wa bandari kwa kukataa kuyatoa makontainer yake bila kuyalipia kodi. Aliitwa ikulu (na mke) na akaishia kuyatoa bila kupenda.

Na ukweli unabakia, kwamba, kama kweli Tanzania tunahitaji mabadiliko ya kutumia rasilimali zetu tuwe kama Singapore au Malaysia, basi mtu kama Magufuli anahitaji kuwa madarakani kwa zaidi ya miaka kumi. Najua hii ni lugha Watanzania wengi, na hasa vyama vya upinzani, hawawezi kuifurahia, lakini huo ndio ukweli. Baada ya hiyo miaka labda ishirini ya Magufuli, basi tunaweza kurudi tena kwenye uraisi wa kipindi cha miaka kumi au hata nane. Tutakuwa tayari tuna "established system" huenda hata kwa kiwango cha Singapore. Kama ikibidi vyama vya upinzani kuungana na CCM kwa sasa ili kufanikisha hilo basi na iwe hivyo.

NB: Naomba niweke wazi kwamba thread hii nimeiweka katika context ya strategic national development, na sio ushabiki wa kisiasa. Nimetukanwa sana humu kwa kumkosoa Magufuli, na bado msimamo wangu ni kwamba kuna mazuri sana anayofanya Magufuli, na pia yapo mabaya sana anayofanya. Mie siko CCM wala upinzani. I just call a spade - spade.
ulaaniwe ufe siku yoyote kuanzia leo
 
Huu ni mwiko mkuu....tukishauvunja huu then hatuna sababu ya kwanin tusivunje mingine yote!
 
Angeanza na Katiba angehitaji miaka miwili tu ya kuibadilisha nchi hii. Lakini kwa kuwa anadhani Katiba sio kitu cha maana ila mawazo yake basi ameshafeli hata kuliko wenzake waliomtangulia japo wenye mawazo finyu wanadhani anafaulu.
 
Hapa unaonesha kuwa kwa miaka 10 atafeli,sasa inamaana ahadi alizotoa ni za uongo?Aache maneno atekeleze ahadi zake
Uko absolutely right! Si rahisi Magufuli, au raisi yeyote wa nchi changa, kufanikiwa kwa miaka 10. Angalia kwamba akijua ana miaka 10 tu, Magufuli anakuwa kama yuko desparate kuanzisha miradi mikubwa ambayo sio rahisi kuikamilisha katika kipindi cha miaka 10; SGR, Stiegler dam (hii mimi naipinga), daraja la Kigamboni hadi Mbezi sijui, Fly overs, Bandari Bagamoyo, elimu bure, Highway four lanes hadi Chalinze, kukuza ATC, LNG plant, Kuhamia Dodoma, etc!

Hivi umewahi kujiuliza gharama za miradi mikubwa hii ni kiasi gani? Na hizo fedha Magufuli atazipata wapi ndani ya miaka 10? Na tukisema haya ni mazuri sana, Magufuli atakuwa ametupeleka mbali sana akifanikisha yote; je ataweza kuyafanikisha ndani ya miaka 10, tukijua lead time za hizi projects?

Kuna faida gani kufuata katiba ambayo itatupa mtu baada ya Magufuli ambae miradi kama hiyo itakuwa ni ndoto kwake kuifanikisha? Labda anakuja aliye bora kuliko Magufuli, lakini suala ni, are we prepared to take that chance given that we already know what kind of leader Magufuli is when it comes to implementing such critical national development projects?

Ukweli hayo yote ni sehemu ya strategic developement, lakini there is no way utasema ni rahisi kuyasimamia yote yakatekelezwa ndani ya miaka 10. Na hakuna uhakika kwamba Magufuli akitoka atakayekuja atayafanikisha kwa sababu anaweza kuwa fisadi kama wale waliotangulia. Na si hii miradi tu, mie nasema na kuna mengi zaidi yanahitajika. Kwa mfano, hata humu JF niliwahi kupendekeza magari yote yanayokwenda kusini kuanzia Morogoro itengenezwe barabara ya kupitia Mkuranga kwa kuwa ni shortcut zaidi ya kupitia Chalinze. Na pia nikasema barabara zote zinazoingia mikoani zitengenezwe dual carriage way (four lanes) kwa angalau km 10 kuepusha misongamano. Sasa vitu kama hivi vikianishwa, vinahitaji raisi anaeweza kusimamia utekelezaji wake awe na zaidi ya miaka 10 kama raisi.
 
Back
Top Bottom