Synthesizer
Platinum Member
- Feb 15, 2010
- 15,415
- 29,584
- Thread starter
- #301
Sina tatizo na mawazo yako mkuu lakini tatizo langu ni moja na Magufuli pamoja na mazuri yake ni mtu ambaye anapenda kuchagua upande wa kuegemea kwa kusema hivyo sihitaji kusema Tanzania ina makabila mangapi, dini za aina ngapi, wasio kubaliana na mitazamo yake na upinzani unazidi kukua kwa kasi ya ajabu nk
sidhani kama pamoja na hayo yote niliyo yataja yatatuvusha salama kwa aina ya uongozi Magufuli
Hivi kuna kipindi watu walikuwa wawajibikaji kama wakati wa Nyerere? Kwa maana hiyo hili la Magufuli kurudisha nidhamu ya utendaji na uwajibikaji sio ndio pekee litatuoa hapa tulipo kwenda kwa kina Malaysia..
Historia ni Somo zuri mkuu kuna kina Mugabe very intelligent and committed aimeshia kuifanyia nini Zimbabwe?
Museveni yupo madarakani miaka mingapi Uganda kuna nini?
Kenya hapo viongozi wao wanakaa muda gani? Mbona wao wanazidi kupiga hatua?.
MKuu, sijasema kwamba kiongozi yeyote akikaa zaidi ya miaka 10 atailetea nchi yake mabadiliko mazuri, la hasha. Ninachosema ni kwamba, ili kiongozi mzalendo ailetee nchi yake maendeleo mazuri anahitaji zaidi ya miaka 10 ya utawala, na nikatoa mifano ya nchi ambazo zilibahatika kupata viongozmi wazalendo sana, wakakaa zaidi ya miaka kumi na kuzibadilisha hizo nchi zilizokuwa katika umasikini mkubwa na kwa namna ya ajabu sana - Singapore, South Korea, Malaysia nk. Au hujasikia kuna wakati Tanzania na nchi kama Malaysia au South Korea zilikuwa karibu sawa tu!
Na ukitaka kujua si kila raisi anaekaa madarakani kwa zaidi ya miaka 10 analeta maendeleo, angalia mtu kama Mobutu. Alikuwa raisi kwa karibu miaka 30 lakini akaiua kabisa Zaire.
Umetaja Kenya. Kenya ni tofauti sana na Tanzania. Wao walipopata uhuru walikuwa na miondombinu bora zaidi yetu kama msingi. Unajua Mwingereza hakutegemea kuondoka Kenya kwa sababu lilikuwa koloni, wakati sisi tulikuwa protectorate. Kwa hiyo Kenya walianza na mtaji mkubwa zaidi yetu. Ila sasa, kama Kenya wangekuwa na aina ya raisi kama Magufuli, basi wangekuwa mbali zaidi sana ya hapa walipo - kwenye ligi ya South Africa, Egypt na Nijeria.
Kwa hiyo swali langu la msingi ni hili; Magufuli ndio aina ya raisi kama wale waliozipeleka mbali Singapore, Malaysia na South Korea ili na yeye tumpe zaidi ya miaka kumi kama walivyopewa hao maraisi ili aibadilishe Tanzania na kuifanya kama Singapore au South Korea ya Afrika?