Ili Magufuli aibadilishe Tanzania, ni lazima awe Rais kwa zaidi ya miaka kumi

Ili Magufuli aibadilishe Tanzania, ni lazima awe Rais kwa zaidi ya miaka kumi

Nyerere alikaa miaka mingapi? Zaidi ya watu kuliwa na simba na sera zake za hovyo kuna jipya? Zaidi yakutaifisha mali za watu kuna jipya?

Mugabe amekaa miaka mingapi? Kuna jipya alilolifanya kwa watu wake?

Maendeleo ya nchi hayaji kwa mtu kukaa miaka mingi madarakani. Sheria na katiba ndio msingi wa maendeleo. Kama mambo yatakuwa hayahaya tunampa miaka 100 atajaza magereza tu
 
Una maana kuna established systems alizoanzisha na ni zipi hizo. siamimi kama tunahitaji mtu mmoja kubadili nchi bali tunahitaji watu wote. tunahitaji bunge lifanye kazi yake constructively. Kwa mazingira ya tanzania kubwa ni maarifa ambayo msingi wake ni elimu elimu elimu. hii si miaka ya Aristotle na Plato. si miaka ya mitume.

Kwangu mimi mchangiaji huyu yupo makini kuliko mtoa mada na wachangiaji wanaounga mkono hoja ya kumwongezea JPM muda wa kuwepo madarakani.Ninamwamini sana na ninakubaliana na hatua nyingi anazozichukua.Ninakubaliana na uwazi wa kukisema,kukisimamia na kufuatilia anachokisema au kuagiza.Sikubaliani hata chembe na ndoto ya kumwongezea muda wa kuongoza nchi yetu.

Kufanya hivyo ni kukiri kuwa hakuna tena watu waaminifu,shuja ,wakweli na wanaoweza kusimamia maslahi ya nchi yetu ila JPM peke yake.Hili siliamini na silikubali kama nisivyokubaliana na ujinga wa kuamini kuwa wazungu wana uwezo mkubwa wa akili kuliko wafrka.

Hata mimi nina mshaka kuwa baada ya JPM kumaliza muda wake anaweza kuja mhuni atakayeharibu kila kitu kizuri kilichoanzishwa.Tunalijua tatizo ,tunajua dawa yake,tusiogope kuinywa.Ni chungu lakini ndiyo tiba yetu.Katiba ya Warioba kabla ya JPM hajamaliza muda wake tuikamilishe.Tuondoe uhuni wote uliochomekwa humo na wahuni kwa maslahi yao kwa kubebwa na CCM.

Tanzania ni zaidi ya CCM na wapinzani wao.
 
Nyerere alikaa miaka mingapi? Zaidi ya watu kuliwa na simba na sera zake za hovyo kuna jipya? Zaidi yakutaifisha mali za watu kuna jipya?

Mugabe amekaa miaka mingapi? Kuna jipya alilolifanya kwa watu wake?

Maendeleo ya nchi hayaji kwa mtu kukaa miaka mingi madarakani. Sheria na katiba ndio msingi wa maendeleo. Kama mambo yatakuwa hayahaya tunampa miaka 100 atajaza magereza tu

Kama hujaona jema lilifanywa na Nyerere kujibizana na wewe ni kupoteza muda.Ni kweli yako mabaya aliyoyatenda.Akili timamu hupima kati ya mema na mabaya kuangalia upande upi una uzito.Akili timamu pia hufuatilia chanzo cha ubaya ulifanyika na lengo la tendo hilo.

Baada ya Nyerere wamepita Mzee Mwinyi,Mkapa,Kikwete na sasa Magufuri kati yao hakuna anayekaribia hata 50% ya aliyoyafanya.

Unamtaja na Mugabe huoni wala hujui alichokifanya.Ni mpuuzi tu ambaye anaweza kuona ni akili kubwa Mugabe akabidhi Zimbabwe kwa Tsvangirai na ategemee walio wengi Zimbabwe wanufaike na mabadiliko hayo.Unaijua vizuri historia ya Zimbabwe kuanzia kipindi cha kupigania uhuru,ahadi za Waingereza kwa wananchi wa Zimbabwe kuhusiana na ardhi na utekelezaji wake? Kama unajua huna tofauti na Tsavangirai,unatamani uwatumikishe raia wa nchi yako kwa maslahi ya wanaokulipa.Hufai kwa M
 
Ipi kaanzisha?

System gani kaanzisha Magufuli?
System ya ku-sign mikataba ya madini na mafuta kuzuia mikataba hovyo! Na hii ya watumishi wa umma kuomba kibali kabla ya kusafiri nje. Dont worry. Ndio kwanza anaanza.
 
Huwa najitahidi kuongea ukweli, japo mara nyingine watu wananikasirikia. Nakumbuka mapema sana, kabla hata jina Bulldozer halijajulikana kitaifa na kimataifa, nilisema humu JF Magufuli ni mchapa kazi sana, lakini labda ningependelea awe na nafasi ya Waziri Mkuu badala ya Raisi, kwa sababu anafanya kazi kama bulldozer, nikimaanisha alihitaji mtu ambaye sio "impulsive" kumwongoza, kama ilivyokuwa kwa Nyerere na Sokoine. Baadaye nilishangaa kuona jina Bulldozer limemnasa Magufuli.

Sasa nitawaambia jambo jingine. Tanzania tumegawanyika kwa sasa, pro na against Magufuli. Huko nyuma nilisema pia Tanzania ilikuwa imefikia pabaya sana na hivyo labda ilikuwa vema na wakati muafaka kupata kiongozi wa namna ya Magufuli, angalau kwa miaka kumi. Lakini sasa najua kwamba miaka kumi haitatosha. Najua hii ni kauli ya kuleta hasira, lakini ndio ukweli wenyewe.

Hakuna Raisi duniani anaweza kuibadilisha nchi toka alipoikuta Magufuli kwa kipindi cha miaka kumi tu. Na hatari ya miaka kumi ni kwamba raisi atakayefuata anaweza kuharibu mazuri yote yaliyofanywa, kwa sababu yale mazuri yanakuwa hayajaota mizizi sawasawa (established sustainable systems). Na hiyo ni ukweli wa-kishule (academic truth) kwamba ili nchi iendelee inahitaji mipango ya muda mrefu isimamiwe na mtu ambaye yuko committed kuisimamia (committed leadership to implement strategic national development plans). Hakuna mpango wa muda mrefu wa kuiendeleza nchi utakaotekelezwa chini ya miaka kumi. Huo ndio ukweli wenyewe.

Ukiangalia historia ya mataifa yaliyoendelea haraka chini ya viongozi wao maarufu, utaona kwamba mafanikio ya nchi hizo hayakuletwa na viongozi waliobadilisha hizo nchi katika kipindi cha miaka kumi tu. Mifano mizuri ni Singapore, Malaysia na hata Rwanda. Singapore kwa mfano, kuna wakati fulani kiongozi wao alilalamikiwa, na hata kukasirikiwa kwa maamuzi magumu aliyofanya, lakini angalia alipoifikisha Singapore, toka taifa masikini sana. Ilimchukua miaka zaidi ya kumi kufanikisha hilo. Malaysia ni hivyo hivyo na Rwanda ndiko wanakoelekea.

Huwezi kuilinganisha Tanzania na nchi kama Marekani, ambao tayari wana "established systems" ambazo hazihitaji raisi mzuri kukaa madarakani zaidi ya miaka nane. Na mie ni wa kwanza kukubali kwamba ukiweka utarataibu wa kutokuwa na kikomo cha uraisi kabla hujampata Raisi mzalendo kama Nyerere au Magufuli, hatari ni kwamba unaweza kumpa nafasi raisi fisadi au mbovu akaharibu sana nchi. Mifano ya nchi za namna hiyo ipo mingi imetuzunguka.

Lakini sasa tunajua Magufuli ni mtu wa namna gani. Yapo ambayo sikubaliani na Raisi Magufuli, na hata kumkasirikia mara nyingine. Lakini ni mengi zaidi ninayokubaliana naye, hasa katika kukabiliana na ufisadi na kuleta nidhamu ya uwajibikaji. Watanzania tulilala sana, tulifikia uozo mbaya sana. Niliwahi kuwaambia kuna mke wa raisi alimfokea kiongozi wa bandari kwa kukataa kuyatoa makontainer yake bila kuyalipia kodi. Aliitwa ikulu (na mke) na akaishia kuyatoa bila kupenda.

Na ukweli unabakia, kwamba, kama kweli Tanzania tunahitaji mabadiliko ya kutumia rasilimali zetu tuwe kama Singapore au Malaysia, basi mtu kama Magufuli anahitaji kuwa madarakani kwa zaidi ya miaka kumi. Najua hii ni lugha Watanzania wengi, na hasa vyama vya upinzani, hawawezi kuifurahia, lakini huo ndio ukweli. Baada ya hiyo miaka labda ishirini ya Magufuli, basi tunaweza kurudi tena kwenye uraisi wa kipindi cha miaka kumi au hata nane. Tutakuwa tayari tuna "established system" huenda hata kwa kiwango cha Singapore. Kama ikibidi vyama vya upinzani kuungana na CCM kwa sasa ili kufanikisha hilo basi na iwe hivyo.

NB: Naomba niweke wazi kwamba thread hii nimeiweka katika context ya strategic national development, na sio ushabiki wa kisiasa. Nimetukanwa sana humu kwa kumkosoa Magufuli, na bado msimamo wangu ni kwamba kuna mazuri sana anayofanya Magufuli, na pia yapo mabaya sana anayofanya. Mie siko CCM wala upinzani. I just call a spade - spade.
Miaka kumi is more than enough msilete mambo yasiyonatija. Urais ni miaka kumi au vipindi viwili, waliotangulia wangebadili katiba tusingekuwa na rais mpendwa JPM na baada ya miaka yake kumi anaweza kuja rais mwingine mzuri zaidi au tofauti yake. Tufuate katiba tu
 
Kwa mtazamo wangu nahic strategic development plans limekaa vizuri sawa lakini pia kama nchi tuwe na a very strict implemented LONG TERM & SHORT TERM DEVELOPMENT PLANS with very clear implemented & articulated VISION and MISSION ambazo hazina budi kutekelezwa regardless ni awamu ipi imeshika hatamu ya madaraka.

Point yangu ya msingi hapa ni kwamba hata kama Magufuli muda wake utakuwa umekwisha baada ya miaka yake kumi basi atakaefata alazimike kuanzia alipoachia mtangulizi wake na hata manifesto ( ILANI ) za chama wakati wa uchaguzi zianishe hivyo.

Sio kama ilivyo sasa kwa mfano Kikwete alipenda sana kilimo kwanza japo efforts zake hazikutosha baadae akahamia kwenye BRN lakini wakati wa uchaguzi manifesto ya chama ikaja na falsafa ya TANZANIA YA VIWANDA kama agenda kuu badala ya kuendeleza falsafa ya kilimo kwanza au dhana ya BRN ( BIG RESULTS NOW) hadi outputs infact positive outputs zionekane. Matokeo yake ni kwamba kilimo kwanza hakuna tena na BRN imetupiliwa mbali.

Tukichukulia mfano wa jirano yetu Kenya mwaka 2009/2010 kama sijakosea walikuja na agenda au mkakati wa maendeleo "KENYA TOWARDS VISION 2030" ambao utekelezaji wake ulianza chini ya rais Kibaki na matakeo yake yakaanza kuonekana lakini hata baada ya utawala wake kuisha na kuingia utawala wa Kenyatta wanaendeleza malengo na mkakati wa kimaendeleo wa VISION 2030.

Hii inasaidia sana katika kuendeleleza mkakati wa mipango ya maendeleo kuanzia pale ulipokomea utawala mmoja hadi kupokelewa na utawala unaofata successfully ( SUCCESSFUL RESSESSION)
 
Kama hujaona jema lilifanywa na Nyerere kujibizana na wewe ni kupoteza muda.Ni kweli yako mabaya aliyoyatenda.Akili timamu hupima kati ya mema na mabaya kuangalia upande upi una uzito.Akili timamu pia hufuatilia chanzo cha ubaya ulifanyika na lengo la tendo hilo.

Baada ya Nyerere wamepita Mzee Mwinyi,Mkapa,Kikwete na sasa Magufuri kati yao hakuna anayekaribia hata 50% ya aliyoyafanya.

Unamtaja na Mugabe huoni wala hujui alichokifanya.Ni mpuuzi tu ambaye anaweza kuona ni akili kubwa Mugabe akabidhi Zimbabwe kwa Tsvangirai na ategemee walio wengi Zimbabwe wanufaike na mabadiliko hayo.Unaijua vizuri historia ya Zimbabwe kuanzia kipindi cha kupigania uhuru,ahadi za Waingereza kwa wananchi wa Zimbabwe kuhusiana na ardhi na utekelezaji wake? Kama unajua huna tofauti na Tsavangirai,unatamani uwatumikishe raia wa nchi yako kwa maslahi ya wanaokulipa.Hufai kwa M
Hao wote waliwatunishia misuli mabwana zao wanaowalisha na kuwapa uwezo wa kila kitu. Mwisho wa siku mzee mchonga alipoona jahazi linazama akasema nang'atuka.

Aliona kwamba ule mpambano wake na mabwana wakubwa ameshindwa na iwe isiwe lazima tufuate sera zao ambazo yeye alizikataa hadharani na kwavitendo. Aliona ataumbuka, akakaa pembeni. Wakati huo ukikutwa na dola 100 wewe ni muhujumu uchumi(kwa sasa utaitwa mtakatishaji).

Tv alikiwa nayo yeye akiona matukio anaamka asubihi kwamba ameoteshwa, kumbe anapiga changa la macho. Mwenzake Mandela aliwahi kusema elimu ndio silaha makini yakupigana na umasikini wetu, je wasomi walikuwa na nafasi gani kwake?

Hatuwezi kujifanya wajuaji saana wakati tunategemea kila kitu cha mzungu, ni upumbavu. Unaamka unasema kesho tutakuwa donor country baada ya wiki unaomba mikopo na misaada ya kujenga miundombinu. Unamtunishia nani misuli ilhali bajeti yako hata robo huwezi kuifikisha kwa pesa zako?

Mugabe naye aliwatunishia mabwana wakubwa misuli kilichotokea hali mbaya kwa wananchi yeye anakula bata na ufalme wake. Mkate dola milioni tano. Kama hujajipanga usiwe mwehu kutukana mamba na mto hujavuka.
 
Nchi inaongozwa kwa katiba au matakwa ya mtu.Magufuli na nyerere nani ni mzuri zaidi?Kama ni nyerere nbona alitawala miaka 24 lakini hamna lolote?
 
Miaka kumi is more than enough msilete mambo yasiyonatija. Urais ni miaka kumi au vipindi viwili, waliotangulia wangebadili katiba tusingekuwa na rais mpendwa JPM na baada ya miaka yake kumi anaweza kuja rais mwingine mzuri zaidi au tofauti yake. Tufuate katiba tu
Mkuu, ni katiba hiii hii ilitupa uozo wa viongozi waliopita. Hivyo basi, sometimes Tanzania inapaswa kuwa kubwa kuliko hata hiyo katiba. Itatusaidia nini ikiwa tunafuata katiba ili tuwe na viongozi wazembe na mafisadi au wasioonea haya ufisadi? Mikataba mibovu tunayotaka sana kubadilisha na wizi wa kutisha uliokuwapo nchini tulivipata chini ya viongozi walioingia madarakani kwa kufuata katiba. Lakini ili tusiji-contradict, tunaweza tukabadili katiba ili tuifuate badala ya kuivunja!

In fact, kwangu mimi, kama ninaona wapinzani hawana uwezo wa kushinda uchaguzi, then ni afadhali Magufuli aendelee. Better the Magufuli whose flaws I now know kuliko fisadi mwingine mpya kutoka CCM aje kuturudisha nyuma tunakotaka kukimbia. Thrice bitten (Mwinyi, Mkapa, JK) should be six times shy. I have just reached a point sijui CCM wanaweza kutoa garbage gani tena kama president. As such, I would rather have Magufuli continue and avoid that risk. Lakini singependa kabisa wapinzani washindwe kwa sababu Magufuli kawahujumu na kuwanyanyasa.
 
Sijui hata niseme nini ila Nyerere alikaa madarakani kwa muda upi? Yeye hakuwa na agenda ya strategic national development?

Ni nini kilitokea baada ya yeye kutoka madarakani?

Fair enough tuseme Magufuli ni visionary mkubwa kumshinda Nyerere akiondoka baada ya hiyo miaka unayotaka kumpa kitafuatia nini akiingia mtu kama Mkwere?
 
Nchi inaongozwa kwa katiba au matakwa ya mtu.Magufuli na nyerere nani ni mzuri zaidi?Kama ni nyerere nbona alitawala miaka 24 lakini hamna lolote?

Nimemuuliza mwenzako mmoja hapo nyuma, kuwa wewe unayesema Nyerere alitawala miaka 24 na hatukuona mabadiliko ulizaliwa mwaka gani, hata usielewe tofauti ya Tanzania/Tanganyika, tulipopata uhuru mwaka 1961, na Nyerere alipostaafu mwaka 1985. Hata nikasema kama sio Nyerere huenda usingezaliwa kwa kuwa wazazi wako labda wangekufa kwa utapiamlo au matatizo mengine utotoni, au kwa kushindwa kutibiwa kwa sababu babu zako hawakuweza kumudu gharama za matibabu na chanjo kwa ajili ya hao waliokuja kuwa baba na mama yako.
 
Sijui hata niseme nini ila Nyerere alikaa madarakani kwa muda upi? Yeye hakuwa na agenda ya strategic national development?

Ni nini kilitokea baada ya yeye kutoka madarakani?

Fair enough tuseme Magufuli ni visionary mkubwa kumshinda Nyerere akiondoka baada ya hiyo miaka unayotaka kumpa kitafuatia nini akiingia mtu kama Mkwere?

Maswali mazuri sana Mkuu. Leo hii, Marekani au hata South Afrika, anaweza kuingia Mkwere na bado nchi isitetereke, kwa sababu imeshajenga momentum/resilience ya ku-absorb ukwere wowote utakaoletwa na raisi Mkwere kwa kipindi cha miaka minane ya uraisi kikatiba. Hicho ndicho ningependa Magufuli aifanyie Tanzania - kumpa nafasi ya kujenga momentum au resilience ya Tanzania kiuchumi na kidesturi (culture) katika uwajibikaji. Na hicho pia ndicho kilifanyika katika nchi kama South Korea na Singapore. Hazikubadilika kwa viongozi kukaa miaka minane au kumi ya kikatiba. Ila sasa zina momentum/resilience ya kutosha kuweka utaratibu wa miaka nane au kumi, na kuhimiri ukwere wowote utakaotokea katika kipindi hicho.

Hivi unajua Tanzania kuna wakati watu walikuwa wanaenda ofisini kupiga soga, kunywa chai na kupiga simu ya ofisi na kurudi nyumbani? I believe Magufuli ana silka ya kubadili hii culture mbovu sana ambayo tuliipata katika awamu moja tu ya kikatiba ya miaka 10. Na tunaongelea zaidi ya miaka kumi kwa kuwa ni rahisi kujenga culture mbaya katika miaka kumi kuliko kuiondoa katika miaka kumi.
 
Huwa najitahidi kuongea ukweli, japo mara nyingine watu wananikasirikia. Nakumbuka mapema sana, kabla hata jina Bulldozer halijajulikana kitaifa na kimataifa, nilisema humu JF Magufuli ni mchapa kazi sana, lakini labda ningependelea awe na nafasi ya Waziri Mkuu badala ya Raisi, kwa sababu anafanya kazi kama bulldozer, nikimaanisha alihitaji mtu ambaye sio "impulsive" kumwongoza, kama ilivyokuwa kwa Nyerere na Sokoine. Baadaye nilishangaa kuona jina Bulldozer limemnasa Magufuli.

Sasa nitawaambia jambo jingine. Tanzania tumegawanyika kwa sasa, pro na against Magufuli. Huko nyuma nilisema pia Tanzania ilikuwa imefikia pabaya sana na hivyo labda ilikuwa vema na wakati muafaka kupata kiongozi wa namna ya Magufuli, angalau kwa miaka kumi. Lakini sasa najua kwamba miaka kumi haitatosha. Najua hii ni kauli ya kuleta hasira, lakini ndio ukweli wenyewe.

Hakuna Raisi duniani anaweza kuibadilisha nchi toka alipoikuta Magufuli kwa kipindi cha miaka kumi tu. Na hatari ya miaka kumi ni kwamba raisi atakayefuata anaweza kuharibu mazuri yote yaliyofanywa, kwa sababu yale mazuri yanakuwa hayajaota mizizi sawasawa (established sustainable systems). Na hiyo ni ukweli wa-kishule (academic truth) kwamba ili nchi iendelee inahitaji mipango ya muda mrefu isimamiwe na mtu ambaye yuko committed kuisimamia (committed leadership to implement strategic national development plans). Hakuna mpango wa muda mrefu wa kuiendeleza nchi utakaotekelezwa chini ya miaka kumi. Huo ndio ukweli wenyewe.

Ukiangalia historia ya mataifa yaliyoendelea haraka chini ya viongozi wao maarufu, utaona kwamba mafanikio ya nchi hizo hayakuletwa na viongozi waliobadilisha hizo nchi katika kipindi cha miaka kumi tu. Mifano mizuri ni Singapore, Malaysia na hata Rwanda. Singapore kwa mfano, kuna wakati fulani kiongozi wao alilalamikiwa, na hata kukasirikiwa kwa maamuzi magumu aliyofanya, lakini angalia alipoifikisha Singapore, toka taifa masikini sana. Ilimchukua miaka zaidi ya kumi kufanikisha hilo. Malaysia ni hivyo hivyo na Rwanda ndiko wanakoelekea.

Huwezi kuilinganisha Tanzania na nchi kama Marekani, ambao tayari wana "established systems" ambazo hazihitaji raisi mzuri kukaa madarakani zaidi ya miaka nane. Na mie ni wa kwanza kukubali kwamba ukiweka utarataibu wa kutokuwa na kikomo cha uraisi kabla hujampata Raisi mzalendo kama Nyerere au Magufuli, hatari ni kwamba unaweza kumpa nafasi raisi fisadi au mbovu akaharibu sana nchi. Mifano ya nchi za namna hiyo ipo mingi imetuzunguka.

Lakini sasa tunajua Magufuli ni mtu wa namna gani. Yapo ambayo sikubaliani na Raisi Magufuli, na hata kumkasirikia mara nyingine. Lakini ni mengi zaidi ninayokubaliana naye, hasa katika kukabiliana na ufisadi na kuleta nidhamu ya uwajibikaji. Watanzania tulilala sana, tulifikia uozo mbaya sana. Niliwahi kuwaambia kuna mke wa raisi alimfokea kiongozi wa bandari kwa kukataa kuyatoa makontainer yake bila kuyalipia kodi. Aliitwa ikulu (na mke) na akaishia kuyatoa bila kupenda.

Na ukweli unabakia, kwamba, kama kweli Tanzania tunahitaji mabadiliko ya kutumia rasilimali zetu tuwe kama Singapore au Malaysia, basi mtu kama Magufuli anahitaji kuwa madarakani kwa zaidi ya miaka kumi. Najua hii ni lugha Watanzania wengi, na hasa vyama vya upinzani, hawawezi kuifurahia, lakini huo ndio ukweli. Baada ya hiyo miaka labda ishirini ya Magufuli, basi tunaweza kurudi tena kwenye uraisi wa kipindi cha miaka kumi au hata nane. Tutakuwa tayari tuna "established system" huenda hata kwa kiwango cha Singapore. Kama ikibidi vyama vya upinzani kuungana na CCM kwa sasa ili kufanikisha hilo basi na iwe hivyo.

NB: Naomba niweke wazi kwamba thread hii nimeiweka katika context ya strategic national development, na sio ushabiki wa kisiasa. Nimetukanwa sana humu kwa kumkosoa Magufuli, na bado msimamo wangu ni kwamba kuna mazuri sana anayofanya Magufuli, na pia yapo mabaya sana anayofanya. Mie siko CCM wala upinzani. I just call a spade - spade.

Nchi haibadilishwi na muhula mmoja au miwili ya uongozi - maana kubadilika ni mchakato endelevu. Mchango wa viongozi waliomtangulia, mchango wake na michango ya viongozi wengine watakaofuata na ushirikiano wao na wasaidizi wao na wananchi wote - kwa pamoja ndiko huwa kunaleta hayo mabadiliko. Ila kitu ambacho kingerahisisha mabadiliko ni Katiba Mpya (walau kwa kuanzia na ile ya Warioba).
 
Acheni uchuro rudisheni rasimu ya tume ya Warioba tupate Tanzania mpya na sio hivi vitimbi vya masakuu.
 
Nchi haibadilishwi na muhula mmoja au miwili ya uongozi - maana kubadilika ni mchakato endelevu. Mchango wa viongozi waliomtangulia, mchango wake na michango ya viongozi wengine watakaofuata na ushirikiano wao na wasaidizi wao na wananchi wote - kwa pamoja ndiko huwa kunaleta hayo mabadiliko. Ila kitu ambacho kingerahisisha mabadiliko ni Katiba Mpya (walau kwa kuanzia na ile ya Warioba).

Mkuu, ni kweli, lakini hilo linawezekana katika nchi iliyoendelea tayari. Nchi kama Norway it does not matter nani anakuwa raisi kwa kuwa raisi anaingia pale kwa ajili ya kusimamia, sio kuendeleza nchi.

Katika nchi changa kama Tanzania, ili nchi iendelee, unahitaji kufanya strategic planning. Strategic planning haiwezi kuwa ya miaka mitano au kumi. Inakuwa ya kuanzia miaka 15 hadi 50. Sasa ikiwa raisi anajua kuwa atakuwa na miaka 10 tu, thinking yake inakuwa confined kwenye timeframe ya miaka 10 - atafanya nini katika kipindi cha miaka 10. Sasa mambo ya kufanya katika miaka 10 mara nyingi sio mambo ya kuleta maendeleo ya muda mrefu au ya kudumu sana. In fact, mara nyingi lead time za project au mikakati mikubwa ya maendeleo ni kuanzia miaka 5 hadi 20.

Kwa mfano, leo Magufuli anaweza hata kuja na development strategy ya miaka 20, akaja mtu mwingine kama raisi baada ya miaka 5 au 10 akaifutilia mbali na akataka iwepo ya kwake. Mind you, huyo mtu sio lazima abadilishe development strategy ya Magufuli kwa sababu anatoka upinzani, anaweza kuwa wa kutoka CCM pia. Vipao mbele vya maendeleo vya Magufuli sio vipao mbele vya Kassim Majaliwa, au hata Mwigulu Nchemba. Hizi ilani za vyama vya siasa si mali kitu - mara nyingi zina mambo madogo madogo sana ambayo hayana impact kubwa kwa uchumi.

Na of course, upande wa pili ni raisi kuwa na muda wa kutosha kujenga culture na descipline ya uwajibikaji katika nchi, kama nilivyosema hapo juu, kuua tabia kama za watu kwenda ofisini kupiga soga, kuiba stationery za ofisi, kutoa photocopy na kuprint document binafsi au kama biashara, kunywa chai ya ofisi na kupiga simu binafsi kwa gharama za serikali. Watanzania ndipo tulifikia hapo. Watu walikuwa wanaenda, na bado wanaenda, ofisini sana sana kufanya hayo, na wanalipwa mishahara.
 
Nakuapia magufuli hata miaka mia moja hataibadilisha nchi
 
Back
Top Bottom