Good point Mkuu. Labda suala la msingi ni kwamba miswaada mizuri ndio tatizo la nchi hii? Angalia South Africa, ni ncho mojawapo ambayo watu watasema ina one of the best constitutions in the world, na pia hata policies na regulatory frameworks. Lakini zinawasaidia? Je uwepo wa raisi Jacob Zuma katika mazingira ya consitution na policies nzuri umeifikisha wapi South Africa?Kama tunaweza kupeleka miswada mitatu kwa ''hati ya dharura'' na kuipitisha ndani ya siku tatu, anahitaji kweli miaka 10 yote ''kuibadirisha'' Tanzania? does he even know what he needs to change (kubadilisha) anyway? Kama tunamuona yeye kama Messiah na tunadhani anaweza kubadilisha vitu vingi individually bila kuwa na institutions imara, then we are doomed for life and we deserve to be so.
Najua tayari mlishapangwa watu wa kueneza hii propaganda ili ishike. Kama ww ndiye uliyeona Tanzania nzima kiongozi anayefaa ni mmoja tu na ni huyo kati ya watu million 50, huo ndiyo mwisho wa uwezo wako wa kufikiri, na upeo wako. Kwa maana hiyo akili zako ndiyo zimegota hapo na huwezi fikiri mbele zaidi. Sorry bahati mbaya sana katiba haimruhusu na ni jambo ambalo haliwezekani hata kama mkijipanga vipi. Hiyo ni ndoto ya alinacha.
ilani inaweza kuwepo, lakini ikakosa kiongozi mwenye nia ya dhati ya kuisimamia utekelezaji wa ilani hio. CCM imekua madarakani muda mrefu, na kwa kipindi chote hiko kumekuwepo na ilani, lakini kasi ya utekelezaji wa ilani ya CCM kwa wakati huu imekua ni ya kuridhisha sana.Unajua kazi ya Ilani ?
Tuanzie hapo kwanza.
Nikirudi kwako Mkuu Pascal, naona watu humu JF wanataka ukimuunga mkono Magufuli kwa jambo fulani, basi unatakiwa uwe na mapenzi naye 100% na kuunga mkono kila anachofanya, hata yale yenye kuudhi sana.Naunga mkono hoja na hili na mimi pia niliwahi kulizungumzia na nikapendekeza tumpe angalau vipindi 4 vya miaka mitano mitano na kusiwe na uchaguzi wa rais ili kubana matumizi.
Kwa Kasi hii ya Magufuli, kuna haja Kufanya Uchaguzi wa Rais 2020?
Nilisema hivi
Pascal
Tumepunguza walipa kodi serikaliniKama hujui kuna faida gani kiuchumi wanapoondolewa wafanyakazi hewa. Kwanini nisikuite hopeless hater.
ni kweli kila mtu ana mawazo yake, pia kila mtu anaruhusiwa kutia mchango wake ili kuleta maendeleo. Tunapoongelea kwa nafasi hii ya Urais ni vyema kumpa nafasi mtu mmoja tunaemuamini akaweka misingi imara, misingi hii imara haiwezi kuwekwa an kuimarika ndani ya kipindi cha miaka 10, huu ndio ukweli.hatuwezi kuendelea kwa kunyamazisha mawazo ya watu wengine na kumtazama mtu mmoja. kila mtu ana mchango wake katika maendeleo hivo kila mtu apewe nafasi.
mkuu unauhakika gani kwamba miaka 10 inatosha? tunajifunza kutoka kwa nchi zilizofanikiwa, tunaona kwamba huko nyuma zilitumia zaidi ya mika 10 kujenga mifumo na misingi ya uendeshaji serikali.We don't need one man show or a strong man, we need strong government systems. Miaka 5 au 10 inatosha sana kuweka system imara. Bahati mbaya naona hata hizo system dhaifu zilizokuwepo kama zinazidi kuwa mfu. Sasa sijui ni indicators gani unazotumia kutoa miaka zaidi ya 10.
Kwani huyu mtu hatakufa? Kwanini tunaweka imani yetu kwa mtu mmoja. Huyu jamaa ni empty set na wote wanaomsapoti
Hahaha! I say, JF mara nyingine ni burudani tosha kabisa. Acha fujo Mkuu.Tumepunguza walipa kodi serikalini
Swali gani sasa hili? Hivi huwezi kuelewa kwamba mipango ya nchi ni zaidi ya ilani na kusimamia ni kiongozi anayesemwa hapa?Unajua kazi ya Ilani ?
Tuanzie hapo kwanza.
Hivi mali za lowasa ni zipiBora ubinafsi wa kujenga uwanja kuliko ubinafsi wa kujilimbikizia mali kama lowassa
Mpaka sasa kafeli. Urais sio kama baba jinsi anavyoongoza familia yake.
Urais ni taasisi inayoshirikiana kikamilifu na taasisi nyingine kama Bunge na Mahakama tukeleza katiba ya nchi.
JPM angeweza kulifanya bunge kuwa huru na yeye kutekeleza yale yanatopendekezwa bungeni basi tungekua mbali.
Tatizo lake anataka kila kitu afanye yeye,kodi za ajabu zilizoanzishwa ndio zimekausha bandari. Wakati anajua bandari inachangia zaidi ya 50% ya pato la nchi. Kwenye utalii nako kavuruga,kaweka kodi zisizokua na nyuma wala mbele. Kaachana na kilimo anakimbilia viwanda,hivi kuna nchi imeendelea kiviwanda bila ya kuwekeza kwanza kwenye kilimo? Kama ipo naomba jibu.
Uyu kafeli na hawezi kutufikisha kokote zaidi ya kuharibu nchi tu.
Mahakama si ipoKuna mtanzania gani asiyejua kuwa lowassa ni miongoni mwa mafisadi wa nchi hii hata mtoto wa darasa la 4 ukimpa swali linalohusu ufisadi anamtaja lowassa
Nina wasiwasi na vyeti vyakoUsi ishie kwenye manenu tuu, hakuna faida ya moja kwa moja na hao wafanyakazi hewa wako karibu kila nchi huwa hawaishi kwa kuwa bureaucracy ina wajanja wengi.
Wabongo acheni kujidanganya katika histria ya Dunia vitu anavo vifanya magufuli havija wahi kuleta maendeleo mcheki mwenzie buhari mbona ana feli!!?
Mi siwez kumchukia Rais wa nchi maana najua akifeli yeye nchi nzima ita feli so usiniseme kwa maneno nipe ushahidi in real life kiongozi gani aliwahi fanya kama Magufuli halafu aka fanikisha maendeleo makubwa ya ki uchumi.
Baada ya miaka 20 rika la hawa mafisadi litakuwa limetoweka na vijana watakaotawala watakuwa wamezoea nidhamu ya kazi na uadilifu. Hapo tunaweza kurudisha utawala wa awamu 2.Huwa najitahidi kuongea ukweli, japo mara nyingine watu wananikasirikia. Nakumbuka mapema sana, kabla hata jina Bulldozer halijajulikana kitaifa na kimataifa, nilisema humu JF Magufuli ni mchapa kazi sana, lakini labda ningependelea awe na nafasi ya Waziri Mkuu badala ya Raisi, kwa sababu anafanya kazi kama bulldozer, nikimaanisha alihitaji mtu ambaye sio "impulsive" kumwongoza, kama ilivyokuwa kwa Nyerere na Sokoine. Baadaye nilishangaa kuona jina Bulldozer limemnasa Magufuli.
Sasa nitawaambia jambo jingine. Tanzania tumegawanyika kwa sasa, pro na against Magufuli. Huko nyuma nilisema pia Tanzania ilikuwa imefikia pabaya sana na hivyo labda ilikuwa vema na wakati muafaka kupata kiongozi wa namna ya Magufuli, angalau kwa miaka kumi. Lakini sasa najua kwamba miaka kumi haitatosha. Najua hii ni kauli ya kuleta hasira, lakini ndio ukweli wenyewe.
Hakuna Raisi duniani anaweza kuibadilisha nchi toka alipoikuta Magufuli kwa kipindi cha miaka kumi tu. Na hatari ya miaka kumi ni kwamba raisi atakayefuata anaweza kuharibu mazuri yote yaliyofanywa, kwa sababu yale mazuri yanakuwa hayajaota mizizi sawasawa (established sustainable systems). Na hiyo ni ukweli wa-kishule (academic truth) kwamba ili nchi iendelee inahitaji mipango ya muda mrefu isimamiwe na mtu ambaye yuko committed kuisimamia (committed leadership to implement strategic national development plans). Hakuna mpango wa muda mrefu wa kuiendeleza nchi utakaotekelezwa chini ya miaka kumi. Huo ndio ukweli wenyewe.
Ukiangalia historia ya mataifa yaliyoendelea haraka chini ya viongozi wao maarufu, utaona kwamba mafanikio ya nchi hizo hayakuletwa na viongozi waliobadilisha hizo nchi katika kipindi cha miaka kumi tu. Mifano mizuri ni Singapore, Malaysia na hata Rwanda. Singapore kwa mfano, kuna wakati fulani kiongozi wao alilalamikiwa, na hata kukasirikiwa kwa maamuzi magumu aliyofanya, lakini angalia alipoifikisha Singapore, toka taifa masikini sana. Ilimchukua miaka zaidi ya kumi kufanikisha hilo. Malaysia ni hivyo hivyo na Rwanda ndiko wanakoelekea.
Huwezi kuilinganisha Tanzania na nchi kama Marekani, ambao tayari wana "established systems" ambazo hazihitaji raisi mzuri kukaa madarakani zaidi ya miaka nane. Na mie ni wa kwanza kukubali kwamba ukiweka utarataibu wa kutokuwa na kikomo cha uraisi kabla hujampata Raisi mzalendo kama Nyerere au Magufuli, hatari ni kwamba unaweza kumpa nafasi raisi fisadi au mbovu akaharibu sana nchi. Mifano ya nchi za namna hiyo ipo mingi imetuzunguka.
Lakini sasa tunajua Magufuli ni mtu wa namna gani. Yapo ambayo sikubaliani na Raisi Magufuli, na hata kumkasirikia mara nyingine. Lakini ni mengi zaidi ninayokubaliana naye, hasa katika kukabiliana na ufisadi na kuleta nidhamu ya uwajibikaji. Watanzania tulilala sana, tulifikia uozo mbaya sana. Niliwahi kuwaambia kuna mke wa raisi alimfokea kiongozi wa bandari kwa kukataa kuyatoa makontainer yake bila kuyalipia kodi. Aliitwa ikulu (na mke) na akaishia kuyatoa bila kupenda.
Na ukweli unabakia, kwamba, kama kweli Tanzania tunahitaji mabadiliko ya kutumia rasilimali zetu tuwe kama Singapore au Malaysia, basi mtu kama Magufuli anahitaji kuwa madarakani kwa zaidi ya miaka kumi. Najua hii ni lugha Watanzania wengi, na hasa vyama vya upinzani, hawawezi kuifurahia, lakini huo ndio ukweli. Baada ya hiyo miaka labda ishirini ya Magufuli, basi tunaweza kurudi tena kwenye uraisi wa kipindi cha miaka kumi au hata nane. Tutakuwa tayari tuna "established system" huenda hata kwa kiwango cha Singapore. Kama ikibidi vyama vya upinzani kuungana na CCM kwa sasa ili kufanikisha hilo basi na iwe hivyo.
NB: Naomba niweke wazi kwamba thread hii nimeiweka katika context ya strategic national development, na sio ushabiki wa kisiasa. Nimetukanwa sana humu kwa kumkosoa Magufuli, na bado msimamo wangu ni kwamba kuna mazuri sana anayofanya Magufuli, na pia yapo mabaya sana anayofanya. Mie siko CCM wala upinzani. I just call a spade - spade.
Mkuu salaam,NB: Naomba niweke wazi kwamba thread hii nimeiweka katika context ya strategic national development, na sio ushabiki wa kisiasa. Nimetukanwa sana humu kwa kumkosoa Magufuli, na bado msimamo wangu ni kwamba kuna mazuri sana anayofanya Magufuli, na pia yapo mabaya sana anayofanya. Mie siko CCM wala upinzani. I just call a spade - spade.