Ili Magufuli aibadilishe Tanzania, ni lazima awe Rais kwa zaidi ya miaka kumi

Mwapachu wakati wa KAMPENI alisema mbio hizi za uchaguzi ni kati ya a leader akimaanisha lowasa and a manager akimaanisha magu....wengi hawakumuelewa ...natumai sasa mwapachu anaeleweka vizuri sana.
OK, hakuna ubaya kama manager akitengeneza standard gauge ya umeme na leader akapita
..au ukawa wenzio kuandamana juu ya flyover za Tazara alizojenga manager kuelekea uwanja Wa ndege kwa mafuriko kumpokea leader
 
Wahi mapema na ushahidi huo...wenzako wameanzisha mahakama ya mafisadi na kesi hakuna....lowasa yupo hawana ushahidi...mahakimu na majaji wamesomea kuhukumu kesi fasta ila serikali imekosa watuhumiwa.
VP tundu lisu naye hana ushahidi?
 
All in all haijalishi wewe ni nani au ni shabiki wa nani. Solution ya kila kitu hapa ni katiba ya Warioba ikiongozana na kuwaondolea immunity watawala basi ili immunity iwe uaminifu na uadilifu ktk utendaji wake tu
Mkuu, Katiba ya Warioba ina nini chenye kuchochea uwajibikaji wa viongozi kwa ujumla? Kubwa tunalohitaji ili Tanzania iendelee ni kuondoa immunity ya kuwashitaki maraisi tu?

Huwezi kuweka culture kwenye katiba.
 
Mkuu, kufa ni suala jingine, na japo tunajua linaweza kutokea, katika positive na optimistic thinking huwa hatuliweki katika kupanga mambo, maana la sivyo unaweza usifanye kitu.

Kwa hiyo hata tunapomchagua mtu kuwa na nafasi fulani kwa ajili ya uwezo wake wa hali ya juu, huwa hatupangi akifa itakuwaje. We cross that bridge when it comes by.

Hvi umewahi kufikiri kwamba Magufuli akifa leo nani atakuwa president wa nchi? Do you think that is the best president Tanzania could have? Sasa sidhani kama CCM walifika mbali kiasi hicho. They just made the assumption we will have Magufuli as the president for the next five or ten years.
Ndo ujinga huo lazma ufikirie na lazma tuandae viongozi sio huyo apige than 5year in 2 terms
 
Huwa najitahidi kuongea ukweli, japo mara nyingine watu wananikasirikia. Nakumbuka mapema sana, kabla hata jina Bulldozer halijajulikana kitaifa na kimataifa, nilisema humu JF Magufuli ni mchapa kazi sana, lakini labda ningependelea awe na nafasi ya Waziri Mkuu badala ya Raisi, kwa sababu anafanya kazi kama bulldozer, nikimaanisha alihitaji mtu ambaye sio "impulsive" kumwongoza, kama ilivyokuwa kwa Nyerere na Sokoine. Baadaye nilishangaa kuona jina Bulldozer limemnasa Magufuli.

Sasa nitawaambia jambo jingine. Tanzania tumegawanyika kwa sasa, pro na against Magufuli. Huko nyuma nilisema pia Tanzania ilikuwa imefikia pabaya sana na hivyo labda ilikuwa vema na wakati muafaka kupata kiongozi wa namna ya Magufuli, angalau kwa miaka kumi. Lakini sasa najua kwamba miaka kumi haitatosha. Najua hii ni kauli ya kuleta hasira, lakini ndio ukweli wenyewe.

Hakuna Raisi duniani anaweza kuibadilisha nchi toka alipoikuta Magufuli kwa kipindi cha miaka kumi tu. Na hatari ya miaka kumi ni kwamba raisi atakayefuata anaweza kuharibu mazuri yote yaliyofanywa, kwa sababu yale mazuri yanakuwa hayajaota mizizi sawasawa (established sustainable systems). Na hiyo ni ukweli wa-kishule (academic truth) kwamba ili nchi iendelee inahitaji mipango ya muda mrefu isimamiwe na mtu ambaye yuko committed kuisimamia (committed leadership to implement strategic national development plans). Hakuna mpango wa muda mrefu wa kuiendeleza nchi utakaotekelezwa chini ya miaka kumi. Huo ndio ukweli wenyewe.

Ukiangalia historia ya mataifa yaliyoendelea haraka chini ya viongozi wao maarufu, utaona kwamba mafanikio ya nchi hizo hayakuletwa na viongozi waliobadilisha hizo nchi katika kipindi cha miaka kumi tu. Mifano mizuri ni Singapore, Malaysia na hata Rwanda. Singapore kwa mfano, kuna wakati fulani kiongozi wao alilalamikiwa, na hata kukasirikiwa kwa maamuzi magumu aliyofanya, lakini angalia alipoifikisha Singapore, toka taifa masikini sana. Ilimchukua miaka zaidi ya kumi kufanikisha hilo. Malaysia ni hivyo hivyo na Rwanda ndiko wanakoelekea.

Huwezi kuilinganisha Tanzania na nchi kama Marekani, ambao tayari wana "established systems" ambazo hazihitaji raisi mzuri kukaa madarakani zaidi ya miaka nane. Na mie ni wa kwanza kukubali kwamba ukiweka utarataibu wa kutokuwa na kikomo cha uraisi kabla hujampata Raisi mzalendo kama Nyerere au Magufuli, hatari ni kwamba unaweza kumpa nafasi raisi fisadi au mbovu akaharibu sana nchi. Mifano ya nchi za namna hiyo ipo mingi imetuzunguka.

Lakini sasa tunajua Magufuli ni mtu wa namna gani. Yapo ambayo sikubaliani na Raisi Magufuli, na hata kumkasirikia mara nyingine. Lakini ni mengi zaidi ninayokubaliana naye, hasa katika kukabiliana na ufisadi na kuleta nidhamu ya uwajibikaji. Watanzania tulilala sana, tulifikia uozo mbaya sana. Niliwahi kuwaambia kuna mke wa raisi alimfokea kiongozi wa bandari kwa kukataa kuyatoa makontainer yake bila kuyalipia kodi. Aliitwa ikulu (na mke) na akaishia kuyatoa bila kupenda.

Na ukweli unabakia, kwamba, kama kweli Tanzania tunahitaji mabadiliko ya kutumia rasilimali zetu tuwe kama Singapore au Malaysia, basi mtu kama Magufuli anahitaji kuwa madarakani kwa zaidi ya miaka kumi. Najua hii ni lugha Watanzania wengi, na hasa vyama vya upinzani, hawawezi kuifurahia, lakini huo ndio ukweli. Baada ya hiyo miaka labda ishirini ya Magufuli, basi tunaweza kurudi tena kwenye uraisi wa kipindi cha miaka kumi au hata nane. Tutakuwa tayari tuna "established system" huenda hata kwa kiwango cha Singapore. Kama ikibidi vyama vya upinzani kuungana na CCM kwa sasa ili kufanikisha hilo basi na iwe hivyo.

NB: Naomba niweke wazi kwamba thread hii nimeiweka katika context ya strategic national development, na sio ushabiki wa kisiasa. Nimetukanwa sana humu kwa kumkosoa Magufuli, na bado msimamo wangu ni kwamba kuna mazuri sana anayofanya Magufuli, na pia yapo mabaya sana anayofanya. Mie siko CCM wala upinzani. I just call a spade - spade.

I

Tatizo ni kwamba wanaoandaa viongozi sio wewe na mimi. Kwani wewe na mimi tulimwandaa Magufuli? Kwanza Magufuli kuwa raisi ilikuwa ni ajali tu. Hata yeye hakutegemea. Ndio maana kama vile ajali ilivyozaa Magufuli, tunaweza tukapata ajali nyingine ikazaa fisadi kama raisi, tukarudi kwenye worse condition kuliko hata kabla ya Magufuli.
 
Kuna ukweli kiasi fulani, lakini hawezi kufanya kazi peke yake. Hawezi kufanya kazi kwa kulazimisha watu wote wawaze kama yeye na wanaokataa anawachukia na kuwafukuza au/pamoja na kuwafungulia kesi. Hiyo siyo sifa ya kiongozi.
 
Huwa najitahidi kuongea ukweli, japo mara nyingine watu wananikasirikia. Nakumbuka mapema sana, kabla hata jina Bulldozer halijajulikana kitaifa na kimataifa, nilisema humu JF Magufuli ni mchapa kazi sana, lakini labda ningependelea awe na nafasi ya Waziri Mkuu badala ya Raisi, kwa sababu anafanya kazi kama bulldozer, nikimaanisha alihitaji mtu ambaye sio "impulsive" kumwongoza, kama ilivyokuwa kwa Nyerere na Sokoine. Baadaye nilishangaa kuona jina Bulldozer limemnasa Magufuli.

Sasa nitawaambia jambo jingine. Tanzania tumegawanyika kwa sasa, pro na against Magufuli. Huko nyuma nilisema pia Tanzania ilikuwa imefikia pabaya sana na hivyo labda ilikuwa vema na wakati muafaka kupata kiongozi wa namna ya Magufuli, angalau kwa miaka kumi. Lakini sasa najua kwamba miaka kumi haitatosha. Najua hii ni kauli ya kuleta hasira, lakini ndio ukweli wenyewe.

Hakuna Raisi duniani anaweza kuibadilisha nchi toka alipoikuta Magufuli kwa kipindi cha miaka kumi tu. Na hatari ya miaka kumi ni kwamba raisi atakayefuata anaweza kuharibu mazuri yote yaliyofanywa, kwa sababu yale mazuri yanakuwa hayajaota mizizi sawasawa (established sustainable systems). Na hiyo ni ukweli wa-kishule (academic truth) kwamba ili nchi iendelee inahitaji mipango ya muda mrefu isimamiwe na mtu ambaye yuko committed kuisimamia (committed leadership to implement strategic national development plans). Hakuna mpango wa muda mrefu wa kuiendeleza nchi utakaotekelezwa chini ya miaka kumi. Huo ndio ukweli wenyewe.

Ukiangalia historia ya mataifa yaliyoendelea haraka chini ya viongozi wao maarufu, utaona kwamba mafanikio ya nchi hizo hayakuletwa na viongozi waliobadilisha hizo nchi katika kipindi cha miaka kumi tu. Mifano mizuri ni Singapore, Malaysia na hata Rwanda. Singapore kwa mfano, kuna wakati fulani kiongozi wao alilalamikiwa, na hata kukasirikiwa kwa maamuzi magumu aliyofanya, lakini angalia alipoifikisha Singapore, toka taifa masikini sana. Ilimchukua miaka zaidi ya kumi kufanikisha hilo. Malaysia ni hivyo hivyo na Rwanda ndiko wanakoelekea.

Huwezi kuilinganisha Tanzania na nchi kama Marekani, ambao tayari wana "established systems" ambazo hazihitaji raisi mzuri kukaa madarakani zaidi ya miaka nane. Na mie ni wa kwanza kukubali kwamba ukiweka utarataibu wa kutokuwa na kikomo cha uraisi kabla hujampata Raisi mzalendo kama Nyerere au Magufuli, hatari ni kwamba unaweza kumpa nafasi raisi fisadi au mbovu akaharibu sana nchi. Mifano ya nchi za namna hiyo ipo mingi imetuzunguka.

Lakini sasa tunajua Magufuli ni mtu wa namna gani. Yapo ambayo sikubaliani na Raisi Magufuli, na hata kumkasirikia mara nyingine. Lakini ni mengi zaidi ninayokubaliana naye, hasa katika kukabiliana na ufisadi na kuleta nidhamu ya uwajibikaji. Watanzania tulilala sana, tulifikia uozo mbaya sana. Niliwahi kuwaambia kuna mke wa raisi alimfokea kiongozi wa bandari kwa kukataa kuyatoa makontainer yake bila kuyalipia kodi. Aliitwa ikulu (na mke) na akaishia kuyatoa bila kupenda.

Na ukweli unabakia, kwamba, kama kweli Tanzania tunahitaji mabadiliko ya kutumia rasilimali zetu tuwe kama Singapore au Malaysia, basi mtu kama Magufuli anahitaji kuwa madarakani kwa zaidi ya miaka kumi. Najua hii ni lugha Watanzania wengi, na hasa vyama vya upinzani, hawawezi kuifurahia, lakini huo ndio ukweli. Baada ya hiyo miaka labda ishirini ya Magufuli, basi tunaweza kurudi tena kwenye uraisi wa kipindi cha miaka kumi au hata nane. Tutakuwa tayari tuna "established system" huenda hata kwa kiwango cha Singapore. Kama ikibidi vyama vya upinzani kuungana na CCM kwa sasa ili kufanikisha hilo basi na iwe hivyo.

NB: Naomba niweke wazi kwamba thread hii nimeiweka katika context ya strategic national development, na sio ushabiki wa kisiasa. Nimetukanwa sana humu kwa kumkosoa Magufuli, na bado msimamo wangu ni kwamba kuna mazuri sana anayofanya Magufuli, na pia yapo mabaya sana anayofanya. Mie siko CCM wala upinzani. I just call a spade - spade.
Hivi ni kwanini wote wanazungumzia Magufuli kuongezewa miaka kinyume na katiba iliyopo hawakamatwi kwa uchochezi dhidi ya KATIBA ya JMT ambayo hata Magu aliapa kuilinda ?
Kama kweli tinachukia kauli za kichochezi hii ilitakiwa kuwa imefungwa watu miaka hata 80 Jela
 
We don't need one man show or a strong man, we need strong government systems. Miaka 5 au 10 inatosha sana kuweka system imara. Bahati mbaya naona hata hizo system dhaifu zilizokuwepo kama zinazidi kuwa mfu. Sasa sijui ni indicators gani unazotumia kutoa miaka zaidi ya 10.

Ameamuru sheria ya natural resources irudi bungeni na kutengenezwa upya ili Tanzania inufaike na maliasili yake.
Hiyo sheria ataondoka nayo huyo one man?
Sasa mikataba itapelekwa Bungeni. Huko nako ataenda kupeleka show yake? au akiondoka mikataba haitapelekwa tena bungeni?
Kuna vitu we must appreciate kuwa sasa tumepata RAIS.
 
Hatuitaji mtu mzuri tunaitaji mfumo mzuri utaotufanya kuwa wazuri kwa nchi yetu.
 
Huwa najitahidi kuongea ukweli, japo mara nyingine watu wananikasirikia. Nakumbuka mapema sana, kabla hata jina Bulldozer halijajulikana kitaifa na kimataifa, nilisema humu JF Magufuli ni mchapa kazi sana, lakini labda ningependelea awe na nafasi ya Waziri Mkuu badala ya Raisi, kwa sababu anafanya kazi kama bulldozer, nikimaanisha alihitaji mtu ambaye sio "impulsive" kumwongoza, kama ilivyokuwa kwa Nyerere na Sokoine. Baadaye nilishangaa kuona jina Bulldozer limemnasa Magufuli.

Sasa nitawaambia jambo jingine. Tanzania tumegawanyika kwa sasa, pro na against Magufuli. Huko nyuma nilisema pia Tanzania ilikuwa imefikia pabaya sana na hivyo labda ilikuwa vema na wakati muafaka kupata kiongozi wa namna ya Magufuli, angalau kwa miaka kumi. Lakini sasa najua kwamba miaka kumi haitatosha. Najua hii ni kauli ya kuleta hasira, lakini ndio ukweli wenyewe.

Hakuna Raisi duniani anaweza kuibadilisha nchi toka alipoikuta Magufuli kwa kipindi cha miaka kumi tu. Na hatari ya miaka kumi ni kwamba raisi atakayefuata anaweza kuharibu mazuri yote yaliyofanywa, kwa sababu yale mazuri yanakuwa hayajaota mizizi sawasawa (established sustainable systems). Na hiyo ni ukweli wa-kishule (academic truth) kwamba ili nchi iendelee inahitaji mipango ya muda mrefu isimamiwe na mtu ambaye yuko committed kuisimamia (committed leadership to implement strategic national development plans). Hakuna mpango wa muda mrefu wa kuiendeleza nchi utakaotekelezwa chini ya miaka kumi. Huo ndio ukweli wenyewe.

Ukiangalia historia ya mataifa yaliyoendelea haraka chini ya viongozi wao maarufu, utaona kwamba mafanikio ya nchi hizo hayakuletwa na viongozi waliobadilisha hizo nchi katika kipindi cha miaka kumi tu. Mifano mizuri ni Singapore, Malaysia na hata Rwanda. Singapore kwa mfano, kuna wakati fulani kiongozi wao alilalamikiwa, na hata kukasirikiwa kwa maamuzi magumu aliyofanya, lakini angalia alipoifikisha Singapore, toka taifa masikini sana. Ilimchukua miaka zaidi ya kumi kufanikisha hilo. Malaysia ni hivyo hivyo na Rwanda ndiko wanakoelekea.

Huwezi kuilinganisha Tanzania na nchi kama Marekani, ambao tayari wana "established systems" ambazo hazihitaji raisi mzuri kukaa madarakani zaidi ya miaka nane. Na mie ni wa kwanza kukubali kwamba ukiweka utarataibu wa kutokuwa na kikomo cha uraisi kabla hujampata Raisi mzalendo kama Nyerere au Magufuli, hatari ni kwamba unaweza kumpa nafasi raisi fisadi au mbovu akaharibu sana nchi. Mifano ya nchi za namna hiyo ipo mingi imetuzunguka.

Lakini sasa tunajua Magufuli ni mtu wa namna gani. Yapo ambayo sikubaliani na Raisi Magufuli, na hata kumkasirikia mara nyingine. Lakini ni mengi zaidi ninayokubaliana naye, hasa katika kukabiliana na ufisadi na kuleta nidhamu ya uwajibikaji. Watanzania tulilala sana, tulifikia uozo mbaya sana. Niliwahi kuwaambia kuna mke wa raisi alimfokea kiongozi wa bandari kwa kukataa kuyatoa makontainer yake bila kuyalipia kodi. Aliitwa ikulu (na mke) na akaishia kuyatoa bila kupenda.

Na ukweli unabakia, kwamba, kama kweli Tanzania tunahitaji mabadiliko ya kutumia rasilimali zetu tuwe kama Singapore au Malaysia, basi mtu kama Magufuli anahitaji kuwa madarakani kwa zaidi ya miaka kumi. Najua hii ni lugha Watanzania wengi, na hasa vyama vya upinzani, hawawezi kuifurahia, lakini huo ndio ukweli. Baada ya hiyo miaka labda ishirini ya Magufuli, basi tunaweza kurudi tena kwenye uraisi wa kipindi cha miaka kumi au hata nane. Tutakuwa tayari tuna "established system" huenda hata kwa kiwango cha Singapore. Kama ikibidi vyama vya upinzani kuungana na CCM kwa sasa ili kufanikisha hilo basi na iwe hivyo.

NB: Naomba niweke wazi kwamba thread hii nimeiweka katika context ya strategic national development, na sio ushabiki wa kisiasa. Nimetukanwa sana humu kwa kumkosoa Magufuli, na bado msimamo wangu ni kwamba kuna mazuri sana anayofanya Magufuli, na pia yapo mabaya sana anayofanya. Mie siko CCM wala upinzani. I just call a spade - spade.
Du! Ndio maana unatukanwa sana. Onyesha mifano ya viongozi waliokaa madarakani kwa muda mrefu wakaleta mabadiliko.
Eg, Nyerere aliyekaa madarakani miaka 25 alibadilisha nini? Mugabe amebadilisha nini Zimbabwe? Museveni?
Vinginevyo usituletee ujinga wako hapa
 
Nikirudi kwako Mkuu Pascal, naona watu humu JF wanataka ukimuunga mkono Magufuli kwa jambo fulani, basi unatakiwa uwe na mapenzi naye 100% na kuunga mkono kila anachofanya, hata yale yenye kuudhi sana.

Siku zote nitakuwa wa kwanza kusema Magufuli ana mambo mazuri sana anafanya kwa nchi hii, na pia ana mabaya sana anafanya kwa nchi hii.
Mkuu Synthesizer, kwanza naomba nianze kwa kukupongeza kwa kuwa ni mtu mkweli, open na genuine. Watu wa type hii humu jf tuko wachache mimi nikiwemo.

Rais Magufuli ni kweli anafanya mazuri mengi, hivyo kustahili kusifiwa na kupongezwa kwa mazuri yake, lakini yeye sio malaika hivyo kuna wakati anakosea, pale anapofanya makosa madogo madogo ya kibinaadamu, then tunaweza kumnyamazia na kuyamezea, lakini pale anapofanya makosa makubwa ambayo ni blunders, tusimyamazie, aambiwe kistaarabu na kiukweli sometimes ni msikivu. Pale rais anapokosea na kuambiwa kistaarabu kabisa "Mhe. Rais Hapa Umekosea" au "Kwenye Hili Umefanya Ndivyo Sivyo" then watu wa aina hii ndio watu wanaomsaidia rais kuliko hata wale wanaoshinda kutwa kucha kumpongeza kwa kila analofanya.

Miongoni mwa makosa madogo madogo ya Rais Magufuli ameyafanya ambayo hatuyapigii kelele sana, ni pamoja na makosa ya double standards kwenye utumbuaji, kuna watu wanatumbuliwa kwa kudhalilishwa akiwemo aliyekuwa Mkurugenzi wa Jiji, Wilson Kebwe na RC wa Shinyanga, Anne Kilango Malecela, kwa Kebwe it's too late, lakini kwa Kilango rais amebaini kosa lake and has made good from make good kwa kufidia na kutoa replacement.
Hili la utumbuaji usio sawia nimelisemea

https://www.google.com/url?sa=t&sou...ggZMAA&usg=AFQjCNFIkCPSsRpU1cKPee3qTc7unQ1ogw

https://www.google.com/url?sa=t&sou...ggZMAA&usg=AFQjCNEUAVa_N3L-cVfdWzDSMU24YpLb4w

Lakini pale rais Magufuli anapofanya makosa makubwa yakiwemo kuikanyaga katiba yetu, hatupaswi kumnyamazia!.

Mfano mzuri ni pale rais alipojikwaa na kuteua wabunge 6 kwenye uteuzi wa rais wakati katiba imeweka ceiling ya limit ya uteuzi wabunge wanaume mwisho ni watano tuu, hivyo baada ya kosa hili, alitengua nafasi ya mmoja wa wateule wake kwa kuteua ubolozi hivyo kustaafu ubunge automatically.

Lakini rais alipokanyaga katiba , tumepiga kelele sana na kumnyooshea vidole.

https://www.google.com/url?sa=t&sou...ggZMAA&usg=AFQjCNFDI-hDx2E3YOutkp1vX5wRE6smnw

https://www.google.com/url?sa=t&sou...ggiMAI&usg=AFQjCNHCWiaB3gLwAoGeEB-alY1uUKsNiw

https://www.google.com/url?sa=t&sou...ggyMAY&usg=AFQjCNFGkqYKDTXz0nDi45BQZ8meaiMnnQ

Humu JF ukimsifu rais kwa mazuri yake kisha ukaja kumkosoa kwa mabaya yake utanyooshewa kidole cha ukigeugeu, huna msimamo, kinyonga etc.
Paskali
 
Tutakuwa tayari tuna "established system" huenda hata kwa kiwango cha Singapore.

How?

Systems zitatoka mbinguni? Utakuwaje na established systems kama hazijengwi?

Magufuli anajenga system gani so far, standard gauge rail system?
 
Mkuu, simaanishi systems unazozisema wewe - infrastructure. Namaanisha organizational, administrative, legal na management systems.
 
Du! Ndio maana unatukanwa sana. Onyesha mifano ya viongozi waliokaa madarakani kwa muda mrefu wakaleta mabadiliko.
Eg, Nyerere aliyekaa madarakani miaka 25 alibadilisha nini? Mugabe amebadilisha nini Zimbabwe? Museveni?
Vinginevyo usituletee ujinga wako hapa
Mkuu, kama huoni alichobadilisha Nyerere toka Tanzania ya Watanzania waliotoka ukoloni hadi aliyoiacha alipostaafu, basi ni wazi una tatizo ambalo siwezi kukusaidia kwa kukuelewesha hapa. Unachoonyesha ni kuwa umefungwa nepi na kujinyea miaka mingi baada ya uhuru, halafu you dare ask Nyerere alileta mabadiliko gani kwa Tanzania. Bila Nyerere huenda wazazi wako wangekufa kwa utapiamulo na wala wewe usingekuwapo, usingezaliwa.

Na pia, ninapoongelea kukaa madarakani kwa muda mrefu na kuleta mabadiliko ninamaanisha kwa kiongozi ambaye ni mzalendo na mwenye nia njema na nchi yake, mwenye constructive vision. Unaniuliza mifano wakati kwenye thread nimekupa mifano, sasa unataka nikueleweje? Wapi nimesema kuwa kiongozi yeyote akikaa muda mrefu ataleta mabadiliko? Mobutu Seseseko wa Zaire alikaa miaka zaidi ya Nyerere - unamaanisha nilimaanisha mabadiliko kama aliyoleta Mobutu kwa Zaire? Mambo mengine bwana kama huna uwezo wa kujadili kaa kimya. Ooh, ndio maana unatukanwa. Nadhani umeona hao wanaotukana wana uelewa mdogo sana kwa kuwa humu JF hata uwe na elimu ya msingi darasa la nne unaruhusiwa kuchangia mada ya professor. Kwa hiyo matusi humu JF wala sioni ni tatizo. Na wewe unatukana naleta ujinga, lakini ukweli ni kwamba wanaotukana kama wewe ni wajinga wasio na shule kama wewe unavyojionyesha hapa. Wewe sio Kidamva, ni kidampa.
 
Hivi ni kwanini wote wanazungumzia Magufuli kuongezewa miaka kinyume na katiba iliyopo hawakamatwi kwa uchochezi dhidi ya KATIBA ya JMT ambayo hata Magu aliapa kuilinda ?
Kama kweli tinachukia kauli za kichochezi hii ilitakiwa kuwa imefungwa watu miaka hata 80 Jela
Mkuu, kama ikibidi Magufuli aongezewe muda, hawezi kuongezewa muda bila kubadilisha katiba. Believe me, kubadilisha katiba ili magufuli aongezewe muda ni kitu kidogo sana. Huenda kikao kimoja tu cha Bunge. Katiba haiko cast in iron my friend, sio msaafu ule. Usijikite sana katika kufikiri ni jambo ambalo haliwezekani. Na kumbuka BUnge lina wingi wa wabunge wa CCM ambao Magufuli anaweza kutumia watu wake watoe hilo pendekezo na likapita.

Katika Afrika, suala la kuongezewa au kutooneza muda wa vipindi vya uraisi ni raisi alieyepo madarakani anaamua, ili mradi anajua chama chake kitamuunga mkono. Au hukuona Rwanda?
 
Naunga mkono hoja na hili na mimi pia niliwahi kulizungumzia na nikapendekeza tumpe angalau vipindi 4 vya miaka mitano mitano na kusiwe na uchaguzi wa rais ili kubana matumizi.

Kwa Kasi hii ya Magufuli, kuna haja Kufanya Uchaguzi wa Rais 2020?
Nilisema hivi

Pascal

Kaka yangu Mayalla, mara kwa mara nimekuwa sikubaliani na comments zako kutokana na mtazamo finyu (sorry kutumia neno hili sina nia mbaya) wa kufiiri kuwa JPM is an angel from heaven. mmoja wa wana filosofia wa kiyunani Aristoti alisema a very weak society depends on a person but a very strong society depends on a system

JMP ana tatizo la kiufundi, anatamani kufanya mambo mazuri kwa kutumia wrong approach.
Huwezi kufanikisha jambo lolote katika jamii kwa kuwachukia watu fulani ndani ya jamii.
JPM ame amejenga chuki mbaya na kutaka jamii imsaidia kumuunga mkono kwenye chuki yake ya kuwachukia wapinzani na wale wote wanaomkosoa.

JPM anahisi yeye tu ndiye anaweza kuibadilisha Tanzania na kuifanya kuwa the best country..wala hajui kama yupo mwingine yeyote hapa Tanzania mwenye uwezo wa kufanya anachoweza kufanya yeye.

Mbaya zaidi ameingiza chuki hiyo kwa wasaidizi wake ili wawachukie wapinzani. hawezi kufanikiwa kwa kutumia mfumo huu anaoenda nao ni hatari sana. Nampenda sana ila I don't like his methods and approach
 
Back
Top Bottom