Ili Magufuli aibadilishe Tanzania, ni lazima awe Rais kwa zaidi ya miaka kumi

Watanzania wengi wamejawa na wivu, wanajiangalia wao wenyewe na maisha yao sio ya Watanzania wote.
 
Sidhani kama hujatumwa kuja kumpigia debe awe kama kagame wetu....

by the way...hata nyerere angeweza kuongoza miaka 40 kama Mugabe.....Zimbabwe imefika wapi.

Pasi moja muachie mwenzio....mazishi ya kiislam haya kila mtu aguse jeneza mwili ufike makaburini....

unataka alibebe mwenyewe kwani maiti atafufuka? NA afufuke I'll iweje sie tushagawana mali za marehemu.

natumai umenisoma vizuri sana...fasihi uswazi at its best.
 
Pasikali nadhani au nawajibishwa na dhamira kuu nafsini mwangu kukubalika kuwa wewe naye ni kati ya wachumia tumbo.
kipi cha ajabu na mno ulichokiona kwa magu na utendaji wake mpaka umesahau kuwa nyerere alishawahi kutahadharisha juu ya ukomo wa madaraka na kwa vipindi viwili tuu.

kama mpaka Leo bado unaamini huyu ndugu ANAHITAJI maiaka 20 ya kutuongoza nadhani una matatizo ya kusoma alama za nyakati...

kifupi huyu bwana hana anachojua au analijua taifa linatakiwa liende wapi...akilala akiamka anafanya linalomjia ndotoni au analokutana nalo kwenye corridors za nyumba nyeupe.

Napinga hoja na ikiwezekana hawa ndio aina ya 1 term presdaaz.

Hawa huwa wanatokea kwenye maisha kama alerts kwa jamii kutorudia makosa....hawa ndio howa wanatokea kwenye jamii Ili laana ya kizazi chake nahata kabila au jamii yake yote ihukumiwe...cursed is the day he was born a bastard.
 
Kama hujaelewa ni wa kuambiwa magu jambo hili nakukabizi ww hakikisha unalisimamia hapo utampenda mjomba magu sio kuwa raisi wa nchi, Was and still is a big mistake ever done him being a president
Mwapachu wakati wa KAMPENI alisema mbio hizi za uchaguzi ni kati ya a leader akimaanisha lowasa and a manager akimaanisha magu....wengi hawakumuelewa ...natumai sasa mwapachu anaeleweka vizuri sana.
 
Bora ubinafsi wa kujenga uwanja kuliko ubinafsi wa kujilimbikizia mali kama lowassa
Wahi mapema na ushahidi huo...wenzako wameanzisha mahakama ya mafisadi na kesi hakuna....lowasa yupo hawana ushahidi...mahakimu na majaji wamesomea kuhukumu kesi fasta ila serikali imekosa watuhumiwa.
 
Huna jipya Njaa ndio inakusumbua.
Sijaona popote uliposhauri mambo ya Msingi.
Ili Nchi au Taifa liendelee linatakiwa liwe na Katiba Imara. Pili kuwe na Mfumo mzuri. Haya umekuwa Mpofu. Tatu kama unata Mheshimiwa aongezewe miaka zaidi ya 10, Shauri Katiba ibadilishwe. Maana yupo kwa Mujibu wa Katiba na Sheria za Nchi. Nne ungeongelea Kilimo ambacho 70% wananchi ni Wakulima. Tano ongelea Uhuru wa Kuongea na Habari. Sita ongelea Watanzania waishio nje, ili watambulike Kikatiba. Saba, Tume huru ya Uchaguzi.
My Take: Miaka 10 ni mingi sana. Ifike mahali hata Rais akivurunda Miaka 5 mwisho.



 
Mkuu, una hoja kuntu sana,, na kimsingi, nimekuelewa mnoo. Hivyo anavyodili navyo Magufuli, ni minor sana ktk kukuza uchumi.

Mambo makubwa angetakiwa kufanya ni kupunguza kodi kwa wawekezaji, bandarini na ktk sekta ya utalii.

Kuweka mazingira rafiki kwa ajili ya kuvutia wawekezaji. Kuisuka upya kabisa Elimu yetu.

Hawa wanaobisha, waseme tumbua tumbua, watumishi hewa, kupandisha kodi, nk, kuna athari gani chanya ktk uchumi? Kimsingi hamna!! Lakini ndiyo yamepewa kipaumbele. Rais angetilia mkazo kwa hayo mambo niliyota hapo juu, hakika nchi ingepiga hatua kwa kasi..

Simchukii Raisi, but i hate his lots of fundamental mistakes.

Genaro..
 
Good kaka Ki ukweli vipaumbele vyake sio.

Nimependa ulivo maliza [emoji1]
 
2017 umeanza tofauti mpaka basi sasa watu wanaonesha tabia zile komavu za kwao saweni bana kama vile mnaishi nje ya hapa TZ
 
WAZO SIOOOO, KIASI AMA KATI NA KATI NDIO MPANGO MZIMA, UKIZIDISHA INAKUWA NOMA.
NAAMINI KWENYE CHAMA PENDWA , KUNA VICHWA ZAIDI YA MAGUFULI VIPO TAYARI KUMPOKEA BAADA YA MIAKA YAKE KUMI.
HALAFU MIAKA KUMI INATOSHA KABISA KUSIMIKA MAONO NA DIRA ZAKO, IKIZIDIA HAPO KINACHOFATA NI KUHARIBU.
MFANO CHAI KIKOMBE KIKUBWA WASTANI NI SUKARI VIJIKO VITATU, HEBU NIAMBIE JE UNAONGEZAGA SUKARI ROBO KILO NZIMA KWENYE KIKOMBE CHA CHAI KWA SABABU TU SUKARI TAMU,
AMA CHUMVI KIJIKO KIMOJA NI TAMU KWENYE BAKULI KUBWA LA SUPU YA MAKONGORO, JE UNAONGEZAGA VIJIKO KUMI ILI TU KUONGEZA UTAMUUU, ????
 
Ume miss point, nchi kama yetu au mwananchi yoyote wa nchi kama yetu anategemea kuona angalau kuna ka-unafuu ka-maisha kuliko ilivyo kuwa awali uongozi mpya unapoingia madarakani. Hakuna mtu yoyote mwenye akili timamu anaetarajia nchi kama yetu iwe kama Singapore au Malaysia ndani ya miaka kumi tu. Issue ya kwanza kabisa ni huduma za kawaida kabisa za jamii, umeme wa bei nafuu, elimu,maji na afya, je ameweza kui-improve kimoja wapo kati ivyo? Jibu hakuna vimedidimia kabisa kuliko ilivyokuwa kipindi cha uongozi wa Kikwete. Kwa mfano tu elimu almost inaenda kufa, ukiachana na tatizo la mikopo na changamoto za elimu ya juu zilizo wekwa na uongozi huu, na (viini macho vya kupandisha alama za grades kwa O-level na A-level), sekondari za leo wiki zima zinafanya vikao vya kutishana karibia siku 3 au 2 za wiki ni vikao vya jinsi ya walimu kutekeleza majukumu yao na kila kikao kinatumia more than 3 hours. Leo hii mkuu wa wilaya na mukrugenzi ambao siyo walimu kabisa nao wanakagua lesson plans na schemes of work. Mwalimu 1 wa somo la sayansi anafundisha zaidi ya watoto 800 na hakuna semina elekezi ya huyu mwalimu ,mbinu gani atumie ili aweze kuhudumia idadi hiyo ya watoto. Na kibaya zaidi waziri wa elimu anataka sayansi wachukue watoto wote isiwe option maana yake nini watoto watazidi 1000. Haya utaje huo uwajibikaji na ufanisi kwa mwalimu kama huyu?. In short hakuna uwajibikaji wowote ulioongezeka bali kilicho ongezeka ni uogopaji, kuridhishana kinafiki na kufurahishana kinafiki. Ufanisi na ubora vimekufa. Bora wakati wa Kikwete hata wakubwa walikuwa wanaelezwa ukweli wanapokosea, leo hii mkubwa ukimueleza ukweli kwamba kakosea na amekurupuka ana kufukaza kazi, maana yake, nini tumeridi tulikokotoka miaka 30 au 40 nyuma, vilio tuletea umasikini ndivyo tunavirudia sasa maana yake nini, tunaenda kuwa masiki zaidi. Uwezo wa vijana kuleta challenge na udadisi pale ambapo viongozi wameboronga umeuliwa kabisa yaani uongozi huu ni shida zaidi ya shida. Kwa hivyo basi Rasi Magufuli akipewa zaidi ya miaka kumi tutakuwa masiki zaid.
 
Nimesoma heading tu ya thread yako na kuamini ina-represent kilichomo ndani. Badala ya kuvuruga democracy ya term mbili tu za miaka mitano mitano, anatakiwa ku-groom watu watakaoendeleza vision yake kama kwenye business jinsi ma-CEO wengi wanavyopatikana kwenye business entities kwani mara nyingi CEO anayetoka uulizwa na board any likely candidate from within au CEO kuanza kumsogeza likely candidate kwa board members. Kwenye public sector board members ni wapiga kura!!!
 
Amalize Muda wake apite hivi[emoji117]

Tunatakiwa tuwe na dira ya taifa ambayo raisi yoyote atakaeingia madarakani ataitekeleza na sio kila chama kuja na ilani yao, tunataka katiba itakayo mwajibisha raisi endapo ataenda kinyume na dira tutakayo iweka na si vinginevyo. Ukombozi wa Tanzania hauitaji mtu mmoja bali watanzania wote na tunaweza endapo tutatengeza katiba mpya ambayo itamwajibisha yoyote atakaenda kinyume nayo

Done
 
Obama aliweza kwa miaka 8 kurudisha uchumi wa marekani. Sasa hivi employment ni less than 5-%. Ulichoandika hapa kwanza ni dharau kwa raisi kwani yeye aligombea akijua kipindi chake ni miaka 5 hivyo Nina mategemeo kuwa alishajipanga namna ya kutekeleza malengo yake aliyojiwekea katika kuleta maendelea ya nchi. Nimalizie nikisema kuwa Magufuli ni CCM na hiki chama ndio kimecreate matatizo tuliyonayo hivyo perhaps si Magufuli au mtu mwingine CCM anayeweza kuyatatua.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…