Ili Magufuli aibadilishe Tanzania, ni lazima awe Rais kwa zaidi ya miaka kumi

Ili Magufuli aibadilishe Tanzania, ni lazima awe Rais kwa zaidi ya miaka kumi

Huwa najitahidi kuongea ukweli, japo mara nyingine watu wananikasirikia. Nakumbuka mapema sana, kabla hata jina Bulldozer halijajulikana kitaifa na kimataifa, nilisema humu JF Magufuli ni mchapa kazi sana, lakini labda ningependelea awe na nafasi ya Waziri Mkuu badala ya Raisi, kwa sababu anafanya kazi kama bulldozer, nikimaanisha alihitaji mtu ambaye sio "impulsive" kumwongoza, kama ilivyokuwa kwa Nyerere na Sokoine. Baadaye nilishangaa kuona jina Bulldozer limemnasa Magufuli.

Sasa nitawaambia jambo jingine. Tanzania tumegawanyika kwa sasa, pro na against Magufuli. Huko nyuma nilisema pia Tanzania ilikuwa imefikia pabaya sana na hivyo labda ilikuwa vema na wakati muafaka kupata kiongozi wa namna ya Magufuli, angalau kwa miaka kumi. Lakini sasa najua kwamba miaka kumi haitatosha. Najua hii ni kauli ya kuleta hasira, lakini ndio ukweli wenyewe.

Hakuna Raisi duniani anaweza kuibadilisha nchi toka alipoikuta Magufuli kwa kipindi cha miaka kumi tu. Na hatari ya miaka kumi ni kwamba raisi atakayefuata anaweza kuharibu mazuri yote yaliyofanywa, kwa sababu yale mazuri yanakuwa hayajaota mizizi sawasawa (established sustainable systems). Na hiyo ni ukweli wa-kishule (academic truth) kwamba ili nchi iendelee inahitaji mipango ya muda mrefu isimamiwe na mtu ambaye yuko committed kuisimamia (committed leadership to implement strategic national development plans). Hakuna mpango wa muda mrefu wa kuiendeleza nchi utakaotekelezwa chini ya miaka kumi. Huo ndio ukweli wenyewe.

Ukiangalia historia ya mataifa yaliyoendelea haraka chini ya viongozi wao maarufu, utaona kwamba mafanikio ya nchi hizo hayakuletwa na viongozi waliobadilisha hizo nchi katika kipindi cha miaka kumi tu. Mifano mizuri ni Singapore, Malaysia na hata Rwanda. Singapore kwa mfano, kuna wakati fulani kiongozi wao alilalamikiwa, na hata kukasirikiwa kwa maamuzi magumu aliyofanya, lakini angalia alipoifikisha Singapore, toka taifa masikini sana. Ilimchukua miaka zaidi ya kumi kufanikisha hilo. Malaysia ni hivyo hivyo na Rwanda ndiko wanakoelekea.

Huwezi kuilinganisha Tanzania na nchi kama Marekani, ambao tayari wana "established systems" ambazo hazihitaji raisi mzuri kukaa madarakani zaidi ya miaka nane. Na mie ni wa kwanza kukubali kwamba ukiweka utarataibu wa kutokuwa na kikomo cha uraisi kabla hujampata Raisi mzalendo kama Nyerere au Magufuli, hatari ni kwamba unaweza kumpa nafasi raisi fisadi au mbovu akaharibu sana nchi. Mifano ya nchi za namna hiyo ipo mingi imetuzunguka.

Lakini sasa tunajua Magufuli ni mtu wa namna gani. Yapo ambayo sikubaliani na Raisi Magufuli, na hata kumkasirikia mara nyingine. Lakini ni mengi zaidi ninayokubaliana naye, hasa katika kukabiliana na ufisadi na kuleta nidhamu ya uwajibikaji. Watanzania tulilala sana, tulifikia uozo mbya sana. Niliwahi kuwaambia kuna mke wa raisi alimfokea kiongozi wa bandari kwa kukataa kuyatoa makontainer yake bila kuyalipia kodi. Aliitwa ikulu (na mke) na akaishia kuyatoa bila kupenda.

Na ukweli unabakia, kwamba, kama kweli Tanzania tunahitaji mabadiliko ya kutumia rasilimali zetu tuwe kama Singapore au Malaysia, basi mtu kama Magufuli anahitaji kuwa madarakani kwa zaidi ya miaka kumi. Najua hii ni lugha Watanzania wengi, na hasa vyama vya upinzani, hawawezi kuifurahia, lakini huo ndio ukweli. Baada ya hiyo miaka labda ishirini ya Magufuli, basi tunaweza kurudi tena kwenye uraisi wa kiindi cha miaka kumi au hata nane. Tutakuwa tayari tuna "established system" huenda hata kwa kiwango cha Singapore. Kama ikibidi vyama vya upinzani kuungana na CCM kwa sasa ili kufanikisha hilo basi na iwe hivyo.
Ili nchi iendelee inahitaji pamoja na mabo mengine misingi ambayo ni kama katiba bora na miongozo mbali mbali iliyoandikwa ambayo itaweza kusimamia kila jambo kwa maslahi ya nchi. Lakini kwa sasa nchi inaongozwa kwa hisia za aliye madarakani, anaweza akafanya mazuri kwa kipindi chake akiondoka kwa kuwa hakuna miongozo ajaye anaweze kuvuruga yote na hata yeye lazima awe na miongozo thabiti ya kumongoza
 
Zaidi ya miaka kumi? Kwa kipimo gani?
Moja ya njia za kuimarisha serikali ni kuwa na strong and committed civil service. Hii itawezesha kujenga conducive and enabling environment for private sector to perform.
Serikali lazima iwe shirishi na isiwe ya kusubiri mtu mmoja atoe maagizo.
 
Ili nchi iendelee inahitaji pamoja na mabo mengine misingi ambayo ni kama katiba bora na miongozo mbali mbali iliyoandikwa ambayo itaweza kusimamia kila jambo kwa maslahi ya nchi. Lakini kwa sasa nchi inaongozwa kwa hisia za aliye madarakani, anaweza akafanya mazuri kwa kipindi chake akiondoka kwa kuwa hakuna miongozo ajaye anaweze kuvuruga yote na hata yeye lazima awe na miongozo thabiti ya kumongoza

MKuu, nakubaliana na wewe 100%. Hata hivyo, ni mapema sana kwa Magufuli kuanza kubadilisha mifumo kwa sasa. NIlisema huko nyuma kwamba unapokuta wakaaji wa nyumba wanaachia uchafu na takataka nyingi zilizooza ndani ya nyumba, huanzi kwa kupanga ratiba na sheria za usafi wa nyumba. Unachukua hatua ya kusafisha kwanza, ndipo inafuata utaratibu au mfumo wa kufanya usafi kwa wakati ujao.
 
Mpaka sasa sijaona vipaumbele vya vya kiuchumi vya awamu hii.

Kwa sasa ni mapema mno kujua kama tunafanya vizuri au tunarudi nyuma. Lakini naamini by the end of this year kila moja Wetu atapata picha halisi!!
 
Unajua kazi ya Ilani ?
Tuanzie hapo kwanza.
Mkuu nadhani ulimaanisha katiba. Ilani haihusiani kabisa na kipindi cha utawala wa raisi. Nianze na wewe hapo kwanza, kabla hujafikia level ya kujadiliana nami thread yangu.
 
Mkuu kwanza nikupongeze kwa makala ndefu
Lakini umetolea mfano way out of context
1. Singapore na Malysia huwezi kuziweka kwenye kundi moja la maendeleo hutajifunza kitu hapo, Singapore wako mbali hadi basi yaani

Mkuu, tuna kitu kimoja common na Singapore na Malaysia; wote walikuwa masikini, na wote walibahatika kupata viongozi makini waliokuwa wazalendo kweli kweli wakainua nchi zao kiuchumi na hata infrastructure. Ni kweli Malaysia mafuta yalisaidia, tofauti na Singapore ambao walikuwa hawana kitu. Hapo unaposema Singapore wako mbali ndipo ninapotaka na sisi tuige. Singapore iliwachukua miaka ishirini toka umasikini wa kutupwa hadi kuwa tajiri - 1965-1985. Kilichowanua ni akili ya kutumia rasilimali zao chache na sera sahihi za uwekezaji. Sisi tunagombana na kina Dangote!

2. Singapore waliendelea kwa ku take advantage of their location, wali tengeneza bandari zao, viwanja vya ndege , walipunguza kodi na regulations za ajabu, wali ifumua elim yao na kuilenga kwenye kuvutia uwekezaji, wao walikuwa ni urban country toka kitambo lakin pia serikali ilipiga kazi kwenye kuwekeza.

Angalau Singapore walitake advantage ya location. Kumbuka hapo 1965 Singapore was basically nchi ya slums kama nchi nyingine za Asia. Tuambie sisi tuna mengi mazuri mangapi zaidi ya location ya Singapore, na tume take advantage yake? Angalia kwa mfano, Singapore waliingia katika petrochemical industries kwa mafanikio sana japo hawana gesi kama sisi!!! Sisi tunaishia kupiga makofi na kushangilia kugundua gesi. Sana sana mwisho wa kufikiri kwetu ni kutumia gesi kwa ajili ya kuzalisha umeme na kuuza Kenya! Pathetic.

2. Malaysia wao wana natural resources kama sisi bongo, halafu wao kidogo hata system zao za siasa ni ngum kidogo na kuna mchanganyiko wa watu mbali mbali so ku wamange ni shida, Malaysia wao wali anza kama Magufuli eti wanatoa rushwa, lakini wataalam wao waka waambia hakuna correlation kati ya rushwa na umaskini wao, walicho fanya ni kuwekeza kwenye madini na mafuta na kilimo, waka ifumua elimu yao na kuwekeza kwenye sayansi mfano kila mwaka wanafunzi wanao graduate vyuo vikuu asilimia 30% wana graduate mechanical engeneering, waka wekeza kwenye kujenga miundo mbinu mizuri kwa ajili ya uwekezaji, pia waka weka mazingira ya kuvutia wataalm wa nje kwenye nafasi za juu za makampuni yao. Japo Malaysia wanakua kwa kasi bado haija ingizwa kwenye kundi la developed countries.

Angalau basi tumepata Raisi wa kuyashughulikia hayo. Lakini baada ya miaka kumi itakuwaje? Tena nakwambia the worst thing to happen baada ya miaka kumi ni CCM kupoteza uchaguzi na chama kipya kuingia ambapo watataka kubadili kila kitu ili wasionekane wanaendeleza ya Magufuli

*japo umejitahidi kumtetea Magufuli hakuna chochote anacho fanya kinacho endana na Malaysia, singapore ndio kabsaa. So sijajua case ya Rwanda labda wenzetu walifanya anacho fanya Magufuli. Lakini this man is failing moja kwa moja

Hapana Mkuu. This man is doing his best for this country, japo sometimes he is misguided. He needs our support kwa sababu he is genuine katika kutaka kubadilisha nchi hii iliyokuwa imeoza sana. Sasa hivi Magufuli ni kama Doctor ambaye anaifanyia Tanzania operation. Maumivu yapo, lakini ni ya muda baada na huwezi kumtukana doctor kwa maumivu anayokupa anapokufanyia operation. Ni kwa faida yako na kuokoa uhai wako.
 
uko sahishi maana kuongoza miaka miaka kumi yani kila baada ya miaka minne anawaza uchaguzi atapita au asipite so hii inawapa wakati mgumu sana kwa maraisi wetu kutekeleza ahadi za maendeleo
mfano saiz Raisi wetu inaweza kua asha anza kuweka mipango ya 2020
kwa iyo inakua vigumu sana kutekeleza long plan ndan ya miaka mitano
na hii kwa nchi za ili mwengu wa tatu kama nchi za kiafrika

kwa iyo raisi anatakiwa apewe muda mrefu ili awe huru kutekeleza mipango ya muda mrefu ya maendeleo..
 
Naunga mkono hoja na hili na mimi pia niliwahi kulizungumzia na nikapendekeza tumpe angalau vipindi 4 vya miaka mitano mitano na kusiwe na uchaguzi wa rais ili kubana matumizi.

Kwa Kasi hii ya Magufuli, kuna haja Kufanya Uchaguzi wa Rais 2020?
Nilisema hivi


Pascal

Mkuu Pascal, jinsi ya kulitekeleza hili na jambo jingine. Japo tunaweza kuwa na mapendezi kumpa Magufuli muda zaidi, lakini suala la msingi la demokrasia ya uchaguzi lazima lifanyike, kama vile tu ambavyo ilivyokuwa wakati wa Nyerere. Labda cha msingi ni kutafuta muafaka na vyama vya upinzani kwamba katika kipindi hicho cha "evolution ya Tanzania" chini ya Magufuli, wao watakuwa wapi kama ikibidi waendelee kuwapo? Ikibidi yanaweza kufanyika makubaliano kwamba wakiwa katika umoja wa namna ya UKAWA, wapewe nafasi ya Uwaziri Mkuu katika serikali ya mseto ya mpito, kama moja wapo ya makubaliano ya Magufuli kuongoza kwa zaidi ya miaka 10. Hiyo pia itatoa fursa nzuri ya kuimarisha upinzani nchini.
 
kwahiyo unataka abadili katiba ili atawale zaidi au???

Hapana. Sitaki abadili Katiba. Kama ni kubadili katiba Watanzania ndio wanaopaswa waibadili. Nataka tutafute namna ya makubaliano na vyama vya upinzani ili hili lifanyike. Nimesema hapo juu kwamba ikibidi kuwe na serikali ya mseto ya kipindi kisichaozidi miaka 10 chini ya Magufuli baada ya kile kipindi chake cha miaka 10 utawala wake wa kikatiba, ambapo upinzani wanaweza kuungana kwa namna ya UKAWA wakapewa nafasi ya Uwaziri Mkuu kwa hiyo miaka 10 ili kumpa Magufuli miaka 20 hivi.
 
tatizo la rais wetu anataka sifa mwenyewe hataki kuweka mfumo ambao utainyoosha nchi hii hata kama akiondoka madarani.

Misifa , misifa, misifa
Sawa Mkuu, labda Magufuli ana hilo tatizo. Lakini, katika suala zima la kuiendeleza Tanzania, unaona kama ni tatizo lake ni baya sana na ni afadhali tungekuwa na aina ya viongozi waliopita (ukiondoa Nyerere) kuliko Magufuli?
 
Kwa hali ilivyo wazo hilo ni baya mleta mada, afadhali kama jamaa angekuwa Democrat , lakini kwa haya kuamka asubuhi katamka hivi na vile hapana jamani.

Vinginevyo hayo mawazo yanayochipuka yakipaliliwa na wabunge wetu hawa wa NDIYOOOOOOOO, basi tutaishi kama kuku wa kizungu

Labda ni afadhali tuishi kama kuku wa kizungu wanaokula chakula kinachojulikana na kupewa huduma muhimu kuliko kama kuku wa kienyeji wanaoswaga kila kitu kitia ndani kinyesi.
 
Kilichomshinda Kambarage Magufuli hakiwezi. Akitaka kujua labda aende Butiama pengine yule mama Mzee amemdokeza kilio chake cha mkwamo mpaka ikamlazimu kung'atuka.
Kwa staili hii ya kuiundava kufanikiwa ni kugumu mno hata kama kweli unaamini unachotaka kufanikisha ni kwa manufaa ya wengi.

Mabadiliko ni watu na uhuru. Na siyo udava na maguvu.

Mkuu,sipendi kumtumia Hitler kama mfano, lakini pamoja na makosa yake makubwa ya kuvimba kichwa na kutaka kuitawala dunia na ukatili wake wa kutaka kufutilia mbali baadhi ya jamii zilizoko duniani, u-bulldozer wake uliifikisha Germany sehemu ambayo kama Hitler asingeliingiza lile taifa katika vita kuu ya pili, leo kungekuwa hakuna taifa duniani linaikaribia Germany kwa nguvu ya kiuchumi! Hata Marekani asingekuwa kitu kwa Germany.
 
Ili afanikiwe anahitajika zaidi kujenga taasisi imara zinazoweza kumsaidia kufikia mipango yake..

Hizi hadithi za kupewa muda wa ziada ni za kipuuzi na zinalenga kushawishi kutokuheshimu katiba yetu..

Afanye kwa kiasi chake muda ukiisha apishe wengine, bado nchi ina hazina ya viongozi tena wazuri kuliko yeye!
 
Hii Nchi ina Watu wa Kujipendekeza Njaa Mbaya Sana

Mkuu, kama unanisema mie, basi elewa kwamba Magufuli hana mchango wowote katika kipato ninachopta kila siku, na wala kazi yangu na haihusiani kabisa na kuteuliwa naye au kuwapo kwake madarakani. Sina sababu yeyote ya kujipendekeza kwake, ila naipenda nchi yangu, sana tu, na ninachukia sana ufisadi na uzembe.

Na kwa taarifa yako, kama nilivyosema, kuna mambo Magufuli anafanya siyapendi kabisa, lakini naona mazuri mengi kuliko mabaya machache anayofanya. Sasa kama hilo kwako ni tatizo shauri yako wewe ambae inaonekana uwepo wa Magufuli unakunyima maslahi fulani.
 
Excuse me Moderator, May you create " DISLIKE " Burton Please.
 
Ili afanikiwe anahitajika zaidi kujenga taasisi imara zinazoweza kumsaidia kufikia mipango yake..

Hizi hadithi za kupewa muda wa ziada ni za kipuuzi na zinalenga kushawishi kutokuheshimu katiba yetu..

Afanye kwa kiasi chake muda ukiisha apishe wengine, bado nchi ina hazina ya viongozi tena wazuri kuliko yeye!

Mkuu, inabidi usome "strategic planning and management" kama sisi wengine ndipo utaelewa tunachosema. La sivyo ni sawa na mtoto wa darasa la saba kujadili hoja ya utawala na Professor na utegemee atatoa hoja za maana.
 
Excuse me Moderator, May you create " DISLIKE " Burton Please.

Mkuu, with a statement like that, I already know what kind of discussion forums you need to take part in; where we post threads like "Waziri wa CCM afumaniwa na mke wa Diwani wa Chadema".
 
Back
Top Bottom