Ili Magufuli aibadilishe Tanzania, ni lazima awe Rais kwa zaidi ya miaka kumi

Mkuu,sipendi kumtumia Hitler kama mfano, lakini pamoja na makosa yake makubwa ya kuvimba kichwa na kutaka kuitawala dunia na ukatili wake wa kutaka kufutilia mbali baadhi ya jamii zilizoko duniani, u-bulldozer wake uliifikisha Germany sehemu ambayo kama Hitler asingeliingiza lile taifa katika vita kuu ya pili, leo kungekuwa hakuna taifa duniani linaikaribia Germany kwa nguvu ya kiuchumi! Hata Marekani asingekuwa kitu kwa Germany.

Ase umeniacha hoi.
Kwa hiyo utawala wa aina Hitler uko sahihi kuwapo siyo?. Yaani ndiyo njia pekee watu huweza kuapta maendeleo siyo?.
Acha utani bana!
 
Hivi Mkuu unajua Historia wewe? Unajua Hitler aliifikisha Germany wapi kabla hajaingiwa na mdudu kichwani? Si kila kitu Hitler alichoifanyia Germany kilikuwa kibaya, japo anapaswa kulaaniwa na dunia nzima kwa ubaya na ukatili aliofanya. Hitler aliistawisha sana Ujerumani hadi kuwa taifa lenye nguvu sana kiuchumi na kijeshi, kukawa hakuna mfano wake duniani.

Kwa taarifa yako, Hitler ndiye aliyeanzisha wazo la kampuni ya Volks Wagen (VW), ambayo tafsiri yake ni "Gari la Watu". Concept yake ilikuwa kwamba kila Mjerumani wa kawaida aweze kumudu kununua gari, na akawaagiza mainjinia wa Ujerumani watengeneze gari ambayo itakuwa na bei nafuu na itaweza kununuliwa na kila Mjerumani. Ndipo gari ya VW beetle ilipoanzishwa. Hata wazo la kutumia upepo kupooza injini ya VW lilitoka kwa Hitler, pamoja na fedha za kufanya utafiti wa gari kama hiyo. Sasa hilo lilikuwa na ubaya gani toka kwa Hitler?

Angalia hapa chini Wikipedia inasemaje;

In 1932, with many of the above projects still in development or early stages of production, Adolf Hitler got involved, ordering the production of a basic vehicle capable of transporting two adults and three children at 100 km/h (62 mph). He wanted his German citizens to have the same access to a car as the Americans. The "People's Car" would be available to citizens of the Third Reich through a savings plan at 990 Reichsmark ($396 in 1930s U.S. dollars)—about the price of a small motorcycle (the average income being around 32RM a week).

Despite heavy lobbying in favor of one of the existing projects, it soon became apparent that private industry could not turn out a car for only 990RM. Thus, Hitler chose to sponsor an all-new, state-owned factory using Ferdinand Porsche's design (with some of Hitler's design constraints, including an air-cooled engine so nothing could freeze). The intention was that ordinary Germans would buy the car by means of a savings scheme ("Fünf Mark die Woche musst du sparen, willst du im eigenen Wagen fahren" – "Five marks a week you must put aside, if you want to drive your own car"), which around 336,000 people eventually paid into. However, the entire project was financially unsound, and only the corruption and lack of accountability of the Nazi regime made it possible.
 
mawazo ya kijinga yanayoshawishi brein za wajinga hoja ni moja tupe hata theluth moja ya maendeleo aloleta zaidi
yakununu ndege mbovu wakati nchi ina chaa watu wanakufa hakuna hata paracetamol anajenga uwanja kijijin kwake anateua tu wasukuma wenzake na kuwafukuza wataalamu kwa kisingizi cha kipuuzi alichokipachika jina la MAJIPU
 
Hahaha! Mkuu, eidha wewe, au ndugu yako ameshatumbuliwa na Magufuli na hupati ulaji tena! Na kwanza Magufuli sio Msukuma, ila anaongea Kisukuma na ana lafudhi kidogo ya Kisukuma.

Pia, kununua ndege badala ya dawa ni suala la priorities. Sidhani kama asingenunua ndege ile fedha ingeenda kwenye dawa, au hata madawati, hivyo hatujui. Kumbuka pia, inawezekana kabisa amenunua ndege sasa badala ya dawa ili baadaye awe na uwezo mkubwa zaidi wa kununua dawa. Hivyo mara nyingine sacrifices zinahitajika ili kuwa na mafanikio kwa kiwango kikubwa na cha kudumu zaidi. Labda tungemlaumu ikiwa angenunua ndege ya raisi badala ya dawa. Mbona humsifii kwa kujenga barabara badala ya kufanya sherehe ya kitaifa ya siku moja? Be fair.

Vumilia, kutumbuana ni sehemu ya maumivu kuelekea nchi ya ahadi. Nakubali watakuwapo baadhi ya watu wanaotumbuliwa kimakosa, innocent casualties of war. Hata tulipopigana kumwondoa Idd Amin kuna watu wasio na makosa ilibidi waumie na hata kupoteza maisha ili kumshinda Amin. Ni filosofia ya maisha katika kutafuta hali bora zaidi.
 
Hizo nchi kama Taiwan Malaysia Singapore south Korea Thailand waliimarisha taasisi(institutions) sio madictator wanaofunga wapinzani!!! Japo Dr mahathir Mohammed alikuwa dictator uchwara lakini alijenga taaisis imara kama mahakama huru,elimu bora,bunge la kidemocrasia. Hawakujijenga ki dictatorship magufuli ukamfananishe na kina duterte au buhari hamna malengo ya muda mrefu zaidi ya kudeal na matukio na sifa za majukwaani
 
Despite heavy lobbying in favor of one of the existing projects, it soon became apparent that private industry could not turn out a car for only 990RM. Thus, Hitler chose to sponsor an all-new, state-owned factory using Ferdinand Porsche's design (with some of Hitler's design constraints, including an air-cooled engine so nothing could freeze). The intention was that ordinary Germans would buy the car by means of a savings scheme ("Fünf Mark die Woche musst du sparen, willst du im eigenen Wagen fahren" – "Five marks a week you must put aside, if you want to drive your own car"), which around 336,000 people eventually paid into. However, the entire project was financially unsound, and only the corruption and lack of accountability of the Nazi regime made it possible.

The problem your too far behind and you don't get/missing what leadership is all about. Leadership is not just dreams !
 
Hizo nchi kama Taiwan Malaysia Singapore south Korea Thailand waliimarisha taasisi(institutions) sio madictator wanaofunga wapinzani!!! Japo Dr mahathir Mohammed alikuwa dictator uchwara lakini alijenga taaisis imara kama mahakama huru,elimu bora,bunge la kidemocrasia. Hawakujijenga ki dictatorship magufuli ukamfananishe na kina duterte au buhari hamna malengo ya muda mrefu zaidi ya kudeal na matukio na sifa za majukwaani

Mkuu, mbona unataka tukimbie kabla ya kutembea? Nimetoa mfano hapo juu kwa watu wote mnaodai Magufuli hajaanzisha taasisi au mifumo. Nimeuliza, ikiwa unakuta nyumba nzuri lakini ndani imejaa takataka zilizooza na kila aina ya uchafu kwa sababu wanaokaa ndani ya nyumba hawafanyi usafi, ni hatua gani utachukua kwanza? Kusafisha au kupanga ratiba na utaratibu wa kudumu wa kufanya usafi? Au kuanza mijadala mingi isiyoisha juu ya njia bora na vifaa vya kutumia kufanya usafi?

Unataka Magufuli kwa sasa ashughulike sana na kupanga ratiba na utaratibu wa kuifanyia Tanzania usafi wakati nyumba imejaa uchafu? Hapana. Lojiki ni kwamba, kwanza safisha nyumba, kisha timua wakaaji wote wanaosababisha uchafu, kisha weka utaratibu wa usafi. Mambo mazuri yanachukua muda kupanga, so, uwe na subira. Hiyo mifumo itakuja tu.
 
The problem your too far behind and you don't get/missing what leadership is all about. Leadership is not just dreams !

Achana na mie Mkuu, umetoa wapi filosofia kuwa kwamba leadership ni dreams? Hebu tuache nenda kule kwenye thread za Waziri wa CCM kafumaniwa na mke wa Diwani wa Chadema. Naona wazi hii thread siyo ligi yako.
 
Mkuu nadhani ulimaanisha katiba. Ilani haihusiani kabisa na kipindi cha utawala wa raisi. Nianze na wewe hapo kwanza, kabla hujafikia level ya kujadiliana nami thread yangu.
Mkuu Ilani ni mipango ya utawala (kwamba katika kipindi cha uongozi wa miaka mitano tutatekeleza hiki na kile)
Maana yangu ni kuwa kama CCM ingesimamia Ilani yake hakuna haja ya Magufuri kuongoza Karne nzima, inamaana Ilani itamsaidia kiongozi anayefuata kuendeleza pale mwingine alipoishia (usiseme Magufuri anachokifanya wengine hawataweza kukifanya na usiseme ana kipawa ambacho binadam wengine hawana hivyo kwa kuwa tumempata yeye basi tuvunje katiba maana inchi imempata malaika).
 
Nchi yetu Inaweza kuaendelea nakujengeka zaidi hata kwa kipindi cha miaka kumi unavyosema tunahitaji miaka 20 kujijenga na nchi kama syria ilivyosasa itahitaji miaka mingapi kuja kuwa na uchumi mzuri. Kwahiyo Ni sekta chache zinahitaji marekebisho na kuwa na mfumo mzuri utakao liwezesha taifa kufika mbali
 
Mkuu Ilani ni mipango ya utawala (kwamba katika kipindi cha uongozi wa miaka mitano tutatekeleza hiki na kile)
Maana yangu ni kuwa kama CCM ingesimamia Ilani yake hakuna haja ya Magufuri kuongoza Karne nzima, inamaana Ilani itamsaidia kiongozi anayefuata kuendeleza pale mwingine alipoishia (usiseme Magufuri anachokifanya wengine hawataweza kukifanya na usiseme ana kipawa ambacho binadam wengine hawana hivyo kwa kuwa tumempata yeye basi tuvunje katiba maana inchi imempata malaika).

Ahaa, nadhani sasa nimekuelewa na utanielewa. Anachofanya Magufuli hapa ni zaidi ya Ilani ya CCM ya uchaguzi. Katika utawala wa Mwinyi, Mkapa na JK, tulikuwa na Ilani za CCM, lakini zilitufikisha wapi? Ziliondoa uzembe na ufisadi nchini? Ziliweka mifumo yenye kusaidia nchi hii? Zilitufanya tufaidike na rasilimali zetu? Sasa haya maswali yanalenga kile anachojaribu kufanya Magufuli kwa sasa, ambacho ni zaidi sana ya Ilaani cha uchaguzi ambazo si lololote si chochote bali maneno ya biashara tu.

Labda pengine tunaweza kusema sawa, Ilani hizo ni muhimu, lakini tulichoona ilani bila "catalyst" inayofaa hazina faida yeyote. Basi Magufuli kawa hiyo "catalyst".

Na unaposema atakayempokea ataendeleza hiyo "Ilani". Unajuaje kama huyo atakayempokea na yeye atakuwa "catalyst" inayofaa? Na je, unasahau kwamba inawezekana kabisa atakaempokea akawa toka chama cha upinzani, ambapo hata hiyo Ilani iwe nzuri kiasi gani anaweza kuitupilia mbali ili aje na "Ilani" ya chama chake ambayo itaturudisha mwanzo tena na huenda kuharibu kila kitu alichofanya Magufuli kwa kuwa bado hakijaota mizizi thabiti? Angalia kule USA, Trump wa Republicans, anasema atafumua kila sera iliyowekwa na Obama wa Democrats. Hivi kweli unakubali kila lililowekwa na Obama lilikuwa baya?

Ndio maana nikasema, ili ku- minimize risks of leadership change na kuweka Tanzania mbele badala ya siasa, kwa kuwa sasa tunajua Magufuli ni mtu wa namna gani katika utendaji kama Raisi, ni bora tuijengee Tanzania misingi imara ambayo itafanya tusiwe tena na tatizo la kuwa na vipindi vya uraisi vya miaka kumi au nane hapo baadaye. Hata kama ikibidi akae miaka ishirini, au kuwaambia upinzani watafute namna ya kuungana na CCM kwa sasa hadi ttakapokuwa tumejenga mifumo dhabiti ya kiutawala na maendeleo ya nchi, kutia ndani uwajibikaji, nidhamu ya kazi na kuua ufisadi. Katika haya tumeona wazi Magufuli yuko serious.
 
Achana na mie Mkuu, umetoa wapi filosofia kuwa kwamba leadership ni dreams? Hebu tuache nenda kule kwenye thread za Waziri wa CCM kafumaniwa na mke wa Diwani wa Chadema. Naona wazi hii thread siyo ligi yako.

Asante. Kumbe uko kiligi badala ya mantiki.
 
Unaona sasa Mkuu, hata maana ya ligi naona hujui. Kwani mie kuwa ki-ligi ni tatizo? Naona niliposema hii siyo ligi yako wazo lililokujia la la ushindani wa mpira, Yanga Vs Simba? Ligi siyo lazima iwe ushindani wa mpira au michezo, ina maana pia kikundi kinachochadili jambo fulani kwa madhumuni maalum!
 
Huwa najitahidi kuongea ukweli, japo mara nyingine watu wananikasirikia. Nakumbuka mapema sana, kabla hata jina Bulldozer halijajulikana kitaifa na kimataifa, nilisema humu JF Magufuli ni mchapa kazi sana, lakini labda ningependelea awe na nafasi ya Waziri Mkuu badala ya Raisi, kwa sababu anafanya kazi kama bulldozer, nikimaanisha alihitaji mtu ambaye sio "impulsive" kumwongoza, kama ilivyokuwa kwa Nyerere na Sokoine. Baadaye nilishangaa kuona jina Bulldozer limemnasa Magufuli.

Sasa nitawaambia jambo jingine. Tanzania tumegawanyika kwa sasa, pro na against Magufuli. Huko nyuma nilisema pia Tanzania ilikuwa imefikia pabaya sana na hivyo labda ilikuwa vema na wakati muafaka kupata kiongozi wa namna ya Magufuli, angalau kwa miaka kumi. Lakini sasa najua kwamba miaka kumi haitatosha. Najua hii ni kauli ya kuleta hasira, lakini ndio ukweli wenyewe.

Hakuna Raisi duniani anaweza kuibadilisha nchi toka alipoikuta Magufuli kwa kipindi cha miaka kumi tu. Na hatari ya miaka kumi ni kwamba raisi atakayefuata anaweza kuharibu mazuri yote yaliyofanywa, kwa sababu yale mazuri yanakuwa hayajaota mizizi sawasawa (established sustainable systems). Na hiyo ni ukweli wa-kishule (academic truth) kwamba ili nchi iendelee inahitaji mipango ya muda mrefu isimamiwe na mtu ambaye yuko committed kuisimamia (committed leadership to implement strategic national development plans). Hakuna mpango wa muda mrefu wa kuiendeleza nchi utakaotekelezwa chini ya miaka kumi. Huo ndio ukweli wenyewe.

Ukiangalia historia ya mataifa yaliyoendelea haraka chini ya viongozi wao maarufu, utaona kwamba mafanikio ya nchi hizo hayakuletwa na viongozi waliobadilisha hizo nchi katika kipindi cha miaka kumi tu. Mifano mizuri ni Singapore, Malaysia na hata Rwanda. Singapore kwa mfano, kuna wakati fulani kiongozi wao alilalamikiwa, na hata kukasirikiwa kwa maamuzi magumu aliyofanya, lakini angalia alipoifikisha Singapore, toka taifa masikini sana. Ilimchukua miaka zaidi ya kumi kufanikisha hilo. Malaysia ni hivyo hivyo na Rwanda ndiko wanakoelekea.

Huwezi kuilinganisha Tanzania na nchi kama Marekani, ambao tayari wana "established systems" ambazo hazihitaji raisi mzuri kukaa madarakani zaidi ya miaka nane. Na mie ni wa kwanza kukubali kwamba ukiweka utarataibu wa kutokuwa na kikomo cha uraisi kabla hujampata Raisi mzalendo kama Nyerere au Magufuli, hatari ni kwamba unaweza kumpa nafasi raisi fisadi au mbovu akaharibu sana nchi. Mifano ya nchi za namna hiyo ipo mingi imetuzunguka.

Lakini sasa tunajua Magufuli ni mtu wa namna gani. Yapo ambayo sikubaliani na Raisi Magufuli, na hata kumkasirikia mara nyingine. Lakini ni mengi zaidi ninayokubaliana naye, hasa katika kukabiliana na ufisadi na kuleta nidhamu ya uwajibikaji. Watanzania tulilala sana, tulifikia uozo mbaya sana. Niliwahi kuwaambia kuna mke wa raisi alimfokea kiongozi wa bandari kwa kukataa kuyatoa makontainer yake bila kuyalipia kodi. Aliitwa ikulu (na mke) na akaishia kuyatoa bila kupenda.

Na ukweli unabakia, kwamba, kama kweli Tanzania tunahitaji mabadiliko ya kutumia rasilimali zetu tuwe kama Singapore au Malaysia, basi mtu kama Magufuli anahitaji kuwa madarakani kwa zaidi ya miaka kumi. Najua hii ni lugha Watanzania wengi, na hasa vyama vya upinzani, hawawezi kuifurahia, lakini huo ndio ukweli. Baada ya hiyo miaka labda ishirini ya Magufuli, basi tunaweza kurudi tena kwenye uraisi wa kipindi cha miaka kumi au hata nane. Tutakuwa tayari tuna "established system" huenda hata kwa kiwango cha Singapore. Kama ikibidi vyama vya upinzani kuungana na CCM kwa sasa ili kufanikisha hilo basi na iwe hivyo.

Inawezekana, akimaliza 10 tumuongezee 10. Kagame aliweza hata SISI tunaweza kuiokoa Tanzania iliyokuwa ikidifimia kwa uchumi wa bandia na wizi wa ajabu
.
 
Ahaa, nadhani sasa nimekuelewa na utanielewa. Anachofanya Magufuli hapa ni zaidi ya Ilani ya CCM ya uchaguzi. Katika utawala wa Mwinyi, Mkapa na JK, tulikuwa na Ilani za CCM, lakini zilitufikisha wapi? Ziliondoa uzembe na ufisadi nchini? Ziliweka mifumo yenye kusaidia nchi hii? Zilitufanya tufaidike na rasilimali zetu? Sasa haya maswali yanalenga kile anachojaribu kufanya Magufuli kwa sasa, ambacho ni zaidi sana ya Ilaani cha uchaguzi ambazo si lololote si chochote bali maneno ya biashara tu.

Kwa hiyo tuko kwenye ilani za mfukoni siyo?
 
Hapana. Sitaki abadili Katiba. Kama ni kubadili katiba Watanzania ndio wanaopaswa waibadili. Nataka tutafute namna ya makubaliano na vyama vya upinzani ili hili lifanyike. Nimesema hapo juu kwamba ikibidi kuwe na serikali ya mseto ya kipindi kisichaozidi miaka 10 chini ya Magufuli baada ya kile kipindi chake cha miaka 10 utawala wake wa kikatiba, ambapo upinzani wanaweza kuungana kwa namna ya UKAWA wakapewa nafasi ya Uwaziri Mkuu kwa hiyo miaka 10 ili kumpa Magufuli miaka 20 hivi.
Kwa chuki na husda aliyonayo Magufuli aliyonayo kwa upinzani hilo halitatokea KAMWE

By the way, Nchi haiendeshwi kwa makubaliano bali kwa katiba ambayo ndo sheria mama ambayo Magufuli aliapa kuilinda na kuitetea.
 
Inawezekana, akimaliza 10 tumuongezee 10. Kagame aliweza hata SISI tunaweza kuiokoa Tanzania iliyokuwa ikidifimia kwa uchumi wa bandia na wizi wa ajabu
.

Ila tusiongee kumuongezea kwa ushabiki wa kisiasa bali kwa kutathmini kile anachofanya, bila kujaliitikadi zetu cha kisiasa
 
Kwa chuki na husda aliyonayo Magufuli aliyonayo kwa upinzani hilo halitatokea KAMWE

By the way, Nchi haiendeshwi kwa makubaliano bali kwa katiba ambayo ndo sheria mama ambayo Magufuli aliapa kuilinda na kuitetea.

Sawa, makubaliano yanaweza kuleta badiliko la muda la Katiba. Katiba hutungwa na watu na ni living document inayoweza kurekebishwa wakati wowote kwa maslahi ya taifa yaliyo wazi
 
Ndio maana nikasema, ili ku- minimize risks of leadership change na kuweka Tanzania mbele badala ya siasa, kwa kuwa sasa tunajua Magufuli ni mtu wa namna gani katika utendaji kama Raisi, ni bora tuijengee Tanzania misingi imara ambayo itafanya tusiwe tena na tatizo la kuwa na vipindi vya uraisi vya miaka kumi au nane hapo baadaye.

Great thinker! Hahaaaaaaaaaa!
Kweli Nchi ya Viwanda iko njiani.
 
Sawa Mkuu, labda Magufuli ana hilo tatizo. Lakini, katika suala zima la kuiendeleza Tanzania, unaona kama ni tatizo lake ni baya sana na ni afadhali tungekuwa na aina ya viongozi waliopita (ukiondoa Nyerere) kuliko Magufuli?
Ana nia nzuri lakini utekelezaji wake ni m'bovu, tatizo la rais wetu, hataki kusikiliza wala kusikia ushauri wa mtu mwingine ktk kuongoza nchi.

Nchi inabidi iendeshwe kitaasisi na ki-mfumo na sio jeshi la mtu mmoja.

Kwa staili yake ya uongozi mara leo akitutoka ghafla {God forbid} nchi hii inarejea kule kule tulipotoka.

Inabidi ajenge mfumo utakaowezesha yoyote atakaekuja apite humo
 
Back
Top Bottom