Ili Magufuli aibadilishe Tanzania, ni lazima awe Rais kwa zaidi ya miaka kumi

Huwa najitahidi kuongea ukweli, japo mara nyingine watu wananikasirikia. Nakumbuka mapema sana, kabla hata jina Bulldozer halijajulikana kitaifa na kimataifa, nilisema humu JF Magufuli ni mchapa kazi sana, lakini labda ningependelea awe na nafasi ya Waziri Mkuu badala ya Raisi, kwa sababu anafanya kazi kama bulldozer, nikimaanisha alihitaji mtu ambaye sio "impulsive" kumwongoza, kama ilivyokuwa kwa Nyerere na Sokoine. Baadaye nilishangaa kuona jina Bulldozer limemnasa Magufuli.

Sasa nitawaambia jambo jingine. Tanzania tumegawanyika kwa sasa, pro na against Magufuli. Huko nyuma nilisema pia Tanzania ilikuwa imefikia pabaya sana na hivyo labda ilikuwa vema na wakati muafaka kupata kiongozi wa namna ya Magufuli, angalau kwa miaka kumi. Lakini sasa najua kwamba miaka kumi haitatosha. Najua hii ni kauli ya kuleta hasira, lakini ndio ukweli wenyewe.

Hakuna Raisi duniani anaweza kuibadilisha nchi toka alipoikuta Magufuli kwa kipindi cha miaka kumi tu. Na hatari ya miaka kumi ni kwamba raisi atakayefuata anaweza kuharibu mazuri yote yaliyofanywa, kwa sababu yale mazuri yanakuwa hayajaota mizizi sawasawa (established sustainable systems). Na hiyo ni ukweli wa-kishule (academic truth) kwamba ili nchi iendelee inahitaji mipango ya muda mrefu isimamiwe na mtu ambaye yuko committed kuisimamia (committed leadership to implement strategic national development plans). Hakuna mpango wa muda mrefu wa kuiendeleza nchi utakaotekelezwa chini ya miaka kumi. Huo ndio ukweli wenyewe.

Ukiangalia historia ya mataifa yaliyoendelea haraka chini ya viongozi wao maarufu, utaona kwamba mafanikio ya nchi hizo hayakuletwa na viongozi waliobadilisha hizo nchi katika kipindi cha miaka kumi tu. Mifano mizuri ni Singapore, Malaysia na hata Rwanda. Singapore kwa mfano, kuna wakati fulani kiongozi wao alilalamikiwa, na hata kukasirikiwa kwa maamuzi magumu aliyofanya, lakini angalia alipoifikisha Singapore, toka taifa masikini sana. Ilimchukua miaka zaidi ya kumi kufanikisha hilo. Malaysia ni hivyo hivyo na Rwanda ndiko wanakoelekea.

Huwezi kuilinganisha Tanzania na nchi kama Marekani, ambao tayari wana "established systems" ambazo hazihitaji raisi mzuri kukaa madarakani zaidi ya miaka nane. Na mie ni wa kwanza kukubali kwamba ukiweka utarataibu wa kutokuwa na kikomo cha uraisi kabla hujampata Raisi mzalendo kama Nyerere au Magufuli, hatari ni kwamba unaweza kumpa nafasi raisi fisadi au mbovu akaharibu sana nchi. Mifano ya nchi za namna hiyo ipo mingi imetuzunguka.

Lakini sasa tunajua Magufuli ni mtu wa namna gani. Yapo ambayo sikubaliani na Raisi Magufuli, na hata kumkasirikia mara nyingine. Lakini ni mengi zaidi ninayokubaliana naye, hasa katika kukabiliana na ufisadi na kuleta nidhamu ya uwajibikaji. Watanzania tulilala sana, tulifikia uozo mbya sana. Niliwahi kuwaambia kuna mke wa raisi alimfokea kiongozi wa bandari kwa kukataa kuyatoa makontainer yake bila kuyalipia kodi. Aliitwa ikulu (na mke) na akaishia kuyatoa bila kupenda.

Na ukweli unabakia, kwamba, kama kweli Tanzania tunahitaji mabadiliko ya kutumia rasilimali zetu tuwe kama Singapore au Malaysia, basi mtu kama Magufuli anahitaji kuwa madarakani kwa zaidi ya miaka kumi. Najua hii ni lugha Watanzania wengi, na hasa vyama vya upinzani, hawawezi kuifurahia, lakini huo ndio ukweli. Baada ya hiyo miaka labda ishirini ya Magufuli, basi tunaweza kurudi tena kwenye uraisi wa kiindi cha miaka kumi au hata nane. Tutakuwa tayari tuna "established system" huenda hata kwa kiwango cha Singapore. Kama ikibidi vyama vya upinzani kuungana na CCM kwa sasa ili kufanikisha hilo basi na iwe hivyo.
Hongera ,Makala yako ni ndefu sana lakini inasomeka.

Sijakubaliana na wewe Katika hili,and I believe any honest human won't agree with you .Zero acceptance.

The truth is ,Magufuli aliaanza ku fail from the very beginning,before even six months in office .
Maguful ni Rais muoga Katika marais wote ambao wameshawai kutokea hapa Tanzania,kwanza ,anatengeneza jamii ya Uoga,ya kumuogopa,na hii ni sifa ya mtu wowote asiye na confidence kwenye mambo yake ,ni hatar sana kua na jamii ya Uoga Katika nchi ,the truth is Maguful hana talent ya kuibadil hii nchi ,anahitaji talent za watu waliomzunguka tena wawe free ku express the bad and the good ,kwa muheshimiwa hilo ni tafauti,he is just reactive guy and not proactive,so he will never get there ,trust me .

Pia ,Rais akil yake inadhan maisha ni just kukusanya kodi tu that is what he is thinking ,anatakiwa atengeneze vyanzo na misingi na opportunities ,ili apate kukusanya kodi za kutosha,mfano ,asilimia kubwa ya graduates wamesomeshwa na bodi,mpaka sasa kuna graduates wengi ikiwemo na hawa medical stuff,doctors etc etc wapo home hawana issue ,but walitumia pesa nyingi za bodi kusoma ,rais anakomaa walipe na mpaka majina yao yamewekwa kwa wadaiwa sugu,the president is not taking time to understand kua,kuacha kuwaajir hawa ni kwamba still government ina poteza pesa nyingi sana,kodi na malipo ya madeni yao serikali ina kosa yote hayo ,huo ni mfano mdogo tu but kuna mengi ya kuongea ,in short maguful hawez kufika huko unapodhan hata akipewa 30 years ,anaendesha nchi kihisia zaid kuliko ki uhalisia.Now ,this ,I accept kua it takes a character to be a leader .Unfortunately,
The Guy is missing that character .
 
Mwapachu wakati wa KAMPENI alisema mbio hizi za uchaguzi ni kati ya a leader akimaanisha lowasa and a manager akimaanisha magu....wengi hawakumuelewa ...natumai sasa mwapachu anaeleweka vizuri sana.
Lkn cha ajabu huyohuyo Mwapachu baada ya Magufuli kushinda uchaguzi akarudi CCM na kusema amegundua Jpm ni GREAT leader hahah
 
Huwa najitahidi kuongea ukweli, japo mara nyingine watu wananikasirikia. Nakumbuka mapema sana, kabla hata jina Bulldozer halijajulikana kitaifa na kimataifa, nilisema humu JF Magufuli ni mchapa kazi sana, lakini labda ningependelea awe na nafasi ya Waziri Mkuu badala ya Raisi, kwa sababu anafanya kazi kama bulldozer, nikimaanisha alihitaji mtu ambaye sio "impulsive" kumwongoza, kama ilivyokuwa kwa Nyerere na Sokoine. Baadaye nilishangaa kuona jina Bulldozer limemnasa Magufuli.

Sasa nitawaambia jambo jingine. Tanzania tumegawanyika kwa sasa, pro na against Magufuli. Huko nyuma nilisema pia Tanzania ilikuwa imefikia pabaya sana na hivyo labda ilikuwa vema na wakati muafaka kupata kiongozi wa namna ya Magufuli, angalau kwa miaka kumi. Lakini sasa najua kwamba miaka kumi haitatosha. Najua hii ni kauli ya kuleta hasira, lakini ndio ukweli wenyewe.

Hakuna Raisi duniani anaweza kuibadilisha nchi toka alipoikuta Magufuli kwa kipindi cha miaka kumi tu. Na hatari ya miaka kumi ni kwamba raisi atakayefuata anaweza kuharibu mazuri yote yaliyofanywa, kwa sababu yale mazuri yanakuwa hayajaota mizizi sawasawa (established sustainable systems). Na hiyo ni ukweli wa-kishule (academic truth) kwamba ili nchi iendelee inahitaji mipango ya muda mrefu isimamiwe na mtu ambaye yuko committed kuisimamia (committed leadership to implement strategic national development plans). Hakuna mpango wa muda mrefu wa kuiendeleza nchi utakaotekelezwa chini ya miaka kumi. Huo ndio ukweli wenyewe.

Ukiangalia historia ya mataifa yaliyoendelea haraka chini ya viongozi wao maarufu, utaona kwamba mafanikio ya nchi hizo hayakuletwa na viongozi waliobadilisha hizo nchi katika kipindi cha miaka kumi tu. Mifano mizuri ni Singapore, Malaysia na hata Rwanda. Singapore kwa mfano, kuna wakati fulani kiongozi wao alilalamikiwa, na hata kukasirikiwa kwa maamuzi magumu aliyofanya, lakini angalia alipoifikisha Singapore, toka taifa masikini sana. Ilimchukua miaka zaidi ya kumi kufanikisha hilo. Malaysia ni hivyo hivyo na Rwanda ndiko wanakoelekea.

Huwezi kuilinganisha Tanzania na nchi kama Marekani, ambao tayari wana "established systems" ambazo hazihitaji raisi mzuri kukaa madarakani zaidi ya miaka nane. Na mie ni wa kwanza kukubali kwamba ukiweka utarataibu wa kutokuwa na kikomo cha uraisi kabla hujampata Raisi mzalendo kama Nyerere au Magufuli, hatari ni kwamba unaweza kumpa nafasi raisi fisadi au mbovu akaharibu sana nchi. Mifano ya nchi za namna hiyo ipo mingi imetuzunguka.

Lakini sasa tunajua Magufuli ni mtu wa namna gani. Yapo ambayo sikubaliani na Raisi Magufuli, na hata kumkasirikia mara nyingine. Lakini ni mengi zaidi ninayokubaliana naye, hasa katika kukabiliana na ufisadi na kuleta nidhamu ya uwajibikaji. Watanzania tulilala sana, tulifikia uozo mbya sana. Niliwahi kuwaambia kuna mke wa raisi alimfokea kiongozi wa bandari kwa kukataa kuyatoa makontainer yake bila kuyalipia kodi. Aliitwa ikulu (na mke) na akaishia kuyatoa bila kupenda.

Na ukweli unabakia, kwamba, kama kweli Tanzania tunahitaji mabadiliko ya kutumia rasilimali zetu tuwe kama Singapore au Malaysia, basi mtu kama Magufuli anahitaji kuwa madarakani kwa zaidi ya miaka kumi. Najua hii ni lugha Watanzania wengi, na hasa vyama vya upinzani, hawawezi kuifurahia, lakini huo ndio ukweli. Baada ya hiyo miaka labda ishirini ya Magufuli, basi tunaweza kurudi tena kwenye uraisi wa kiindi cha miaka kumi au hata nane. Tutakuwa tayari tuna "established system" huenda hata kwa kiwango cha Singapore. Kama ikibidi vyama vya upinzani kuungana na CCM kwa sasa ili kufanikisha hilo basi na iwe hivyo.
Madictator huamini miaka term moja ya pili na ya tatu haitoshi kubadili nchi na hatimae huamua kwamba hatuondoki tena.Hata hivyo hushindwa kuleta maendeleo na badala yake huleta khofu kubwa.Raisi wetu kipenzi mungu amuepushie huko
 
Nimefuata mtoa maada alicho kisema tena nimetoa na mfano,
Wenzenu malaysia walidhani ufisadi ndio chanzo cha umasikin wao lakin waliambiwa sio.
Nimetoa mfano jinsi walivo tumia madini na kuimarisha muliundo mbinu.
Wenzetu walibadilika ki sera, sasa magufuli sera gani au sheria gani kabadilisha!!, wao walishusha kodi na regulatuons pia.
Hivi Magufuli kabadilisha nini!!? Sheria gan imechange!!?,sera ipi ime change, tuna faidika na madini?, umeona elim kama ina badilishwa!!?

Mi siyo hater wa Magufuli nimecheki mada nimeunganisha facts nimeona hakuna anacho fanya.
Mfano:waki isha wafanyakazi hewa tuta faidikaje ki uchumi!!?
Ili hizo sera Na sheria Unazopendekeza zirekebishwe kwanza lazima mindset Na Tabia Za watu zirekebishwe Na ndio anacho fanya magufuli , sheria Na sera bila productivitity ni bure , Na Kama Ina zungumzia sheria Na sera Sijui Kama kuna nchi iliyotushinda Kwa sera Za elimu bure, afya , Kilimo , dira ya maendeleo etc kilo chokosekana ni nidhamu ya Kazi Na uongozi nia ya dhati ndio maana tukafikia hapa tulipo sasa.
 
Ili hizo sera Na sheria Unazopendekeza zirekebishwe kwanza lazima mindset Na Tabia Za watu zirekebishwe Na ndio anacho fanya magufuli , sheria Na sera bila productivitity ni bure , Na Kama Ina zungumzia sheria Na sera Sijui Kama kuna nchi iliyotushinda Kwa sera Za elimu bure, afya , Kilimo , dura ya maendeleo etc kilo chi kosekana Na ni nidhamu ya Kazi Na uingozi ndio maana tukafikia tulipo sasa.
Mtu mmoja hawezi badili mindset ya wananchi na nchi bila utaratibu unaoeleweka , atu tu ni mkali .

Tuwe na katiba bora ya wananchi na Sera bora ya taifa kiuchumi, kielimu & kikodi then mtu hata akisema anainyosha nchi hapo sawa
 
Kwa hali ilivyo wazo hilo ni baya mleta mada, afadhali kama jamaa angekuwa Democrat , lakini kwa haya kuamka asubuhi katamka hivi na vile hapana jamani.

Vinginevyo hayo mawazo yanayochipuka yakipaliliwa na wabunge wetu hawa wa NDIYOOOOOOOO, basi tutaishi kama kuku wa kizungu
Hakuna nchi iliyoendelea kwa democracy.
 
Huyu hata apewe miaka 30 hawezi kufanya lolote la maana, hivi hamuoni? Huyu hakuna kitu.
 
Wahi mapema na ushahidi huo...wenzako wameanzisha mahakama ya mafisadi na kesi hakuna....lowasa yupo hawana ushahidi...mahakimu na majaji wamesomea kuhukumu kesi fasta ila serikali imekosa watuhumiwa.
Ameshathibitishwa na kamati ya mwakyembe inatosha kuanzia
 
Kusema kuwa kapambana na ufisadi kama tiki ya kumpa vipindi vinne hiyo peke yake haitoshi. Swali la kujiuliza, Je akikaa miaka 20 ataumalizaje huo ufisadi au hata kuupunguzaje huo ufisadi?, na je akiondoka baada ya hiyo miaka 20 atakuwa ameweka mfumo gani ili kupunguza huo ufisadi hata baada ya kuondoka kwake? Maana hawezi kutawala milele!
 
Ili hizo sera Na sheria Unazopendekeza zirekebishwe kwanza lazima mindset Na Tabia Za watu zirekebishwe Na ndio anacho fanya magufuli , sheria Na sera bila productivitity ni bure , Na Kama Ina zungumzia sheria Na sera Sijui Kama kuna nchi iliyotushinda Kwa sera Za elimu bure, afya , Kilimo , dira ya maendeleo etc kilo chokosekana ni nidhamu ya Kazi Na uongozi nia ya dhati ndio maana tukafikia hapa tulipo sasa.
Huwezi ukawafundisha watu wazima nidhamu, sheria na sera huwa hazisubiri watu, zinapangwa na kama ni nzuri utakuta tayari watu wana ji adjust kwenye mfumo mpya, unadhani nchi ni maskini kwa sababu ya nidhamu!!?, ukisimamisha ajira watu wana pataje nidhamu!!?, ukizuia kupanda mishahara watu wana pataje nidhamu!? Huyu anaweka uoga sio nidhamu.
Nchi ni maskini kwa kuwa tuna viongozi wasio na maono ya ki uchumi, unatoza VAT hadi kwenye benki halafu unasema ma benk ndio yana takiwa yalipe, wakat VAT sku zote humuangukia consumer wa mwisho. Hapo una muumiza mwana nchi na una discourage maendeleo.
Una lipa madeni ya nje una acha ya ndani!! Sioni haja ya kutetea poor thinking ya Magufuli.
Ajifunze Malaysia nao walijifanya wana anza hivo, wakaambiwa haisaiidii waka anza ku deal na sera kubwa, ila kumbuka ana elekea mwaka wa pili now, hakuna anacho fanya.
Naheshim ofis ya Rais lakin siheshim maamuzi yake na kitaalam hayawez kuja kuinua uchumi.
 
Tulikuwa Na Nyerere, Na sera Na dira ya Taifa , mipango wa maendeleo, Na taasisi ya kuzuia rushwa Na sheria Na sera zetu zilifuata kilichofanywa malasyia, India Na china , je ni wapo tulipokosea?? Ni kwenye utekelezaji kutokana Na uzembe.
Kaja Mwinyi Na kukaribisha wawekezaji kutoka semi- closed system to fully open system , tukashindwa, akaja Mkapa Na mambo ya nidhamu kidogo Na uwekezaji wa nje tukapigwa Na ajira zenye Maslaha wakapewa expatriate au watu walio soma nje, Na hata Leo hii utaambiwa wa Tz Wengi hawapo tayari Luganda Kazi kwenye mashirika ya kimataifa au multi national companies wanaoweza ni say 20% , akaja JK wa pili naye licha ya juju do zake Za kupata miss ads Kwa wingi Na Biashara huria watu wakawa eanapishana aangani , tupo kwenye hizi barabara zisizo Na viwango Na Biashara kila mahali hata Mbele ya Geti Lako watu wanaweza kuju kuwekeza Sasa Hapo sijui utaniambia sheria zinawaruhusu? Au sera Kama sio kukosa nidhamu tu ya kuzaliwa ambayo tumekata au tunachelea kuitumia.Nenda kapande daladala uone viti vilivyo banana Na basi likivyo chini ya kiwango utasema nalo linahitaji sheria Na sera Kama sio utekelezaji ?? Mwl kuhudhuria bioinformatics vyake nalo linahitaji sheria, ukienda Ardhi faili Lako limepotea nalo Lina hitachi sheria ???
 
Ni upuuzi mtupu kuilinganisha Rwanda na Tanzania.

Rwanda ni kama kamkoa kamoja tu ka Tanzania .
Hatuwezi kuilinganisha Rwanda na Tanzania.
Rwanda wanatumia kila mbinu kuihujumu kongo na rasilimali zake.
Kwa hiyo hatuwezi kujilinganisha na kanchi ka kiporaji.
Kujenga Barabara ya Lami kutoka Mtwara mpaka Karagwe ni sawa na kujenga barabara zote za Rwanda mpaka zile za majumbani kutoka jikoni kwenda chooni kwa kiwango cha lami. Gharama za Kutoa umeme wa gridi ya Taifa kutoka Ubungo mpaka Mwanza ni sawa na kuwawekea wanyarwanda wote umeme na vyombo vya umeme bure majumbani mwao.

Kujenga Bomba la Ges kutoka Mtwara mpaka Dsm ni sawa na kumpatia gesi ya bure kila mnyarwanda nyumbani kwake.
Kujenga Bomba la maji toka ziwa viktoria mpaka Kahama ni sawa na kumwekea maji bure kila Mnyarwanda.
N.k.n.k.
Kulinganisha Rwanda na Tanzania ni sawa na kulinganisha jua na Karabai.

Kuhusu Magufuli kutawala zaidi ya miaka kumi hiyo ni kauli ya uchochezi na ya kitoto kabisa.
Tatizo la waafrika ni unafiki.
Hata kundi la JK nao walimfurahia sana na kumwona kuwa ameiletea Tanzania na watanzania maisha bora na maendeleo makubwa.
Tatizo kila mtu anampenda kiongozi anayetawala kutokana na nafasi anayopewa. Ukipata ukuu wa wilaya kwenye awamu inayokuwepo basi unatamani aliyekuchagua aishi na kutawala milele.

Nyerere alipotaka kustaafua aliwaambia waliokuwa wanamsifia na kumtaka asing'atuke kwa kuwcla eti hatapatikana wa kuongoza nchi, aliwaambia kuwa wanataka aendelee kwa sababu wanahofia kupoteza nafasi zao.

Uislam ni dini inayokua kwa kasi sana na kila muislam muda wote anailinda na kuinusiru dini yake kutokana na sheria za dini hiyo ndani ya koran. Sheria na Katiba ndio kitu cha muhimu sana kwa nchi yenye watu wa dini na makabila tofauti.
Kama Magufuli anataka kuiacha nchi vizuri au kuinyoosha vizuri basi alete maadili na miiko ya uongozi kwenye katiba ili kila mtu ajipime kama anastahili kuwa kiongozi.
Kwa sasa kuna watu bado hawastahili kuwa madarakani lakini hakuna miiko ya kuwabana
maranyingi wadanganyika huwa tunajitetea Kijinga sana...kama Rwanda ni sawa na Mkoa kuna Mkoa gani huku kwetu unaofanana na RWANDA
 
Tulikuwa Na Nyerere, Na sera Na dira ya Taifa , mipango wa maendeleo, Na taasisi ya kuzuia rushwa Na sheria Na sera zetu zilifuata kilichofanywa malasyia, India Na china , je ni wapo tulipokosea?? Ni kwenye utekelezaji kutokana Na uzembe.
Kaja Mwinyi Na kukaribisha wawekezaji kutoka semi- closed system to fully open system , tukashindwa, akaja Mkapa Na mambo ya nidhamu kidogo Na uwekezaji wa nje tukapigwa Na ajira zenye Maslaha wakapewa expatriate au watu walio soma nje, Na hata Leo hii utaambiwa wa Tz Wengi hawapo tayari Luganda Kazi kwenye mashirika ya kimataifa au multi national companies wanaoweza ni say 20% , akaja JK wa pili naye licha ya juju do zake Za kupata miss ads Kwa wingi Na Biashara huria watu wakawa eanapishana aangani , tupo kwenye hizi barabara zisizo Na viwango Na Biashara kila mahali hata Mbele ya Geti Lako watu wanaweza kuju kuwekeza Sasa Hapo sijui utaniambia sheria zinawaruhusu? Au sera Kama sio kukosa nidhamu tu ya kuzaliwa ambayo tumekata au tunachelea kuitumia.Nenda kapande daladala uone viti vilivyo banana Na basi likivyo chini ya kiwango utasema nalo linahitaji sheria Na sera Kama sio utekelezaji ?? Mwl kuhudhuria bioinformatics vyake nalo linahitaji sheria, ukienda Ardhi faili Lako limepotea nalo Lina hitachi sheria ???
Yaan walicho fanya Mkapa na Kikwete ilikuwa ndio afadhali, lakini kosa moja lilikuwa ni kutumia sheria zile zile na taratibu lile lile ku adress matatizo mapya na dunia mpya. Hivo watu wana tumia loopholes kujipgia pesa.
Ndio maana nasema, toka tuingie na Magufuli sheria ipi imeweza kufanyiwa marekebisho!?, ni sera ipi mpya ya madini au gesi imekuja!? Na naongelea kuwa haija wahi tokea duniani kitu anacho fanya Magufuli sasa kika lenga kuleta maendeleo ya mwana nchi!? Na maisha ya watu wa Tanzania yata improve vipi kwa haya anayo yafanya!?
 
Kumbukeni jpm ni msikivu,hivyo ushauri kama huu ni hatari kwa mustakbali wa taifa au katiba ya nchi
 
Kiongozi yeyote asiye washirikisha wachumi na wataalam wa maendeleo..na uhusiano thabiti wa mataifa kwa manufaa ya pende mbili win win solution
Kilimo na elimu kisipo pesa kipaumbele kwa hali ya juu basi twaafwaa
Kiongozi anae Fanya siasa inayo fuata mfumo wa science yaani anabase kwenye utafiti..kuliko masilahi ya wachache yaan interest of minority kwenye mgongo wakuwalubuni majority na kuwalubuni...maendeleo ni ngumu
Tatizo ni mfumo unabase kwenye chama badala ya kubase kwenye masirahi ya Watanzania wore..ndio chama baadae
 
Back
Top Bottom