Ili Magufuli aibadilishe Tanzania, ni lazima awe Rais kwa zaidi ya miaka kumi

aisee! Na JK angehitaji miaka mingapi kufikia malengo yake!
 
Sawa, makubaliano yanaweza kuleta badiliko la muda la Katiba. Katiba hutungwa na watu na ni living document inayoweza kurekebishwa wakati wowote kwa maslahi ya taifa yaliyo wazi
Uko sahihi mkuu,

Lakini kwenye suala la katiba, mkulu alishasema sio kipaumbele chake kwa sasa. Labda akikubali kushaurika!
 
Kwa hiyo tuko kwenye ilani za mfukoni siyo?

Hapana, Ilani nyingi zina maneno mazuri tu, za CCM, Chadema nk. Tatizo ni kwamba zinaandikwa kama marketing docuemnts zaidi ya kuwa long term development strategies ambazo zitazaa practical and sustainable development plans.

Leo hii nikienda kwa Magufuli nikamwomba anionyeshe national development strategy na plan, akanipa Ilani ya uchaguzi ya CCM, nitamwambia wazi kwamba "Mr. President, you are not serious".

Ilani ya Uchaguzi ya chama inalenga zaidi kukifanya chama kishinde uchaguzi. Pure marketing stuff.
 
aisee! Na JK angehitaji miaka mingapi kufikia malengo yake!

One term for JK was one too many! Na kama ulivyosema, yalikuwa malengo ya JK. Tunajua kwa dhati Magufuli hayupo kutekeleza malengo yake, pamoja na mabaya yote tunayoona kama anafanya.
 
Tulio wengi humu hatuna majibu ya kuendeleza taifa letu,bali tunajua yaliotukuta na kutunyima maendeleo.
Ni ukweli kuwa Singapore na Malaysia wapo juu,japo wao na sisi mwanzoni tulikuwa sawa,pili Viongozi wa mwanzo wa nchi hizo walikuwa marafiki na lika mmoja na Raisi Nyerere.Wao wakapasua maendeleo yeye akaziba maendeleo.
Vivyo hivyo waliofuatia maraisi wengine 3 miaka 30 baadae nao wamelamba magalasa tu.
Mpe Raisi Magufuri miaka minne ikiobakia tutaweza kumpima.
Yawezekana ameanzia kwanza kusafisha maovu ndio aanze kujenga upya Taifa.
 
Uko sahihi mkuu,

Lakini kwenye suala la katiba, mkulu alishasema sio kipaumbele chake kwa sasa. Labda akikubali kushaurika!

Mkuu, alikuwa akiongelea mabadiliko ya Katiba yaliyoanza kipindi cha JK. Sio kwa hili suala. Na nisingependa kuona suala na utawala wa raisi usio na kikomo liwe jambo la kudumu katika katiba, ndio maana nikasema kwa Magufuli linapaswa liwe jambo maalum la muda kutupeleka katika milestone fulani.
 

I hear you Mkuu, lakini huenda hiyo staili ya Magufuli ndio inayohitajika kwa sasa, ikiwa ni sehemu ya kujenga nidhamu, uwajibikaji na kumaliza ufisadi. Umefikiria juu ya hilo? Suala la kujiuliza ni kwamba, je katika yote anayofanya, hata yale tunayoona kuwa mabaya, lengo lake ni nini? Kujinufaisha yeye binafsi na kikundi fulani cha watu, au ni kwa ajili ya faida yetu na Tanzania kama nchi? We have to see further than the end of our noses katika kila Magufuli analofanya au kusema. Mfano hapo juu, watu wanasema alinunua ndege badala ya dawa; je kwa nini? Alitumia fedha za dawa kununua ndege? Alinunua ndege ya raisi? Au alifanya sacrifice kidogo ya muda mfupi kwa lengo la kujipa uwezo mkubwa na wa muda mrefu wa kununua dawa baadaye?

Mara ngapi sisi binafsi tuna sacrifice vitu ili kufanikisha lengo fulani kutia ndani kuwa na nyumba, kusoma chuo nk? Mara nyingine hata mama zetu wazazi hatuwatumii hela ili kufanikisha lengo fulani. Basi tuhukumiwe kama tunavyomhukumu Magufuli juu ya ndege kwa kukosa dawa kwa miezi miwili sijui? Na kweli tulikosa dawa kabisa?
 
Watanzania Ndio wana jukumu la kuibadili Tanzania waitakayo na si vingnevyo
 
Kumbe kuipoteza Tanzania kabisa katika ramani ya Dunia ni kuibadilisha!!!!!!!!!!!!!!!. Huu mmoja tu tumepotea kabisa akifikisha mitano???. Mungu tusaidie
 
propaganda hizi ungezihamishia kwenye njaa ,migogoro ya wafugaji na wakulima ,kero za maji mjini na vijijiini ,ueleze kwa mapana na marefu na ung,ate na kupuliza jamii ingeelimika Zaidi .
 
Mmeanza kidogo kidogo kushawishi watawala kuchezea katiba,acheni ushawishi ambao ni hatari Kwa usalama wa taifa ww ndio unamwona ni rais anayefaa kuendelea kukaa uongozini, ni lazima utaratibu tuliojipangia utekerezwe, hakuna cha kupendwa au kutopendwa!
 
propaganda hizi ungezihamishia kwenye njaa ,migogoro ya wafugaji na wakulima ,kero za maji mjini na vijijiini ,ueleze kwa mapana na marefu na ung,ate na kupuliza jamii ingeelimika Zaidi .

Na haya yote unayosema, njaa, migogoro ya wafugaji na wakulima, kero za maji mjini na vijijiini, hayakuwapo huko nyuma ila yameletwa na Magufuli? Na kile Magufuli anachokazia kila siku juu ya viongozi kuhakikisha wanashughulikia matatizo ya wananchi la sivyo atawatumbua, kinahusu nini hasa?

Kuna watu hapa Tanzania, hata mngeletewa malaika wa mbinguni awe raisi wa nchi hii bado mtalalamika kwamba hafai. Kizazi cha uvivu, uzembe na ufisadi.
 

Unajua Mkuu, wewe ukiwa chama cha upinzani, hata Magufuli awe anafanya mazuri kiasi gani, bado tapendelea chama chako kishinde uchaguzi ili aondoke. Hilo nalielewa. Sasa mie siangalii chama wala Magufuli, na wala sisemi haya kwa kuwa nampenda Magufuli, bali kwa kuwa napenda anachofanya na nilitamani atokee mtu katika Tanzania wa kufanya anachofanya Magufuli, iwe wa Chadema, CCM, CUF, TLP nk. Sasa nisingependa kuona anachofanya Magufuli kinafikia mwisho baada ya miaka kumi na tunarudi kule kule kulokonifanya nitamani atokee mtu kama Magufuli Tanzania.

Sasa siko tayari kuona nchii hii ikiharibiwa ili mradi tu tufuate utaratibu, hata kama huo uratatibu unatupeleka kubaya. NIkiwa manager, kuna wakati niko tayari kuvunja urataibu pale ninapoona inabidi kuvunja uratatibu kwa manufaa makubwa kubwa zaidi ya yale yatakayoletwa na utaratibu iliopo.
 
Hakuna maendeleo bila demokrasia kwani ujenzi wa taifa lazima kukubali kukosolewa ili ujirekebishi huwezi ukilala na kuota jambo asubuhi unalitolea matamko na uongozi ni fomula!
 
Naunga mkono hoja, siyo rahisi kumpata mzalendo kama Mh.Magufuli ambae anaweza hata kuwaambia wana CCM,CDM NA WENGINE waache ufisadi, ni nadra sana kupata raisi wa hivyo, ona tangu aondoke nyerere na sokoine, mpaka 2015 ndo tukampata Mh. magufuli. Hata vivyo najua wanao taka uraisi ili wapige dili hawawezi kufurahia hili pendekezo kwakuwa nao wanataka waingie ikulu ili waibe, ila kiukweli Mh. magufuli ana deserve kuongezewa atleast awamu mbili (mihula minne) ili atusogeze walau tuwe kwenye dunia ya pili kiuchumi au hata ya kwanza, nikiangalia hata ndani ya chama, sijaona anae weza kuwa mzalendo kiasi hicho, wengine wanapewa wizara hatujaona kinacho fanyika kwa kasi anayo itaka mh.magufuli.
 
Labda ni afadhali tuishi kama kuku wa kizungu wanaokula chakula kinachojulikana na kupewa huduma muhimu kuliko kama kuku wa kienyeji wanaoswaga kila kitu kitia ndani kinyesi.
Afadhali ya kuku wa kienyeji ana akili ya kujitegemea, sio wa kizungu kila kitu kupimiwa kama mnavyotaka kutupimia . Hatukupigania uhuru ili tutawaliwe tena kama hivyo mnavyotaka
 

Kwani nini kuna tatizo gani na marketing?

Naona hauko serious!
Ebu pitia ila ya CCM 2015.
ilani ya uchaguzi ya ccm kwa ajili ya - JamiiForums

 
Awe wa ƙuɗumu milele na milele Amina.Mɓona kardinal habadilishwi,..
 
Kwani nini kuna tatizo gani na marketing?

Naona hauko serious!
Ebu pitia ila ya CCM 2015.
ilani ya uchaguzi ya ccm kwa ajili ya - JamiiForums

Siko serious? Unajua maana ya marketing lakini? Yaani wewe ukiambiwa Aspro mbli kwa magonjwa ishirini basi unaamini hata kwa daktari hutaki kwenda tena? Unafikiri ni kwa nini walilazimishwa kuongezea mwisho wa matangazo "maumivu yakizidi muone daktari"?

Nitarudia tena. Lengo la la msingi la Ilani ya uchaguzi ni kukiuza chama kwa wapiga kura.
 
Afadhali ya kuku wa kienyeji ana akili ya kujitegemea, sio wa kizungu kila kitu kupimiwa kama mnavyotaka kutupimia . Hatukupigania uhuru ili tutawaliwe tena kama hivyo mnavyotaka

He, mlipigania uhuru nyie?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…