Ili nipate uteuzi ni lazima kuwa kada wa CCM au niwe Chawa wa Mama?

1. Uwe na unatashi wa kupata kazi unayoitaka.
2. Uwe well connected na watu sahihi kama mapadre, mkuu wako wa kaz, chama, usalama na wizaran

3. Mlengo wa kisiasa ujulikane, umtukuze mama

4. Pesa, kwa ajiri ya nauli, kuhudumia koneksheni na kuhonga itakapobidi.
Naomba ufafanuzi hapo kwa mapadre tu. Hao watu kwani wana uhusiano na serikali ya mama
 
INTRODUCTION
Eeh bwana ehh habari zenu

Nikiri Mimi sio shabiki kabisaa wa siasa. Yaani sina Kadi ya chama chochote na sifikirii kuwa na Kadi ya chama chochoteee kileee.

Na kifupi huwa sifatilii zile habari za siasa zaidi ya hizi ambazo zinapostiwa insta kwenye page za habari za labda msingwa, Ikulu, na Wizara.

Mimi ni mtumishi wa halmashauri, Elimu yangu ni Bachelor of Science in ..... na Masters of Science in ....., na nina miaka 10 kazini Halmashauri (experience).

SCENARIO
Juzi mama alivyoteua ma-DC Kuna jambo nikakumbuka, nimeoma niwashirikishe ili mnipe jibu.

Kipindi kile mama alivyomteua nadhani Mkuu wa Magereza nilikua Dodoma kwenye semina Morena Hotel.

Sasa tukiwa tunapiga breakfast seminani zikapita gari V8 kaliii nyeusi na ving'oro pale kwenye lami ya Morena, kwamba Mkuu wa Magereza anaenda Ikulu kuapishwa.

Mimi nikaropoka "Mimi huyo miaka 5 ijayo nitapanda hizo gari nikielekea Ikulu kuapishwa baada ya kula uteuzi wa Mama"

Sasa tukiwa pale mezani jamaa mmoja akaniuliza "Una Kadi ya Chama?" Jibu likawa hapana. Ila tulipiga story na vitu vingiii kuhusu uteuzi na CCM, ila niliondoka na hili.

PROBLEM
Ili upate uteuzi haijalisha muda wako wa Kazi (Experience/duration), Haijalishi Elimu yako, ila KINACHOTAKIWA UWE NA KADI YA CHAMA CCM.

Kwamba, hata upige Kazi vipi ofisini ila ili uonekane Basi ni lazima uwe na Kadi ya CCM. Yaani ukitaka tobo la uteuzi basi shikiria Kadi ya CCM na uitangaze kama unayo, yaani ishi ki-CCM.

QUESTION

Sasa Je, ni kweli hili jambo ni sahihi? Kwamba pamoja Nina Miaka 10 serikalini na elimu ya Masters ila bado natakiwa kuwa Kadi ili mama anione mimi mtumishi wake Bora huku Kijijini?

(Halmashauri yetu ni Chaka/vijiji hasa)

Yaani ili nilambe uD(R) C, uDED, uD(R)AS, na vyengine ni lazima nijinadi ndani ya CCM na kuwashughulika na hoja za wapinzani mpaka mama atakaponisikia na kuniona?

Kwamba nikiwa hivihivi Neutral (kama nilivyosasa sina Kadi) basi hata nipige Kazi haswa ila NISAHAU UTEUZI?

#YNWA
Huo ujinga aliuleta mpumafu Mmoja Magufuli. . huwezi teua from nowhere paaaa ... Mkurugenzi hata file movement hajui... Paaa DC ... Hata Decentralization Act (Sheria ya Ugatuaji wa Madaraka) inakataaa akajiwahi ...walipohoji ... Mara Vuuuu akaivuta TAMISEMI (TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA ambayo inatakiwa kikatiba na kisheria kusimamiwa na Waziri Mkuu) akaivuta kwake paaaaap... Asihojiwe ..na huyu mama naye kaingie mkenge mnamsifu tu ... Waziri Mkuu Kwa sasa ni Ceremonial Figure tu hana mamlaka yeyote .... Ni kidole pistol ...
 
Huu uzi utamuumiza sana yule member anaitwa Lucas Mwa-farm!
Maana alijua chawa pro max na promo kibao majukwaani lakn kapigwa kata funua kwenye teuzi sasa hv hata keyboard haijui.
Tumtegemee siku chache zijazo abadili ID af aanze kuiponda sirikali
 
Hata mimi sijui, lakn mdogo wangu alipata uteuz ngaz ya kata kwa kupendekezwa na paroko kwa RAS kwenye gambe.

dogo anapga noti tu, hata hajui kuna mishahara.
 
Uteuzi Gani huo wa level ya kata una mkwanja hivyo?

#YNWA
 
INTRODUCTION
Eeh bwana ehh habari zenu

Nikiri Mimi sio shabiki kabisaa wa siasa. Yaani sina Kadi ya chama chochote na sifikirii kuwa na Kadi ya chama chochoteee kileee.

Na kifupi huwa sifatilii zile habari za siasa zaidi ya hizi ambazo zinapostiwa insta kwenye page za habari za labda msingwa, Ikulu, na Wizara.

Mimi ni mtumishi wa halmashauri, Elimu yangu ni Bachelor of Science in ..... na Masters of Science in ....., na nina miaka 10 kazini Halmashauri (experience).

SCENARIO
Juzi mama alivyoteua ma-DC Kuna jambo nikakumbuka, nimeoma niwashirikishe ili mnipe jibu.

Kipindi kile mama alivyomteua nadhani Mkuu wa Magereza nilikua Dodoma kwenye semina Morena Hotel.

Sasa tukiwa tunapiga breakfast seminani zikapita gari V8 kaliii nyeusi na ving'oro pale kwenye lami ya Morena, kwamba Mkuu wa Magereza anaenda Ikulu kuapishwa.

Mimi nikaropoka "Mimi huyo miaka 5 ijayo nitapanda hizo gari nikielekea Ikulu kuapishwa baada ya kula uteuzi wa Mama"

Sasa tukiwa pale mezani jamaa mmoja akaniuliza "Una Kadi ya Chama?" Jibu likawa hapana. Ila tulipiga story na vitu vingiii kuhusu uteuzi na CCM, ila niliondoka na hili.

PROBLEM
Ili upate uteuzi haijalisha muda wako wa Kazi (Experience/duration), Haijalishi Elimu yako, ila KINACHOTAKIWA UWE NA KADI YA CHAMA CCM.

Kwamba, hata upige Kazi vipi ofisini ila ili uonekane Basi ni lazima uwe na Kadi ya CCM. Yaani ukitaka tobo la uteuzi basi shikiria Kadi ya CCM na uitangaze kama unayo, yaani ishi ki-CCM.

QUESTION

Sasa Je, ni kweli hili jambo ni sahihi? Kwamba pamoja Nina Miaka 10 serikalini na elimu ya Masters ila bado natakiwa kuwa Kadi ili mama anione mimi mtumishi wake Bora huku Kijijini?

(Halmashauri yetu ni Chaka/vijiji hasa)

Yaani ili nilambe uD(R) C, uDED, uD(R)AS, na vyengine ni lazima nijinadi ndani ya CCM na kuwashughulika na hoja za wapinzani mpaka mama atakaponisikia na kuniona?

Kwamba nikiwa hivihivi Neutral (kama nilivyosasa sina Kadi) basi hata nipige Kazi haswa ila NISAHAU UTEUZI?

#YNWA
Kwani mkuu hukuona teuzi za ma DED kuna vitoto vidogo vikada vikipewa uDED wakati eneo hilo hilo kuna wakongwe kama wewe mnao jua halmashauri nje ndani?
 
kama unafanya kazi halmashauri hakikisha unakua mkuu wa idara, hapo ndio utaanza kuisogelea mbingu. otherwise kuwa mvumilivu
 
Back
Top Bottom