in fact,
Tanzania imejaaliwa na kusheheni watu wazalendo na wachapakazi mno huku wavivu wachache kutwa kulalamika tu.
Lakini pia Tanzania imejaaliwa ardhi kubwa, nzuri sana na yenye rutuba mno. Ajira bwerere za kutosha waTanzania wote ziko shambani na wengi wanachapa kazi vizuri mno. Lakini wachagua kazi na wavivu wachache wapo wanazurura tu mijini na hawana mbele wala nyuma wakijipa matumaini eti siku moja watatoboa. Sasa sijui watatoboaje kwa kuzurura.
Tanzania,
ina mfumo wa siasa za safi za vyama vingi. Kila mTanzania yuko huru, ana haki na uhuru wa kuanzisha chama cha siasa au kujiunga na chama chochote cha siasa kadiri apendevyo. Tuna mfumo huru wa uchaguzi kwa mujibu wa katiba na tu tume huru ya uchaguzi iliyoundwa kwa mujibu wa katiba na ndio maana demokrasia ya Tanzania inasitawi kila uchwao.
Tangu uhuru,
Tanzania imebarikiwa kua na uongozi safi unaotokana na matakwa ya wananchi kupitia sanduku la kura, mfumo ambao utaendelea kutupatia uongozi safi na madhubuti wa taifa letu, regardless ya setbacks za vibaraka wa mabwenyenye ya magharibi.
So,
TANZANIA ina watu, ardhi,siasa safi na uongozi bora kama ilivyo asisiwa na wapigania uhuru wa taifa letu na ndio maana we are currently more united, powerful and more stronger than before kisiasa, kijamii, kiuchumi kitaifa na kimataifa 🐒