Robert Heriel Mtibeli
Platinum Member
- Mar 24, 2018
- 40,153
- 93,069
Anaandika, Robert Heriel
Mtibeli
Watu wengi husubiri siku nzuri zije, nafasi ijitokeze, au mtu fulani abadilishe maisha yao. Lakini maisha hayabadiliki kwa sababu muda umepita; hubadilika pale fikra, maamuzi na tabia za mtu zinapoanza kubadilika.
Maisha yako hayabadilishwi na kile unachofikiri na kuamini pekee. Maisha yako yatabadilika kwa kuchukua hatua, kuthubutu na kufanya kwa vitendo.
Kuna siri watu wengi hawaijui. Siri ya kitibeli. Dunia ina react na actions and motions not words and ideas. Kwamba Dunia yako inajibu kwa matendo na mijongeo yako na soo maneno na mawazo yako. Wanasema maneno hayajengu ghorofa.
Maskini wa kweli si yule asiye na fedha pekee, bali ni yule aliyeridhika kuishi maisha ya jana wakati dunia inaishi kuifuata kesho. Akili inayokataa kujifunza, kubadilika na kuwajibika hujijengea gereza lisiloonekana.
Ukibaki ukisubiri mazingira yakubadilikie kabla hujabadilika wewe, kuna uwezekano mkubwa miaka itapita, lakini maisha yabaki palepale. Mabadiliko ya nje huanza na mabadiliko ya ndani. Pale unapobadilisha mtazamo, nidhamu na matendo yako, ndipo maisha nayo huanza kubadilisha mwelekeo.
Hakuna wa kubadili maisha yako isipokuwa Wewe mwenyewe kuchukua hatua.
Sio mimi Mtibeli.
Sio Tundu Antipas Lisu.
Sio Samia Suluhu,
Sio Chadema wala CCM,
Sio Mwamposa wala sheikhe Kipoozeo.
Sio Mganga wa kienyeji.
Hakuna. Kesho yako iko mikononi mwako. Wewe ndiye wakuibadilisha.
Nimemaliza.
TaikonMaster
Kwa sasa Dar es salaa.