Ilikuwaje mara ya kwanza ulipokutana na mtu mliyechati mtandaoni kwa nia ya kuwa wapenzi?

Ilikuwaje mara ya kwanza ulipokutana na mtu mliyechati mtandaoni kwa nia ya kuwa wapenzi?

Matongee

JF-Expert Member
Joined
Jun 17, 2023
Posts
1,056
Reaction score
2,729
"Samahani sana ninavyokuona sio kama nilivyotegemea, HATUENDANI"... baada ya kusema hivyo jamaa aliyekuwa naye kwenye Toyota Hiace nyeupe akaniangalia na kutabasamu kisha akaondoa gari. Mimi nikaachwa nimesimama. Kibaya zaidi hata kwenye gari hakushuka. Sikuweza kujua yule kijana alikuwa nani yake hadi leo. Ilitokea Arusha maeneo ya Njiro nje tu ya Njiro Complex (Bugaluu).

Mwaka 2007 kupitia mtandao wa marafiki.com niliweza kupata mchuchu mwenye asili ya kiasia na kuanza kuchat naye. Chats zilikuwa nzuri sana za kuvutia utadhani tumejuana kitambo sana. Siku tunakutana kwa mara ya kwanza nje ya Njiro Complex ndo akakata tamaa na kunijibu kama nilivyoandika kwenye aya ya kwanza. Ilikuwa ni aibu kubwa sana kwenye haya maisha yangu. Bahati nzuri hakukuwa na mtu niliyeenda naye eneo la tukio kwahiyo aibu ilikuwa ni yangu binafsi.

Ila sikumchukia wala kumlaumu yule binti wa kishua kwa sababu kwa wakati ule kweli nilikuwa nimepigika haswa. Yaani nilikuwa mwembamba ila ule wembamba wa lishe duni. Kiufupi nilikuwa nimekonda. Kama unavyojua mtu mwenye njaa ndo mwenye sura mbaya kwahiyo hata mimi nilikuwa mtu mwenye sura mbaya sana kwa hisani ya NJAA. Zilikuwa nyakati ambazo kutembea kwa mguu kutoka Mianzini hadi Mbauda ni kitu cha kawaida sana. Au wakati mwingine Clock Tower - Njiro ilikuwa jambo dogo. Akitembea tajiri huwa ni matembezi ya hisani ila mimi sijui ilikuwa matembezi ya kuchochea umaskini?

Nakumbuka mwaka 2010 ndo nilipata matumaini makubwa sana baada ya manzi mmoja wa Chalinze kuniambia mimi ni handsome. Huyo manzi nilikutana naye nilipokuwa natoka Iringa kuchukua cheti cha form six.

Kimsingi baada ya tukio la 2007 nikaanza kuogopa sana kutongoza demu mtandaoni. Hadi leo nikiona manzi mtandaoni huwa hadi nifuatilie sana kumjua kiasi na sio kukurupuka.
 
Hatukuwahi kuonana tena. Ila hadi sasa hata atakuwa mama wa watoto kadhaa.
Huyo manzi ukikutana nae tena wewe utamuonea yeye huruma kwa alivyo chokaaa.

Kuna demu wangu wa kishua aliniwacha kwa jeuri nimeonana nae mwaka jana amebaki Oohh wangu wa zamani sijui bado unanipenda?.

Nilimwambia kibwengo wewe mimi wa nini katafute urefu na uzuri kwanza ndio uje tuongee.
 
Alinambia "kumbe una komwe mchongoko kiasi hicho mahi wangu, mbona kwenye picha halionekani au ulilipeleka likizo".

Nikalia, nikabubujikwa machozii mimi. Chozi moja la jicho la kushoto likashuka likadondoka na kugonga mabuti yangu ya kimgambo. Akanisonkola na kidole kwenye kichwa huku akinifyonyaa....

Nililia, nilimwaga machozi pipa tatu, nikazimiaa nikajikuta nimelazwa wodi ya wagonjwa wenye upungufu wa maji mwilini chini ya usimamizi wa DR Mambo Jambo

Extrovert Poor Brain mshamba_hachekwi
 
Back
Top Bottom