Ilikuwaje Mkoa wa Mara ukaitwa 'Jamhuri ya Watu wa Chui'?

Ilikuwaje Mkoa wa Mara ukaitwa 'Jamhuri ya Watu wa Chui'?

Kwa nn sasa hawajatufundisha haya mambo mashuleni? Basi hata haya kwenye historia tunayoyajua ni fake.
 
Wakuu kwakweli kama kuna mambo yanayoumiza na kuhuzunisha ni kipindi hicho watu wa mara walitendewa unyama mbaya sana yaani ilifika hatua vijana wakalazimishwa kulala na mama zao na baba na mkamwana wake wanafanya tendo la ngono tena mchana mbele za watu kisa wanaombwa bunduki kuna watu hata leo wako tayari kutoa ushahidi na wengine wanawafahamu pili sababu kuu hasa ya nyamaghanya kutangaza taifa huru la ENGWE ni manyanyaso ya nyerere kukusanya ng'ombe za watu kipindi cha vita ya kagera kwamba wanachangia vita ya kagera sasa kuna bwana mmoja alikuwa akiishi kagera akaja pale gibaso akamwambia Amiri jeshi mkuu wa jamhuri ya watu wa engwe kwamba uganda haikuvamia tanzania bali ikuwa ni mbinu ya mwalimu kumsaidia obote hata lile daraja lilipigwa na jeshi letu la tz nyamaghanya aliposikia hivyo akaitisha mkutano mkubwa GWITÖNGA akauliza vijana je mpo tayari kutetea mifugo na watu wenu ndindipo wote wakajibu tuko tayari siku hiyo saa tano na nusu usiku wimbo wa taifa tukufu la engwe ukapigwa na kupandisha bendera ya ngozi ya chui nina ushahidi na vielelezo hata mkivitaka leo wakuu ina umma sana kwa unyama ambao watu wa mara walitendewa na askari toka zanzibar ni kitu ambacho sintakisahau kamwe!!

Mi nafikri wewe na wenzio wenye kampeni kama hizi ni wahaini
Na mnafaa kushitakiwa au kunyongwa kwa uhaini!!!
Una separatism idea n kutetea ujinga
 
Kama mtakumbuka miaka ya 1985 ilianzishwa oparation maalum ya kurejesha silaha ilikuwa kwa mwaka mara mbili wilaya ya Tarime na Serengeti
Walikuwa wanatembea askari jeshi 10 wakifika kwenye mji ni lete siraha vijana na wazee wenye nguvu walichezea kichapo ko ilikuwa ikifika hicho kipindi wanabaki watoto na vibabu na vibibi home
Nakumbuka babu aliombwa silaha akaleta biblia alikuwa msabato wakacheka muda huo bibi kaleta busara (togwa) wakanywa wakasonga kwa jirani ni virugu tupu wanachanja po pote tu hawafatishia njia mara pa kijana wa jirani kajiachia kwenye jiwe anang’oa funza kwenye vidole vya miguu anaulizwa na wewe akajibu shikamo, kaulizwa unafanya nini nichimbonde nkwiha (najitoa funza) kipigo lete siraha akapiga yowe wakaenda kwa brother’ake kile kishindo tu cha buti zao pale home na mikwara tu alikuwa dalini akalopoka ni olongo nde (nipo dalini) huku anashuka kujileta kwenye kipigo na kuambiwa amkubatie shemeji’ake
Yaani kwa ujumla ilikuwa ni fedheha na udhalilishaji ambao kwa sasa unahitaji fidia kubwa mno.
Matokeo yake vijana enzi hizo walikuwa wakiona askari polisi wanakimbia bila sababu wanatokomea pasipojulikana baadae night ndo watarudi makwao.
 
Nyamhanga aliteremsha Bendera ya Tanzania na kupandisha ngozi ya chui na kutangaza rasmi kuwa hiyo si tena Tanzania , kuanzia siku hiyo majeshi yalikusanywa nchi nzima kama vile kulikuwa na vita ya Kagera.

Mapambano yaliendelea kwa siku zipatazo 7 hivi kabla ya Nyamhanga kupitia chini ya nyuma ya mtungi na kupotelea bondeni.

Kama ilivyokuwa kwa Hitira kuna habari za kutatanisha kuhusu huyu bwana baada ya vita kwisha. Kuna wengine wanasema yalitupwa mabomu mengi sana huko alikokimbilia na wengine wanasema alitorokea nje ya nchi.

Kuna Simulizi nyingi tu ambazo siwezi kuziandika hapa hasa kwa sababu zinahusiana na ushirikina wake, nami sina imani na ushirikina.
kipindi hicho nilikuwa Mugumu mkoa mzima ulisafishwa siraha zote zilichukuliwa mpaka kisu.

Ffu jwtz walitapakaa mkoa mzima.chini ya utawala wa mchonga.mabasi yalipitia arusha kwenda tarime kirumi hapakupitika kwa usalama. Daaaa mara kiboko
 
Kama mtakumbuka miaka ya 1985 ilianzishwa oparation maalum ya kurejesha silaha ilikuwa kwa mwaka mara mbili wilaya ya Tarime na Serengeti
Walikuwa wanatembea askari jeshi 10 wakifika kwenye mji ni lete siraha vijana na wazee wenye nguvu walichezea kichapo ko ilikuwa ikifika hicho kipindi wanabaki watoto na vibabu na vibibi home
Nakumbuka babu aliombwa silaha akaleta biblia alikuwa msabato wakacheka muda huo bibi kaleta busara (togwa) wakanywa wakasonga kwa jirani ni virugu tupu wanachanja po pote tu hawafatishia njia mara pa kijana wa jirani kajiachia kwenye jiwe anang’oa funza kwenye vidole vya miguu anaulizwa na wewe akajibu shikamo, kaulizwa unafanya nini nichimbonde nkwiha (najitoa funza) kipigo lete siraha akapiga yowe wakaenda kwa brother’ake kile kishindo tu cha buti zao pale home na mikwara tu alikuwa dalini akalopoka ni olongo nde (nipo dalini) huku anashuka kujileta kwenye kipigo na kuambiwa amkubatie shemeji’ake
Yaani kwa ujumla ilikuwa ni fedheha na udhalilishaji ambao kwa sasa unahitaji fidia kubwa mno.
Matokeo yake vijana enzi hizo walikuwa wakiona askari polisi wanakimbia bila sababu wanatokomea pasipojulikana baadae night ndo watarudi makwao.
muraaa tata chui land
 
Kuna mjinga mmoja kutoka Mara ndio alikuwa anajiita IDD AMIN wa pili, alishauaga Chui ndio akaona kuwa anaweza kuua yeyote yule.

Kuna kipindi alipandisha ngozi ya chui aliyemuua juu na kushusha bendera ya Taifa...sasa kwasababu Wajinga walikuwa wengi wakati huo basi wakawa wanamsifia tuu na kumtukuza kwa huo ujinga

Kwa jamii ilivyostaarabika sasahivi asingefikia kupata hizo credit za kijinga.

Wewe ndio mjinga, unaongea kitu ukielewi.
 
hazina mantiki
pia zinachochea uovu tu!!
kwa sababu binadamu wenye mawazo kama ya hao watu wapo, kwahiyo utakapomfundisha mwanafunzi unamjengea hali ya kuwa "kumbe inawezekana eeh"

baada ya miaka unakuta wamejaa wa hivo tele

Mbona Historia ya mapinduzi imewekwa wazi?.
 
Mi nafikri wewe na wenzio wenye kampeni kama hizi ni wahaini
Na mnafaa kushitakiwa au kunyongwa kwa uhaini!!!
Una separatism idea n kutetea ujinga

Ujinga kwako. Usilazimishe usilolipenda liwe la wote.
 
Wajitokeze kama kuna waanga na waombe fidia kwa madhira waliyoyapata kama hakuna basi ni stori za kijiweni.Dunia ya sasa sio kama ya zamani
 
Back
Top Bottom