Ilikuwaje mpaka ACP Abdallah Zombe akanusurika kufungwa?

Teko Modise

JF-Expert Member
Joined
May 20, 2017
Posts
2,331
Reaction score
7,733
Ushahidi uko wazi kabisa juu ya order alizotoa kwenye mauaji yale ya wafanyabiashara ikawaje yeye hakukutwa na hatia? Inanikumbusha picha moja ya kihindi inaitwa "Andha Kanoon" maana yake "Sheria Kipofu"

Wakuu ilikuwaje mpk Zombe akanusurika kufungwa? Karibuni
 
Jaji wa kesi hii alikuwa ndiyo kwanza kateuliwa kutokea kuwa wakili binafsi.

Hapa fikiria wakili msomi Kibatala ateuliwe kuwa jaji na kesi ni dhidi ya mshitakiwa yeyote.

Majaji wa namna hii kuegemea zaidi kwenye yote yaliyo na afueni zozote kwa mshitakiwa.
 
Sio kweli...hakukua na ushahidi wa hizo order uliotolewa mahakamani!
 
Jaji wa kesi hii alikuwa ndiyo kwanza kateuliwa kutokea kuwa wakili binafsi.

Hapa fikiria wakili msomi Kibatala ateuliwe kuwa jaji na kesi ni dhidi ya mshitakiwa yeyote.

Majaji wa namna hii kuegemea zaidi kwenye yote yaliyo na afueni zozote kwa mshitakiwa.
Unamaanisha jaji wa mahakama gani sasa maana kesi ilisikilizwa mahakama kuu na ya rufaa.
 
Jaji alisema zombe siye aliyefyatua risasi kuwaua wale watu.
Hata hivyo Coplo saad ambaye ndiye aliyefyatua risasi hakuweza kukamatwa na haijulikani yupo wapi mpaka leo

Kuna kamanda wa polisi amehukumiwa kunyongwa sababu alikuwepo eneo la tukio na ndie alietoa amri. Zombe yeye hakuwepo eneo la tukio na wala hakuna ushahidi uliomuonesha kama zombe alitoa amri watu hao wauwawe maana hata hao watu wakati wanakamatwa hakuwaona na hata wakati wanapigwa risasi hakuwepo pia
 
Unamaanisha jaji wa mahakama gani sasa maana kesi ilisikilizwa mahakama kuu na ya rufaa.

Nina maana kutokea mahakama kuu.

Kumbuka hukumu inaweza kusilibwa kiasi kuwa hata ukate rufaa wapi nafasi ya kuyabadili matokeo inakuwa haipo.

Ikumbukwe pia udhaifu kutokea upande wa mashtaka nao ulichangia ambapo badala ya framing ya kesi na kuupangilia ushahidi dhidi ya watuhumiwa vilivyo, hisia zaidi za uovu wao ziliendekezwa.

Ninakazia mahakama ya rufaa haiangalii ushahidi mpya zaidi tu ya yale yaliyowasilishwa kutokea mahakama ya chini dhidi ya hukumu iliyotolewa.

Hapa ndipo ulipo mchezo wenyewe. Kwa kesi yoyote (hasa huku makwetu) hukumu inaweza kuwa yoyote. Hii ni kama vile vile ambavyo misahafu ile ile inavyoweza kuhalalisha lolote.
 
Pitia series kwenye gazeti la mwananchi imeandikwa vizuri sana. Kiufupi ni ujinga na uzembe wa serikali. Zombe alishitakiwa kwa mauaji, na hakuua wa kuwepo eneo la tukio. Hata kama ni kweli alitoa amri, je sheria zetu zinasema ukituma au kutoa amri ya kuua kinyume na sheria ni kosa la kuua? Ndio maana akatoboa kirahisi, halafu Jamhuri baada ya kuona imechemka, ikamuomba Jaji ampate na hatia ya kupanga mauaji. Wakaambia hiyo sio kesi iliyopo hapa.

Bageni aliyekuwepo eneo la tukio na ndie alikuwa most senior officer yeye alihukumiwa kunyongwa baada ya serikali kukata rufaa.

Wanasheria wa serikali uzembe hawajaanza na kesi ya Mbowe, ndio jadi yao.
 
Ushahidi uko wazi kabisa juu ya order alizotoa kwenye mauaji yale ya wafanyabiashara ikawaje yeye hakukutwa na hatia? Inanikumbusha picha moja ya kihindi inaitwa "Andha Kanoon" maana yake "Sheria Kipofu"

Wakuu ilikuwaje mpk Zombe akanusurika kufungwa? Karibuni
Zombe hakuuwa unamshtaki vipi kwa kesi ya mauwaji?

Zombe ilipaswa ashtakiwe kwa kesi ya kula njama, kwenye murder case awe shahidi tu.

Ndio haya ya ugaidi wa shilling laki sita, hakuna Jaji anaweza kufanya ujinga huu labda wale majaji aliowatajaga Lisu.
 
Ushahidi uko wazi kabisa juu ya order alizotoa kwenye mauaji yale ya wafanyabiashara ikawaje yeye hakukutwa na hatia? Inanikumbusha picha moja ya kihindi inaitwa "Andha Kanoon" maana yake "Sheria Kipofu"

Wakuu ilikuwaje mpk Zombe akanusurika kufungwa? Karibuni
Ya Zombe yashapita kwanini mnapenda kufukuwa Makabuli mnatafuta nini kwa Mzee Zombe?
 
Ula uchawi upo nyieee, kuna askari nae alikuwa ni mtuhumiwa kwenye kesi hiyo, zamu yake ya kutoa ushahidi ilipowasili akaanza kuumwa tena akivimba kichwa, hivyo kesi ikawa inapigwa danadana mpaka jamaa akafa!

Wengi wanasema kama jamaa angeweza kupanda kizimbani na kutoa ushahidi Zombe angekuwa pabaya leo hii!
 
Jaji wa kesi hii alikuwa ndiyo kwanza kateuliwa kutokea kuwa wakili binafsi.

Hapa fikiria wakili msomi Kibatala ateuliwe kuwa jaji na kesi ni dhidi ya mshitakiwa yeyote.

Majaji wa namna hii kuegemea zaidi kwenye yote yaliyo na afueni zozote kwa mshitakiwa.
Hoja hiyo sio ya kweli,Jaji alikuwa Salum Masati nakumbuka huyo Jaji hadi anasikiliza lile shauri tayari alishakuwa kwenye Ujaji kwa muda kidogo.
 
Ula uchawi upo nyieee, kuna askari nae alikuwa ni mtuhumiwa kwenye kesi hiyo, zamu yake ya kutoa ushahidi ilipowasili akaanza kuumwa tena akivimba kichwa, hivyo kesi ikawa inapigwa danadana mpaka jamaa akafa!

Wengi wanasema kama jamaa angeweza kupanda kizimbani na kutoa ushahidi Zombe angekuwa pabaya leo hii!
Anaitwa RASHID LEMA.
alitoka ukurutu kisha akafa
 
Back
Top Bottom