Ilikuwaje Nyerere akamshinda Sykes?

Mosi, watu wa Dar mnaamini sana kuzaliwa na kukulia Dar ni sifa ya ziada.
Pili, wao ndio walimtaka kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo usomi.

Tatu, ukumbuke Nyerere alitokea familia ya kichifu.
 
Hili swala la waislam kupigania uhuru alioandika sheikh Mohd Said ingalikuwa uongo kanisa katoliki hasa Pengo angalikuwa ashaomba msaada wa kifedha vatikan ili wajibu hoja. lkn kwa sababu limekuwa gumu kwao ndio maana wapo kimya
Toka lini kanisa linajibizana na Waislamu?
 
Huyu ndio kiboko ya wagalatia, wanaufyata akitajwa tu, wanaishia kumtusi na kejeli wakishindwa hoja, wa kubishana nae hajazaliwa
Mungu amuhifadhi na ampe umri twawil wenye manufaa na watanzania
Ndugu huu ni ushauri pengine ni nje ya mada. Mgalatia mchukulie kama ndugu yako. Safari yetu ni moja tunamtafuta Mungu, tufike kwake tukiwa wakamilifu. Labda tumetofautiana usafiri tunaotumia lakini dhamira yetu ni moja.

Tunaamini katika Mungu, basi mtangulize yeye kwanza kwenye kila jambo. Dini isiwe sababu ya kumuona John ni kafiri, Jesca ni wa motoni. Kama dini fulani ingekua ndio tiketi ya kuiona pepo bila kuangalia uhalali wa matendo basi maisha yetu ya kiimani yangekuwa mepesi sana.

Sio lazima unijibu hili swali ila fanya hivi, Jirani yako hana dini na hajawahi kumkufuru Mungu kwa namna yoyote ile amekuwa akiishi katika matendo ya kupendeza, kusaidia maskini, haibi, hadhulumu, hasemi uongo nk..lakini ni hana dini.

Wewe unaamini dini yako ni ya haki na kweli unaswali swala tano sawa, lakini wewe ni mwizi, jambazi, mzinzi, unadhulumu yatima na Wajane nk lakini una dini na unaswali fresh tu.

Narudia tena sio lazima unijibu ila jiulize ni yupi ana nafasi mbele za Mungu? Kwamba atamchoma moto Jirani kwa kuwa hakuwa wa dini fulani na atakuchagua wewe kwa kuwa wa dini fulani?

Mwenyezi Mungu ameweka kitu ndani yetu, uwe una dini usiwe na dini, uwe unaamini Mungu uwe haumini ila unapotenda jambo jema unajua na unapotenda jambo baya unajua. Labda ndio tunda la mti wa mema na mabaya.

Unaweza kukutana na comments zangu kwenye mijadala mbalimbali hapa Jf hasa ya kidini ila sijawahi kumchukia mtu asiye wa imani yangu kwa namna yoyote ile. Nikimchukia Muislamu ni sawa na nimemchukia rafiki yangu wa toka utotoni, ni sawa nimewachukia Mama zangu wadogo, Dada zangu na wadogo zangu.

Nikiona kuna mtu anatumia dini kuhubiri chuki, anatumia dini kugawa watu huwa lazima nimjibu, japo sipendagi muendelezo naamini jibu langu moja au swali langu linatosha umeshindwa kubadilika basi Mungu awe pamoja nasi.

Leo unamuita Mgalatia, Kesho kafiri, kesho wanaajiri wao tu, wiki ijayo serikali inawapendelea yanaanza machafuko.
Mungu wetu ni wa wote, tujitahidi kupendana. Kukinzana mawazo kupotu lakini kusizae chuki. Kama wote wote tunatoa damu nyekundu, haijalishi rangi zetu, dini zetu. Basi sisi ni wa baba mmoja.
 
Hata wahindi, na watu wa mataifa mengine pia
 
Somo: Wazee waliopigania uhuru hawakuwa na udini, ukabila wala ushamba mamboleo wa huyu wa kijijini huyu wa mjini bali walikuwa wazalendo kuchagua kiongozi wa nchi. Nyerere kijana msomi alikuwa na uelewa mkubwa. 🙏🙏🙏
Nyerere ndiye aliyeanzisha udini. Alikiri mwenyewe.
 
Papaya,
1953 Abdul Sykes alikuwa amepata nafasi ya kuingia Princeton University, New Jersey.

Yeye alikuwa akasome Makerere lakini Waingereza wakamtia KAR na kumpeleka Burma.

Lakini hakwenda Princeton.
Abdul Sykes alikuwa A student.

Tujifunze historia za hawa wazalendo kwanza ndipo tujadili.
 
Mohammed Said nini maana ya haya maneno "Aliporudi Dar es Salaam Abdul alifanya kama walivyokubaliana Nansio na Nyerere akapita uchaguzi ule lakini kwa kura chache sana."

Uchaguzi ulifanyika au hakufanyika, Nani aliyeshinda.
 
Ikulu yenyewe ilikuwa chuo cha Waislam, Mjerumani akaifanya ikulu.
 
1953 kwenda Burma kufanya nini , kupingana pekee yake , vita ya pili ya Dunia 1944. Na ya Kwanza kabla ya hapo. Sasa hii ya 1953 ilikuwa ni ya nini
 
Katika Uislam hakuna somo lisilofundishwa.

Masomo yote, unayoyajuwa na usiyoyajuwa yameanzia Madrassa.
Madrasa ni ya watoto wadogo. Niko nao next door and some families are my close friends. Hakuna kitu kama hicho ulichokisema. Nina katoto ka shemeji zangu 5 yrs kanasoma madrasa, naona anachofundishwa na vibao vya kizamani vya kuandikia , ndio madaftari.
Kuna jirani a friend of mine anasema kisiri siri kuwa mwanangu mimi haendi huko hakuna cha maana kwake katika ulimwengu wa sasa. Wako shule za kawaida English medium!
 
Elimu mtu wangu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…