Ilikuwaje Nyerere akamshinda Sykes?

Ilikuwaje Nyerere akamshinda Sykes?

Kulingana na mahojiano ya Tundu Lissu na mtangazaji wa ITV , Lissu alidai mara ya Mwisho CCM kufanya uchaguzi wa Mwenyekiti kwa ushindani ilikuwa mwaka 1954 kati ya Julius Nyerere na Abdulwahid Sykes. Ambapo Nyerere alimbwaga Abdulwahid Sykes. Uchaguzi huo ulifanyika kwenye ukumbi wa Anatoglou.

Swali la msingi ilikuwa ni kwamba ilikuwaje Nyerere amshinde Sykes ambaye alikuwa ni mtoto wa hapa Dar na baba yake alikuwa kiongozi wa TAA hapo kabla. Yani Nyerere kutoka Musoma aliwezaje kuwashawishi wajumbe wamchague yeye wamuache Sykes wa Dar.

Tusaidiane mbinu alizotumia Nyerere kushinda uchaguzi huo maana haikuwa rahisi.
Jibu ni fupi tu, Hapakuwa na kubebana kama sasa hivi, uwezo wa mhusika ndio uliongea.
 
Hili ni swali zuri kwa FaizaFoxy na Mwenzake Mohamed Said wanaopenda kudanganya kuhusu Uislam na Uhuru wa Tanganyika kwa kuangaza Kariakoo as if Kariakoo ndiyo Tanganyika

Wamekuwa wanamdanganya Sana watu. Wameitengeza picha ya kwamba Nyerere aliachiwa tu, kumbe walifanya uchaguzi na kila mgombea alipewa muda wa kujieleza mbele ya wajumbe ndani ya ukumbi wa Anatoglou Ilala
 
J K Nyerere alikuwa msomi wa kiukweli akiwa ni mhitimu wa Edinburgh (Master of Arts) huku akiwa mwalimu wa Pugu Sec. Wakati Abdulwahid Sykes alikuwa msimamizi wa madalali wa sokoni na elimu ya madrasa. Sasa angemshindaje Nyerere?? Sawa kutegemea Singida United iwafunge Real Madrid

haaaaaaaaa haaaaaaaaa! Mkuu pamoja na kuchekesha ila umeongea ukweli wa wazi kabisa.
 
Kulingana na mahojiano ya Tundu Lissu na mtangazaji wa ITV , Lissu alidai mara ya Mwisho CCM kufanya uchaguzi wa Mwenyekiti kwa ushindani ilikuwa mwaka 1954 kati ya Julius Nyerere na Abdulwahid Sykes. Ambapo Nyerere alimbwaga Abdulwahid Sykes. Uchaguzi huo ulifanyika kwenye ukumbi wa Anatoglou.

Swali la msingi ilikuwa ni kwamba ilikuwaje Nyerere amshinde Sykes ambaye alikuwa ni mtoto wa hapa Dar na baba yake alikuwa kiongozi wa TAA hapo kabla. Yani Nyerere kutoka Musoma aliwezaje kuwashawishi wajumbe wamchague yeye wamuache Sykes wa Dar.

Tusaidiane mbinu alizotumia Nyerere kushinda uchaguzi huo maana haikuwa rahisi.
Mzee Said Mohamed mtaalam wa Historia ya Mitaa ya Tandamti, Kongo na Msimbazi atatupa majibu soon!
 
Kusadikika
Huwa sikisii:
1724733122750.png

Hapo nyerere kawachwa kwenye mataa, Malkia anaongea na mtawala wa kweli, Joan Wicken, alipokuja Dar.
 
Binafsi niligunduwa baadae kumbe aliyetuzidi wote ujanja alikuwa Muingereza, hata Ikulu Waingereza walimweka Nyerere kama kanyaboya tu.
. Mtawala wa Ikulu alikuwa mwanamke wa Kiingereza aitwae Joan Wicken.

Unalijuwa hilo?

Unapotosha Sana. Unataka kuniambia waingereza ndio walimchagua Nyerere pale Anatoglou?. Kuhusu Wickens yule alikuwa Katibu Mukhtasi na Wala hakuwa na mamlaka yoyote. Kumbuka baada tu ya kupata uhuru wasomi walikuwa wachache hivyo tulikopa waingereza watusaidie.
 
Back
Top Bottom