econonist
JF-Expert Member
- Jul 11, 2015
- 20,189
- 29,663
- Thread starter
- #61
Economist,
Nyerere hakufanya chochote.
Katika mazungumzo yaliyofanyika nyumbani kwa Hamza Mwapachu Nansio Ukerewe kati ya Mwapachu Abdul Sykes na Ali Mwinyi Tambwe walikubaliana kuwa Nyerere achaguliwe kuwa President na mwaka unaofuatia 1954 TANU iundwe kwa nia ya kudai uhuru na Julius Nyerere aongoze harakati hizo.
Kwa nini walikwenda kwa Hamza Mwapachu?
Sababu yeye ndiye alikuwa kiongozi wa harakati hizi za kuwaleta vijana wasomi ndani ya TAA kwa nia ya kukibadili chama kiwe chama cha siasa kamili wadai uhuru.
Hamza Mwapachu akamwambia Abdul Sykes amsaidie Nyerere achaguliwe ili mkakati huu wao ufanikiwe.
Aliporudi Dar es Salaam Abdul alifanya kama walivyokubaliana Nansio na Nyerere akapita uchaguzi ule lakini kwa kura chache sana.
Angalia video:
View: https://youtu.be/QKV-whFBnWY?si=ZtnHJjhUW1QvNWbB
Ilikuwaje huyo Sykes akaukubali kugombea na Nyerere?.