Ilikuwaje Nyerere akamshinda Sykes?

Hilo la Arnatoglo wewe umelisoma wapi?

Hilo la Wicken mimi nakupa kitu kipya kabisa.

Ulishamuona katibu mukhtasi gani mwengine Tanzania hii au duniani akikutana na head of states, hususan Malkia?
 
Economist,
Nyerere hakufanya chochote.

Katika mazungumzo yaliyofanyika nyumbani kwa Hamza Mwapachu Nansio Ukerewe kati ya Mwapachu Abdul Sykes na Ali Mwinyi Tambwe walikubaliana kuwa Nyerere achaguliwe kuwa President na mwaka unaofuatia 1954 TANU iundwe kwa nia ya kudai uhuru na Julius Nyerere aongoze harakati hizo.

Kwa nini walikwenda kwa Hamza Mwapachu?

Sababu yeye ndiye alikuwa kiongozi wa harakati hizi za kuwaleta vijana wasomi ndani ya TAA kwa nia ya kukibadili chama kiwe chama cha siasa kamili wadai uhuru.

Hamza Mwapachu akamwambia Abdul Sykes amsaidie Nyerere achaguliwe ili mkakati huu wao ufanikiwe.

Aliporudi Dar es Salaam Abdul alifanya kama walivyokubaliana Nansio na Nyerere akapita uchaguzi ule lakini kwa kura chache sana.

Angalia video:


View: https://youtu.be/QKV-whFBnWY?si=ZtnHJjhUW1QvNWbB
 
Si wewe weka ukweli kuupanguwa upotoshaji wake. KInakushinda nini?

Umekazana "anapotosha" wakati hicho unachokiandika umekisoma kwake. Au unacho mbadala chenye ukweli?
Majanga.

Hapana Mimi sichukui chochote Kwa huyo Mzee. Jana historia imewekwa wazi.
 
Kama kasema hivyo, kadanganya, CCM haikuwepo wala haikujulikana kama itakuwepo mwaka huo.
 
Picha inaongea maneno 1,000 hiyo.

Ulishamuona katibu mukhtasi yupi duniani akakutana na malkia? Hata wa kwao Uingereza hutomuona. Protokali haziruhusu, itakuwa dharau kwa Malkia.

Lakini hapo? Unajionea mwenyewe.

Hiyo pîcha imepigwa Mwaka gàni?
Ulikuwa ni Muda WA Kazi?

Kuongea Jambo Kwa kujitungia NI uongo.
Uislam umekufundisha kujitungia mambo?
 
Mwaka 1954 ulitaka watu wabebe maboksi ya kura hadi Tandahimba mkuu?
Hapo Dar si kulikuwa na mchanganyiko wa wakazi kutoka sehemu mbalimbali, Nyerere mwenyewe si ni mzaliwa wa Mara.
 
Hilo la Arnatoglo wewe umelisoma wapi?

Hilo la Wicken mimi nakupa kitu kipya kabisa.

Ulishamuona katibu mukhtasi gani mwengine Tanzania hii au duniani akikutana na head of states, hususan Malkia?

Wewe unakataa kwamba Nyerere hakuchaguliwa , lakini unanilazimisha nikubali kwamba Secretary wake ndio alikuwa Rais wa Nchi. Unafurahisha Sana.
 
Picha inaongea maneno 1,000 hiyo.

Ulishamuona katibu mukhtasi yupi duniani akakutana na malkia? Hata wa kwao Uingereza hutomuona. Protokali haziruhusu, itakuwa dharau kwa Malkia.

Lakini hapo? Unajionea mwenyewe.

Hapo walikuwa kwenye tafrija wanaongelea. Sio kwamba malkia alifungwa official visit kuja kuonana na hiyo secretary wa Nyerere.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…