Ilikuwaje watu wakaamini kwamba Tanzania inaweza kuendelea bila kushirikiana na dunia?

Mkuu hata usiponiheshimu mimi sina shida yoyote ile, kwasababu mimi napenda kusimamia ukweli siku zote.
Haya turudi kwa Raisi Donald Trump, hivi unafahamu ni madhara gani ya muda mrefu ambayo ameyaleta kwa Marekani na dunia nzima ??? Sasa iko hivi:

Sehemu kubwa za kimkakati kwa taifa la Marekani ni hizi zifuatazo:
-The Western Hemisphere,
-Europe,
-The Persian Gulf,
-The Middle-East,
-The Pacific,

Afrika haijawahi kuwa ni sehemu ya kimkakati ya nchi ya Marekani japo ina umuhimu sana kwake. Marekani iliyojengwa na Franklin Delano Roosevelt na Harry S Truman ni nchi ambayo imekuwa na nguvu duniani kwasababu ya ushawishi iliyofanikiwa kuujenga kwenye hayo maeneo.

Nakuachia maswali sasa:
  • Kwanini leo hii Ursula Von Deleyen anapendekeza EU wake na jeshi lao ilhali wako ndani ya NATO ???
  • Kwanini mataifa kama UCHINA na URUSI yanafikiri kuacha kutumia dola katika biashara yao ???
  • Kwanini siasa za Mashariki ya kati zimekuwa hatari sana kuliko kipindi chochote kile ???

Majibu yake sasa ndiyo, The Trump Effect......
 
Tanzania ilipoteza dira baada ya Nyerere kufariki.

Awamu ya tatu na ya nne Tanzania lost its soul ikabakiza historia ya marehemu.

2015 hivi aliyeruhusu Magufuli awe rais alikuwa anawaza nini ?
Nyerere ndie aliyeanza kupoteza dira kwa kuacha mfumo sahihi wa kuleta maendeleo ulioasisiwa na wakoloni.Angechukua mazuri ya wakoloni akaenda nayo
 
Nyerere ndie aliyeanza kupoteza dira kwa kuacha mfumo sahihi wa kuleta maendeleo ulioasisiwa na wakoloni.Angechukua mazuri ya wakoloni akaenda nayo
Nafikiri hoja yako iko kwenye mada tofauti kidogo.
 
Inasikitisha kuwa watu kama mtoa uzi huu wapo wengi tu!! Akili yao haifanyi kazi!! Wanaamini kuwa bila msaada wa wengine hatuwezi chochote! watu waliofilisika kichwani hadi leo wanaabudu ubeberu!!! Pole yao!
Umewaza kijinga msome tena jamaa utamulewa
 
Naamini Tanzania inaweza kuendelea bila kutegemea misaada bali ikabaki tu kuheshimiana na kushirikiana kwenye maendeleo...

Wakubwa wa dunia wanaamini kwenye umafia kwa kuendelea kufanya wengine masikini kwa kutumia baadhibya tools zai kila mahala..Wakubwa wadunia wakigundua una mtazamo tofauti wakuwatoa watu kwenye utumwa wa kiuchumi basi hutumia tools zao na vibaraka waliopandikizwa kila mahala kukumaliza..... WaAfrica tujaribu kuwa real na Uafrica wetu tusishupaze shingo na kubabaika sana na hawa pua ndefu....
 
Dah! Wewe kweli "AKILI KUBWA"!
 
Malcom Lumumba naamini wewe ni mtaalamu mzuri wa diplomasia

Na mwana diplomasia kama wewe ni lazima utakua unawafahamu wajuvi wenzako wa diplomasia ndani ya nchi hii

Swali langu...

Tuambieni watanzania, utaalamu wenu wa diplomasia ulitusaidiaje kama nchi kujikomboa na janga la umasikini?(before&after magu, maana kwa mujibu wako huyu ni sufuri kwenye diplomacy)
 
Sasa wewe utakuwa first world lini? Au umelizika kuwa third world?
 
Kwa watawala gani hawa wanaobambikia kesi wenzao kukwepa mijadala
 
Nakubaliana kabisa na wewe, lazima tulinde rasilimali zetu kwa WIVU MKUBWA, lakini siyo kutumia ile njia ambayo kipenzi chenu alikuwa anaitumia. Amevuruga mambo na itifikati katika kiwango kikubwa sana,.....
Kuna njia ipi mbadala ambazo nchi za Afrika zitatumia kulinda masilahi yake? Huoni aliyoyapa Gadaffi? Labda utasaidie hata kidogo, nchi kama Tanzania itawezaje kulinda rasilimali zake kwa njia ya urafiki na mabeberu?
 
Nchi hii watu wenye akili hawapewi nafasi sababu hawana muda wakusifu ujinga
 
Nchi hii watu wenye akili hawapewi nafasi sababu hawana muda wakusifu ujinga
Yawezekana hujamwelewa Lumumba, yeye amejikita zaidi katika awamu ya tano...

Ndio maana naamini kabla na baada ya awamu ya tano, nyinyi wataalamu mlipewa nafasi na makafanya kazi

Swali langu, kabla na baada ya Magufuli mmeisaidiaje Tanzania katika vipengele alivyotaja Malcom?

Asante.
 
Ukitaja kujua tuliongukia mikono mwa matapeli washamba, msikilize Kabudi akielezea mirabaha kwenye madini, sijui tutapata 50/ 50 laki wakati huo huo tuna shares 16%. Halafu huo utapeli hawataki mtu ahoji bali ni ww kusifia tu, eti nchi mkononi kwa mzalendo! Ila Mungu amtuepusha na yule kiongozi muovu, acheni Mungu aitwe Mungu.
 
Je USA anaheshimu diplomasia yz kimataifa? Nieleze kuhusu ushiriki wake katika mahakama ya ICC.
 
Umeongea vizuri umemalza ayo mengine ndio ayo ayo ambayo chanzo cha sahihi kuwa apa akili,sasa mtu anakuulza swali et tanzania masikini unazan kutakua na maelewano apo ,akili za binadam zimetofautiana sana ila naona kwa Africa utofaut wetu na mkubwa zaidi ikiwemo tz umo umo ndio tunapata viongozi matokeo yake ndio aya
 

Watu hawakuwa wanaamini ule utapeli, bali ilikuwa ni shuruti. Na ilikuwa ukionyesha kwenda kinyume na ule utapeli unatekwa, kuuwawa au kubambikiwa kesi. Yaani tulipata kiongozi muovu, hisia zake akawa anatulazimisha tuziamini!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…