Image ya saini ya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere

Image ya saini ya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere

Hivi nini maana ya sahihi? Mimi nikiangalia naona ni majina mawili, la kwanza na la mwisho lile la katikati kaliandika kwa ufupi yaani kwa kutumia herufi ya kwanza ya jina Kambarage hivyo ukiangalia inasomeka "Julius K. Nyerere" Sasa majina hayo ndiyo sahihi? Kwakuwa tarehe za kuandikwa ni tofauti huenda tofauti ndogo zisikosekane. Katika hilo mimi nafikiri la muhimu ni kuangalia content kama ni valid badala ya kudeal na sahihi tu

Mambo ya kisheria hayaendi hivyo. Maana ya kuwekwa sahihi ni kuwa alieweka sahihi anakubali yaliyoandikwa. Sasa kama huna uhakika wa sahihi uhakika wa kilichoandikwa utapatikana vipi?

Kuhusu muda na kubadilika maandishi nakubaliana nawe lakini basi na iletwe document nyengine aliyoisaini kipindi hicho nyuma zilinganishwe!
 
saini-564x272.jpg
zote saini zilizopo hapo Bingeni ni Fake km zilisaini Document yeyote ya Muungano )fuatilia Taarifa za Habari za Kituo cha ITV LEO 02/04/2014

Kamati za Bunge la Katiba leo zimecharuka na hata Sendeka kajiumauma
Waandishi wamembana Nahodha ambye ni Mwenyekiti wa Kamati mojawapo kuhusu hizo saini na kujiumauma kwa Pius Msekwa kuwa hazikumbuki vizuri kwa hiyo hizo Hati za Muungano sizo zenyewe kabisa kwani Kituo cha ITV kimeonesha kituko chote kizima.
FUNNY enough Nahodha kawauliza Waandishi waliomkabili na maswali

km Kiongozi mkubwa wa Serukali na DINI akipayuka hivyo ujue kabanwa na ukweli anaujua

Ulishawahi kumuona kiongozi wa Tanzania akajali dini? Huoni ni udhaifu wa imani kumuhusisha mungu na upuuzi wao! Yeye Nahodha anapopiga makelele ya Mapinduzi daima aliyaona hata akayakubali?
 
Hata wewe mleta uzi, ukichunguza vizuri sahihi zako utakuta zina slight difference, sahihi sio nakala ( Copy) kiasi cha kulazimisha kuwa zipo sawa kila kitu. Hata ukichukua sahihi za Mwl kwenye masuala mbalimbali ambayo hayatiliwi shaka ukichunguza unaweza kukuta slight diffrence kama hizo. Cha msingi cha kujadili ni hizo Contents za mkataba wenyewe badala ya kuleta ubishi kwa mambo ambayo ku prove itachukua muda kama vile ubishi wa kikanuni kwenye bunge.
Zijadiliwe contents zilizosainiwa na nani ikiwa sahihi si yake? Uhalali na maana ya kujadiliwa unakuja kwa kuzingatia maamuzi ya wahusika wawili tu Nyerere na Karume!
 
hahahahah! ama kweli! hivi ni kwa nini mambo haya yanatokea? je ni kweli hizo ndo sahihi za Mwalimu.
 
Zote zake hizo.

Nilibishana na wafanyakazi wa NBC Morogoro mwezi uliopita nilipoenda kuchukua pesa dirishani wakasema sahihi ipo tofauti na ya kwenye database yao,nikawaambia hiyo ilikuwa mwaka 2007 leo 2014 mnatarajia nini.??!!
Chochote kinawezekana,sahihi inaweza kubadilika muda wowote ndo maana watu makini hutumia Finger print hata baada ya kupiga sahihi kwenye nyaraka muhimu.
 
Zijadiliwe contents zilizosainiwa na nani ikiwa sahihi si yake? Uhalali na maana ya kujadiliwa unakuja kwa kuzingatia maamuzi ya wahusika wawili tu Nyerere na Karume!

Huna uwezo wa kutambua kitu kilichoghushiwa kama hujawahi kuona kitu halisi kinafananaje.

Suala la Sahihi za Mwl kupishana hata kwenye Hati mbalimbali ambazo Mwl alisaini ukichunguza utakuta tofauti kidogo. Chukua Peni na Karatasi then weka saini zisizopungua Tano halafu zichunguze kwa umakini utakuta kuna Slight difference na Ndio maana wataalamu wa saini wakifanya uchunguzi wa Sahihi hawa base kwenye Mikunjo ya Herufi bali Mgandamizo wa Mtu anae saini

Watu wa Bank mara nyingi sana huingia kwenye Mizozo na Wateja kwa kulazimisha Sahihi za wateja zifanane na zilizopo kwenye Data base yao kwa 100% kitu ambacho ni kigumu hata wao wenyewe wakiambiwa warudie.
 
Huna uwezo wa kutambua kitu kilichoghushiwa kama hujawahi kuona kitu halisi kinafananaje.

Suala la Sahihi za Mwl kupishana hata kwenye Hati mbalimbali ambazo Mwl alisaini ukichunguza utakuta tofauti kidogo. Chukua Peni na Karatasi then weka saini zisizopungua Tano halafu zichunguze kwa umakini utakuta kuna Slight difference na Ndio maana wataalamu wa saini wakifanya uchunguzi wa Sahihi hawa base kwenye Mikunjo ya Herufi bali Mgandamizo wa Mtu anae saini

Ndugu yangu usitake kulifanya swala la Nyerere kuwa tofauti na hali nyengine. Ni mara ngapi wameeitwa wataalamu wa maandishi kuthibitisha sahihi kwa hivyo haiwezi kuwa tofauti na kesi hii. Iwapo kuna utata basi ufanyike uchunguzi au wewe kama wewe huamini kuwa watu hughushi sahihi?
 
saini-564x272.jpg
Ipi ni saini yake ya kweli ???

Hata ukiangalia kwenye herufi J, u, na l kunatofauti ya kuona kwa macho bila kutegemea microscopic device. Sasa huyo aliyefoji hiyo dokumaa anachukuliwa hatua gani? Hiyo dokumaa si mali ya serikali?
 
Hata ukiangalia kwenye herufi J, u, na l kunatofauti ya kuona kwa macho bila kutegemea microscopic device. Sasa huyo aliyefoji hiyo dokumaa anachukuliwa hatua gani? Hiyo dokumaa si mali ya serikali?

Inasikitisha kuona tunajadili upuuzi... sahh zinabadilika kutegemea na nyakati pamoja na mikao.
Ukiandika umekaa itatua tofaut na ya kusimama.

Sahih ya mwaka jana kuna uwezekano isiwe sawa na ya mwaka huu.
Huo mkasa umenikuta bank ya exim juzi bank teller anazngua kunipa hela kisa sahihi zimetofautiana.

Mkono si sawa na photocopy machine kiasi kwamba utende sawa kila wakati.

Msiwe mnajitoa ufahamu kutetea ujinga usiokuwa na mashiko wala tija kwa taifa.
Nyie ndo mnachangia hii nchi ionekane imejaza wapumbavu na wajinga lundo.
 
saini-564x272.jpg
Ipi ni saini yake ya kweli ???

Hii yote ni uovu wa ma-ccm tu ktk kulazimishia kutawala umma wa tanganyika na zbar kwa kulazimisha chini ya muungano mfu wa magumashi...watashindwa siku sii nyingi zijazo...
Sala ya kuombea waovu hawa ma-Ccm yanayoipinga kauli ya umma wa watanganyika...naomba tusali wote.
.Eeee Muumba wetu tuletee Tanganyika yetu haraka...waangamize waovu hawa na wote wanaoificha nchi yako uliyowaandalia watoto wako na wajukuu wa Tanganyika...watumbukize waovu hawa ktk shimo la Giza ...wasirejee nyuma kujitambua kamwe...wavuruge kama ulivyowavuruga waovu wale ktk mnara wa babel...hadi taifa lako jipya la Tanganyika lijikomboe na liwe huru daima na milelee..amina!...wote tuseme aaaamen...amen!
 
na wewe ni majanga tu kama binamu yako! mbona hujamuelewa kikwete anayeupigania muungano?

Kila Mtanzania ana haki ya kutoa maoni yake, usifikiri kuwa Kikwete ni alien.

Mimi binafsi muungano ukiwepo sawa usipokuwepo ndio kheri, nimeishi kwenye muungano kabla ya huu feki. Muungano ulikuwa ni ule wa asili na asili, kati ya Zanzibar na Tanganyika si huu feki wa Nyerere.
 
Back
Top Bottom