Mshana Jr
Platinum Member
- Aug 19, 2012
- 376,316
- 871,876
Sakata la watu wawili linachukua sura mpya kila uchao..... Na kila anajitokeza kuliongelea ama anazidi kuharibu ama anazidi kukoleza moto.. Na lisipodhibitiwa sasa linaweza kuja kuleta mgawanyiko mkubwa ndani ya imani moja ama madhara makubwa
Sasa kwenye hili.. Inayoumizwa ni imani. Kwakuwa jambo husika lilianzia ndani ya nyumba ya ibada na wahusika wakuu ni viongozi wa dini
Tuhuma ndogo iliyoleta mvurugano wote huu ni tuhuma ya michezo ya kitapeli kama ile ya mitume na manabii feki.. Tuhuma hii inawataja baadhi ya wahadhiri wanatumia utapeli wa kuwachoma mbuzi sindano za sumu ya ya kuanza kisomo cha dua kwa mtu mwenye shida
Basi kisomo kitapigwa pale huku mhitaji akiwa kamshikilia mbuzi akiwa hai mpaka anafia mikononi mwake
Justification ya hili ni kwamba kisomo kilikuwa kikali na vita ilikuwa kubwa mpaka matatizo ya mhusika yametoka na kuhamia kwa mnyama
Hapo hata wewe lazima uamini na kutoboka mfuko!
Sasa hii tuhuma ilitolewa na mhadhiri mwalikwa kwenye nyumba ya ibada inayoongozwa na Kishk na hakutajwa mtu.,, lakini akaibuka mtu anaitwa Ostaz Juma Namusoma na kuanza kumshambulia Kishk na maisha yake binafsi na lundo la kashfa na tuhuma
Sasa Kishk hamjibu Namusoma bali kuna watu wa kada mbalimbali, na wa imani tofauti ndio wanamjibia ama kumtetea
Sasa kila anayesimama na kusema lolote anazidi kuharibu na kukoleza moto huku wakishindwa kabisa kuitenga imani na mambo binafsi
Sasa ni wazi kuna mambo yalikuwa yanaendelea kimyakimya kwa muda mrefu na sasa yamepata upenyo wa kusanuka
Kuna tuhuma za utapeli
Kuna tuhuma za watu binafsi kujinufsisha na misaada toka nje
Kuna tuhuma za uasherati na uzinzi
Kuna tuhuma za unyanyasaji wa kingono
Kuna tuhuma za ushoga nknk
Sasa ni mwendo wa mafaili ya maisha binafsi.. Yamejitokeza makundi mawili yanayosigana kila moja likimtetea mtu wake na kinyume chake
Kwenye hilo sakata matusi, kejeli na kashfa vinatumika sana...
Hivi seriously hawana vyombo vyao vinavyoweza kuwakalisha chini na kuwasuluhisha baada ya kujua kiini na ukweli wote?
View: https://vm.tiktok.com/ZSXNaskVb/ This post is shared via TikTok Lite. Download TikTok Lite to enjoy more posts: TikTok