Imani potofu huchangia sana umaskini

Imani potofu huchangia sana umaskini

Bora ukawa hauna hela Ila usiwe na fixed mindset

Maana nimeona familia Fulani wanamwaga sukari kilo 50 shimoni kisa aliyewapa huo msaada wanahisi ni mtego

Ukiwa masikini wa akili you can't move anywhere
Daah
 
Umetumia njia isiyo sahihi kutoa msaada. Ni vyema baada ya kupata hiyo taarifa kutoka kwa mtoto ungechukua hatua ya kumfuata mzazi na ukamuambia kuhusu nia yako ya kutaka kutoa msaada, kama angekubali ndiyo ungetoa huo msaada.
Basi mwenye makosa mimi
 
Kuna mtoto wa jirani mtaa wa pili kamezoea kila nikipita kakiniona lazima kanipungie,japo hajawai kuniona hanakwahana basi tu ivo kakiona gari kanaikimbilia na kuipungia. Sasa leo nimepita kwa mguu nilivokaona nikakaita, nikamuuliza jina na ufaham wa hapa na pale. Lkn kakaniomba ela kakadai kana njaa hawajala,mama yao kaenda kwenye kibaruani(ni mtoto km miaka minne ivi).
Basi nikamuita mkubwa wake ambae ana umri km miaka 8,9 ivi nikaenda nako dukani nikamuemelea mchele, sukari, mafuta, chumvi, na mahitaji muhimu ya kula. Nikampandisha kwenye boda ninaemfahamu na kunifahamu akampereka nyumbani.
Nashangaa boda huyo ananipigia simu eti kamkuta mamake mtoto karudi yuko nyumbani, amekataa kupokea huo mzigo eti siku izi watu wanachukua nyota za watu kupitia misaada izo, kanamwambia boda arudi navyo. Kwaio ananihisi huo msaada wangu una lengo lake.
Kwa mazingira ya hiyo familia na hivyo huyo mtoto alivyonambia ana njaa ndo ikanishawishi nimsaidie na ni kweli alionekana ana njaa,na niliplan kumfanyia mengine zaidi. Na si kwamba mamake hanifahamu...ananifahamu. Kwanini maskini ukimpa kitu cha bure anahisi ni mtego na ukimwambie akilipie anaona ni gharama au unataka umuibie!? Nimelishangaa sana hili.
Nakubaliaba nawe100%imani potofu ndio umaskini wenyewe.
 
Hakuna Mtu Mwenye akili timamu atachukulia poa Msaada uletwe Kupitia mwanae.Yaani hiyo ni aibu kubwa Sana.Yaani ukiona mwanao anakuja na kitu na amepewa unatamani akitupe.Tukiwa wadogo tukiambatana na mama zetu Kwa Majirani,hata kama tuna njaa,kwa Majirani kuna msosi,mama alikuwa anapiga jicho 1 la kukwambia ukome.Utakula nyumbani.Marehem mama yangu nikiwa sekondari aliwahi niambia,Mwanangu kama Karo na Matumizi ya Shule hutapewa hapa ndani usiende Kwa Mjomba wala Kwa shangazi,vumilia Hadi utumiwe Kwa posta.Baadaye niligundaua hekima iliokuwa ndani Yake.Shule inapoisha hata ambaye hakukusaidia anaanza Kupiga mayowe tumekusomesha.Marehem Mkapa akiwa Rais hakuwa anapenda Mawaziri wawe wakitangatanga Kwa donors Kuomba msaada.Nenda straight Kwa Mkuu wa Kaya saidia.
 
Labda cjui km mimi ndo nimefanya makosa
Iko hivi,maskini anajiongezea umaskini kwa imani yake mbovu,fikiria mganga wa kienyeji,huyu ni mtafutaji kama alivyo chinga,muha,mama ntilie,ama mangi kiduka,na kawaida mganga hufuatwa kama alivyo mangi kiduka,ama muha kahawa,kashata na urembo.
 
Kuna mtoto wa jirani mtaa wa pili kamezoea kila nikipita kakiniona lazima kanipungie, japo hajawai kuniona ana kwa ana basi tu hivyo.

Kakiona gari kanaikimbilia na kuipungia. Sasa leo nimepita kwa mguu nilivokaona nikakaita, nikamuuliza jina na ufaham wa hapa na pale. Lakini kakaniomba hela kakadai kana njaa hawajala, mama yao kaenda kwenye kibaruani (ni mtoto km miaka minne ivi).

Basi nikamuita mkubwa wake ambae ana umri km miaka 8,9 ivi nikaenda nako dukani nikamuemelea mchele, sukari, mafuta, chumvi, na mahitaji muhimu ya kula. Nikampandisha kwenye boda ninaemfahamu na kunifahamu akampereka nyumbani.

Nashangaa boda huyo ananipigia simu eti kamkuta mamake mtoto karudi yuko nyumbani, amekataa kupokea huo mzigo eti siku izi watu wanachukua nyota za watu kupitia misaada izo, kanamwambia boda arudi navyo.

Kwaio ananihisi huo msaada wangu una lengo lake.
Kwa mazingira ya hiyo familia na hivyo huyo mtoto alivyonambia ana njaa ndo ikanishawishi nimsaidie na ni kweli alionekana ana njaa,na niliplan kumfanyia mengine zaidi. Na si kwamba mamake hanifahamu, ananifahamu.

Kwanini maskini ukimpa kitu cha bure anahisi ni mtego na ukimwambie akilipie anaona ni gharama au unataka umuibie!?

Nimelishangaa sana hili.
Ulikuwa sahihi kutaka kuwasaidia. Ungeweza kuwapa watoto hela ya kununua chips wala huyo mama asingestuka. Umekuwa muungwana na kuwapa chakula na zaidi yeye anaamini unataka kuchukua nyota yake! Nyota gani aliyonayo ambayo ikichukuliwa itamuathiri? Hizi imani za kijinga kwa kweli zinatuharibia sana. Utasikia ukimpa mtu anayekuomba pesa mkononi mwake ataondoka na nyota yako! Kwa kweli tuna safari ndefu.

Amandla...
 
Hata wazungu wanafundishwa shule (dont talk to strangers)
yaaani kama wewe mwanaume kesi ya ulawiti inanukia!!!!!
 
"Yatakuja kukupata majanga kwa fadhili zako za kijinga." Abdu Baka, Haifai.
 
Nyota gani aliyonayo kwanza?

Angekuwa ana hiyo nyota asingekuwa masikini!

Hana nyota yoyote ya kuibiwa.
 
Back
Top Bottom