Imani ya Bunge haiwezi kujengwa chini ya Tulia Ackson

Imani ya Bunge haiwezi kujengwa chini ya Tulia Ackson

Ngungenge

JF-Expert Member
Joined
Jun 11, 2016
Posts
2,914
Reaction score
3,386
Kwanza ni mfuasi na kiongozi mwandamizi wa lile kundi alilotoka Ndugai, kundi lililotaka Rais Samia asigombee 2025 na kupanga mikakati ya kumdhoofisha Mh. Rais.

Pili ni mtu asiyeamini katika kazi za Rais Samia, Tulia hakuwahi kuvaa barakoa wala kuhamasisha chanjo hadharani sio ndani wala nje ya bunge.

Tatu Tulia amekuwa aki provoke Mawaziri na wabunge walio nje ya kundi lao wakati wa vikao vya bunge na kuwapa credit wale walio katika kundi lao almaarufu "Sukuma Gang".

Nne Kundi la upinzani kwa Rais Samia bungeni almaarufu kama Sukuma Gang linamtegemea Tulia kama muhimili wao katika kujiimarisha kuelekea 2025 baada ya Ndugai kufurushwa

Tano Tulia hajawahi kujivunia kuwa na Rais Mwanamke. Tangu Samia aingie madarakani tulia is upset hatujui sababu ni msiba ule au ana conflict binafsi na Madam President

Vipimo vya uzani, vinakataa kuwa Tulia anaweza kubahatika kuwa kiongozi kwenye muhimili wa Bunge ama Spika ama kuendelea kuwa Naibu baada ya hili sakata la boss wake ambaye yeye ni mtu wa jikoni kabisa.

Vipimo vinasoma chini ya uzani wa wastani.

Rais Samia 2025
KAZI IENDELEE
 
Kimsingi alishiriki uovu mwingi tu alioufanya boss wake, nimatarajio kuwa kilichotokea ni somo tosha, na hata covid19 atajitenga nao iwapo akamrithi boss wake.
 
Pamoja na kwamba ni bunge la chama kimoja bado hamuaminiani? Kwahiyo humo ndani kuna kambi ya sukuma gang, na Msoga line? Kimsingi watanzania wengi hawana imani na bunge lote, regardless tofauti zenu za kimaslahi za madaraka, na siasa za uchaguzi wa 2025.

Matatizo ya msingi ya wananchi yamewashinda huku mfumuko wa bei ukishika kasi, nyinyi Mmebaki kushindania kambi za kimadaraka!
 
Pamoja na kwamba ni bunge la chama kimoja bado hamuaminiani? Kwahiyo humo ndani kuna kambi ya sukuma gang, na Msoga line? Kimsingi watanzania wengi hawana imani na bunge lote, regardless tofauti zenu za kimaslahi za madaraka, na siasa za uchaguzi wa 2025. Matatizo ya msingi ya wananchi yamewashinda huku mfumuko wa bei ukishika kasi, nyinyi Mmebaki kushindania kambi za kimadaraka!
Watu wanashindana kufanya mema sio maovu.
 
Hili ni tarajio la wengi
Katiba inaruhusu
Wapo watu wenye busara nje ya bunge

Hata akiingia mtu huru humo ndani kuna spika atashia kuchafuka tu. Mwenye nguvu kwenye hilo bunge ni mwenyekiti wa bunge na sio spika. Mwenyekiti wa bunge ni mteule wa rais, na yeye ndio anaamua mijadala iweje ndani ya bunge.

Kwa madaraka haya ya mwenyekiti wa bunge, ni wazi bado bunge litafanya atakacho rais na kambi yake ya kimadaraka.
 
Nasikia ameshaongezewa ulinzi.

Lakini mihimili miwili kuongozwa na....
sidhani kama vidume vitakubali.
 
Kwanza shikamoo mama. Kwa sasa ni kinyume chake.
Kila mtu yupo huru na fikra zake, mema kwako si mema kwangu.

Mema "kwako" ni kutoa sadaka za pombe msibani, mema kwangu ni kutoa pilau msibani. Wapi na wapi?
 
Nasikia amesha ongezewa ulinzi.

Lakini mihimili miwili kuongozwa na ..... Sidhaami kama vidume vitakubali.
Hii ni sababu anakaimu kiti hadi Spika apatikane
Niko ndani kabisa hawezi kuwa Spika mark my words
 
Kila mtu yupo huru na fikra zake, mema kwako si mema kwangu.

Mema "kwako" ni kutoa sadaka za pombe msibani, mema kwangu ni kutoa pilau msibani. Wapi na wapi?
Na wewe unaendaga wapi
Unapotea mwaka mzima
 
Hata akiingia mtu huru humo ndani kuna spika atashia kuchafuka tu. Mwenye nguvu kwenye hilo bunge ni mwenyekiti wa bunge na sio spika. Mwenyekiti wa bunge ni mteule wa rais, na yeye ndio anaamua mijadala iweje ndani ya bunge. Kwa madaraka haya ya mwenyekiti wa bunge, ni wazi bado bunge litafanya atakacho rais na kambi yake ya kimadaraka.
Mtu anayehitahika ni mtu mwenye kujua watanzania wanataka nini na chama kinataka nini.

Hapo toa individuals ao wapo ku implement izo agenda kuu mbili
 
Hata akiingia mtu huru humo ndani kuna spika atashia kuchafuka tu. Mwenye nguvu kwenye hilo bunge ni mwenyekiti wa bunge na sio spika. Mwenyekiti wa bunge ni mteule wa rais, na yeye ndio anaamua mijadala iweje ndani ya bunge. Kwa madaraka haya ya mwenyekiti wa bunge, ni wazi bado bunge litafanya atakacho rais na kambi yake ya kimadaraka.
Ndio upeo wako ulipoishia.

Ndugai alishapeleka deni na tozo zikajadiliwa bungeni na zikapitishwa, kiranga gani kilichomtuma azipeleke hoja hizo kwa wagogo wenzanke? Tunasema "Kiranga komo".

Tunawafahamu mna "fever ya 2025".
 
Back
Top Bottom