Imani yangu juu ya uchawi inanipa mashaka

Imani yangu juu ya uchawi inanipa mashaka

kwisha

JF-Expert Member
Joined
Sep 9, 2021
Posts
1,779
Reaction score
4,982
Katika akili yangu sijawahi kuamini uwepo wa uchawi

Lakini kila nikijaribu kukumbuka baadhi ya matukio mbali mbali ambayo nimewahi kushuudia na kuona katika maisha yangu kunanifanya niwe na maswali mengi juu ya imani hii

Mwaka 2014 kuna brother fulani ambaye tulikuwa tunaishi naye village moja alifanikiwa kupata visa yake ya kwenda Australia baada ya mke wake kumfanyia reunification

Jamaa akafanya sherehe akaalika ndugu zake na marafiki watu waka

Jioni ya siku hiyo jamaa alipotea wakaanza kumtafuta cha ajabu walikuta amejinyonga porini

Mkasa mwingine ambao unanifanyaga mimi niamini ukweli uchawi unaweza ukawepo

Ni kutokana na tukio fulani ambalo lilinikuta mimi na rafiki yangu

Usiku kuna siku mimi na rafiki yangu tulikwenda kumcheki demu fulani usiku wa saa 2 tu tukarudi uko saa 5 usiku sasa kuna njia fulani ambayo tulikuwa tunapita p kila siku njia hiyo ilikuwa na kapori kidogo na pia palikuwa fesi kwasababu kulikuwa na mantaki ya maji

Sasa siku hiyo mimi na rafiki yangu tulikuta na mtu ambaye hatuelewi alikuwa mzimu au mchawi na wakati mwingine na semaga labda ulikuwa uoga wetu

Mtu uyo alikuwa na nywele nyingi na tulikuwa hatumuoni usoni vizuri kwasababu ya nywele zake zilikuwa zimefunika sura kabla ya kufika alipokuwa tulianza kusikia harufu mbaya na nywele zikawa kama zinakokotwa na mwili kusinyaa tulivyomuona tu tukakimbia mbio alikuwa anasimama kwenye mti

Tukio ilo linanipaga maswali mengi sana juu ya imani hii
Inawezekana ikawepo kweli

Na matukio mbali mbali nimesikia ya kutisha kabisa
Inawezekana hii imani ipo kweli au ni uongo
 
Morogoro vijijini huko kuna mganga wanawake wa mjini Daslamu na Unguja wanamtumia sana kupora wanaume wa watu. Ni mganga ambae anaua kabisa jina la adui likipelekwa kwake leo kesho anazikwa.

Ni mganga wa mama we jamaa mmoja maarufu sana kwenye mpira wa bongo rafiki yake na huyo mmama ana miliki kituo cha watoto wa Yatima kwenye wilaya moja jijiji darusalama ni mmama mmoja ana sigda kubwa sana nyeusi. Ushamjua?

Anyways kwa asie amini kuhusu uwepo wa uchawi aende akayakanyage huko.. Yule " mwalimu " alivyo gombana tu jamaa kibarua kimeota nyasi.
 
Uchawi ni Teknolojia beyond current Technology. Inapoishia sayansi ya kina Newton, Sayansi hiyo huanzia.

Ujinga ni kutaka kujaribu kutumia kanuni za kisayansi ya sasa kuelezea Uchawi, HAIWEZEKANI.

UPO uwezekano wa maarifa rasmi tuyaonayo Leo ni 5% tu ya maarifa yote Ulimwenguni.
TUSIJIFUNGIE KWENYE VIBOKSI VIDOGO VYA MAARIFA, TUELEE KATIKA BAHARI KUU.
 
Upo jamaa sister kuna siku kama sa5 usiku tumemaliza kula tunapiga story akaona paka akamfukuza. Yule paka alimrudia sa8 alimrarua rarua shingo kusikia fujo akigombana na paka ndo tukaenda kuangalia tulikuta sister yuko hoi. Usiku unamengi sana
 
Back
Top Bottom