KOCHA TP MAZEMBE: WASITAFUTE SABABU MAPEMA,TUMEJIPANGA KUSHINDA USHINDI WA KISHINDO:
Lubumbashi- Congo
Kocha wa miamba ya soka Barani Afrika amesikia taarifa za kutoka kwa viongozi wa Simba ikihusisha Timu yake kufanya hujuma ya kubadili waamuzi ili waweze kuifunga Simba katika mchezo wao wa marudio unaotarajiwa kupigwa siku ya jumamosi tarehe 13/04/2019.Baada ya kusikia taarifa hizo kocha huyo amezibeza na kusema kuwa ni uoga wa ajabu sana kufanywa na timu iliyofuzu hatua hiyo ngumu ya robo fainali CCL."Nimesikia habari za viongozi wa Simba kuhusisha kitendo cha CAF kubadili waamuzi wa mchezo wetu na hujuma za kupanga matokeo,niwaombe tu hao viongozi wa timu hii dhaifu wasianze kutafuta visingizio na huruma mapema kutoka kwa mashabiki wao,wakae watafakari kuwa sisi sio mara kwanza kucheza michuano hii kwa hatua hii,tumefika mara nyingi na hata kuchukua ubingwa tena tukipambana na timu kubwa sembuse timu ndogo ambayo imekuwa ikitegemea ushirikina ili kushinda mechi zao za nyumbani?" Alipoulizwa kuhusu ugumu wa mechi hiyo itakayoamua timu inayoenda kucheza nusu fainali ya michuano hiyo alisema hana wasi wasi na timu ya Simba kwani ana uhakika wa kushinda mechi hiyo tena kwa idadi kubwa ya magoli ikianzia 8 na kuendelea."Tupo vizuri hatuna hofu yoyote kuhusu mechi hiyo,nilisema toka awali kuwa tutatumia mchezo huu kuzifundisha timu zisizo na sifa ya kucheza hatua hii ngumu ya mashindano haya,timu hii haina sifa ya kufika hatua hii ngumu hivyo tutawafurahisha mashabiki wetu kwa ushindi mnene wa magoli yasiyopungua 8"
Timu hizo zote zina nafasi ya kutinga hatua ya nusu fainali ya michuano hiyo hasa timu ya TP Mazembe ambayo imekuwa ikitumia uwanja wao vizuri kwa kupata matokeo na idadi kubwa ya magoli huku rekodi yao kubwa kwenye mashindano ya mwaka huu ni kuifunga miamba ya soka ya Afrika Club Africain kwa magoli 8-0.Simba ina wakati mgumu katika mchezo huo kwani katika mechi 3 walizocheza ugenini wamepoteza zote kwa idadi kubwa ya magoli kwa kila mechi.