Imani za kishirikina haziwezi fua dafu ukiwa unatoa fungu la kumi, Je hivi ni kwanini?

Imani za kishirikina haziwezi fua dafu ukiwa unatoa fungu la kumi, Je hivi ni kwanini?

Siku nikituma sadaka nataka nione jina linakuja Yesu Kristo Jehovah

Sio bonifas Mwamposa
Siò Musa lymo
 
Nina mengi ila nakupa ushuhuda mdogo sana.
Nilikuwa na madeni ambayo chanzo chake ni uchawi/roho ya chumaulete. Coworkers nao ni washirikina na wamepigana kuniharibu, na taarifa zote napata kupitia ndoto/ulimwengu wa roho ambazo ni za uhalisia, na mwishowe kupata matokeo yake ktk ulimwengu wa mwili. I was suffer kinyamaaa!
Uzuri nilikuwa natoa taarifa kwa kulalamika kwa mchungaji na viongozi wengine wa dhehebu langu, so mchungaji akanishauri kuvunja madhabahu walizojenga maadui zangu kwa kutoa sadaka. Baada ya hapo akanishauri kuanza kutoa 10%. Imagine nina madeni na ninapaswa kutoa 10%! Ni ngumu sana mzee ila ilinibidi nitumie imani ya KIMUNGU, nilitoa 10% kabla sijatumia pesa yoyote ktk mshahara wangu even kulipa deni! Guess what happen? Baadhi wafanyakazi wenzangu wakaanza kunikwepa na mwingine kuniita mchawi na mambo maovu yakaanza kuwarudia wao.
Umelioaje.madeni?
 
kwenye ibada sadaka ina umuhimu muhimu.
 

Attachments

  • Screenshot_20240808-134416.jpg
    Screenshot_20240808-134416.jpg
    175.2 KB · Views: 2
  • Screenshot_20240805-195543.jpg
    Screenshot_20240805-195543.jpg
    46.2 KB · Views: 2
  • Screenshot_20240805-195355.jpg
    Screenshot_20240805-195355.jpg
    347 KB · Views: 2
  • Screenshot_20240805-195312.jpg
    Screenshot_20240805-195312.jpg
    328.8 KB · Views: 2
  • Screenshot_20240805-195040.jpg
    Screenshot_20240805-195040.jpg
    323.4 KB · Views: 2
Nimesikia kua ukiwa na biashara fulani ukatolea zaka mtaji wako na baada ya hapo ukawa mwaminifu kulipa fungu la kumi katika faida unazovuna.. hapa UTAKUA UMEMALIZA MZIZI WA FITINA WA CHUMA ULETE. hivi hii inabe applied kwa vipi wabobezi wa imani naomba ufafanuzi.
Asee ni kwelii
Me bwana niliwahi fungus biashara ya kwanza sikutoa Zaka wala nn. Basi nikapitia changamoto ya kuuguza mtu wa karibu ikakosa usimamizi nikaifunga. Sikupatq hata mteja wa kununua zile kabati za vioo had Leo ziko stoo

Bas baada ya muda kama miaka 3 mbele nkafungua tena biashara Ila ile HeLa niliitolea zakaa. Kutokana na changamoto za umbali nikashindwa kusimamia. Nimekaa miezi 2 kimya sifungui maana sikuwa hata na Kodi kwa kuwa sijafungua. Nikawa nawaza nifunge tu Ila nkasema zile shelf ntazihifadhi wapi, grills na kabati zingine. Wakati bado najitafakari mwenye frem akanipigia nkajua a naomba Kodi kumbe alikuwa ananiambia vipi bado unahitaj hii frem nikamwambia usimamizi nashindwa kuisimamia Bora nimpe mtu anirudishie changu. Basi akanambia kuna wateja wamefika hapa wanataka wafungue biashara kama yako. Njoo muelewane mhesabiane gharama za vitu waichukue. Nilienda asee Yule kaka alinunua Hadi viti vibovu. Vitu alivyoacha ni vile mm mwenyewe nilikataa. Akanipa milion zangu kadhaa cash sikuamini. Kuanzia shelf za kisasa, grill LA mlangoni, na kila takataka iliyokuwepo. Zaka ni mwisho wa matatizo
 
Sababu kuu ni kuwa,

Usipolipa ZAKA, Mungu huondoa ulinzi kwenye Uchumi, AFYA, kibali nk nk, na hapo ndipo Shetani hupata nafasi ya kukutesa kupitia chuma ulete, magonjwa nk nk

Sasa ukilipa ZAKA, umemkaribisha Mungu alinde mambo Yako, sasa Kwa kuwa Mungu ni zaidi ya shetani, lazima shetani atimuliwe mbali.

Mimi nimepractice jambo Hilo najua Kwa uhalisia.
 
KWA TABU NILIYO PATA NA KANISA HAKUNA LILICHO NISAIDIA

WAKAJA KUNISAIDIA WATU WENGINE AMBAO HATA KANISANI HUWA HAWAFIKI

HAPO NDIPO NILIPO FAHAMU NINI MAANA YA UPENDO NA NDIPO NILIPO BADILI MAAMUZI

FUNGU LA KUMI LANGU NITAMNUNULIA HATA MPIGA DEBE MSOSI STENDI
Ukiona umelipa ZAKA sehemu Fulani na hufanikiwi, chunguza madhabahu hiyo, yaezakuwa wanatumia ushurikina, wachungaji na watumishi wa UONGO ni wengi sana nowadays.

Anyway kusaidia wajane, kulisha maskini pia ni Mahali salama kupeleka fungu la kumi.

Ushauri: Kabla ya kulipa ZAKA muombe Mungu athibitishe mawazo Yako juu ya wapi upeleke ZAKA, Ishara ni peace ndani Yako upelekapo ZAKA.
 
Mchungaji akiumwa anapelekwa hospital kubwa Muumini akiumwa aombewe 😁😁 hata Yesu Anashangaa huu unafiki
Acha uzushi,

Maombi Si mbadala wa hospitali.

Ukiugua nenda hospitali, hata madaktari na matabibu ni watumishi wa Mungu pia kusaidia watu.

Maombi hufanywa pale madaktari wanaposhindwa Kutoa ufumbuzi wa tatizo linalokusumbua.

Kuwa mkweli, Hila mwachie nyoka.
 
Zaka sio sadaka kwakuwa sadaka ni ya hiyari kulingana na Baraka za Mungu juu yako.
Zaka ni lazima na ni fixed. Haipaswi ipungue wala izidishwe.
Zaka ni takatifu
Zaka ni fungu La kumi la mapato yako yote HALALI (zingatia neno halali).
Sasa mtu anapata million 3 anatoa la elf 50 anasema anatoa zaka. Hiyo sio zaka kamili kwakuwa asilimia 10 ya million 3 ni laki 3.
Ukishamaliza zaka ndo utaamua sadaka utoeje sasa. Kama ni million au laki 5 ni wewe sasa.
 
Kwamba no nguvu yeyote ya MUNGU inazuia unyama wa chuma ulete?
Nilisahau alama ya kuuliza..... Haiwezi kuwa hivi....?

Pia nilitaka kuongezea sababu zaidi kwamba muda mwingine sio nguvu za giza bali ni wizi na kutofanya mahesabu.

Kwa kipengele cha ushirikina jiulize tu swali? Ni kwa nini chuma ulete haijawahi kuhusika benki????

Tukirudi kwenye mada, kama sababu ni uchawi kweli italinda lqkini ninakuhakikishia uchawi una kanuni zake na pesa zina kanuni zake. Uchawi mixer pesa kanuni zake zitakuwa tata sana kiasi ambacho ni wachache sana watakaoweza kuutumia kichawi
 
Zakat au sadaka ni lazima wapewe wanaohitaji zaidi kama yatima, masikini na wanaohitaji sana
Toa moja kwa moja kwa walengwa
 
Naona watu wanataka kupitiliza mipaka!

Baraka haziuzwi kwa bei ya zaka au sadaka! Meaning, kutoa kwako zaka na sadaka hakumlazimishi Mungu akulipe hapa hapa duniani kwa namna tutakayo sisi!

Tusirudishe Tena biashara haramu ya kuuza baraka za Mungu!
 
Imani za kishirikina hazifanyi kazi sababu ushirikina wenyewe haupo.
 
Fungu lenyewe wa kuwapa kina kiboko ya wachawi na Gwajiboy mkono wa baunsa ??

Kalishe mayatima, tembelea mahospital saidia kimya kimya no show off
 
Sababu kuu ni kuwa,

Usipolipa ZAKA, Mungu huondoa ulinzi kwenye Uchumi, AFYA, kibali nk nk, na hapo ndipo Shetani hupata nafasi ya kukutesa kupitia chuma ulete, magonjwa nk nk

Sasa ukilipa ZAKA, umemkaribisha Mungu alinde mambo Yako, sasa Kwa kuwa Mungu ni zaidi ya shetani, lazima shetani atimuliwe mbali.

Mimi nimepractice jambo Hilo najua Kwa uhalisia.
Amen
 
CHARITY BEGINS AT HOME
kabla ya kwenda huko nje kusaidia wanyonge (masikini,mayatima,walemavu,wagonjwa ,wajane,wagonjwa ,wenye shida mbalimbali, n.ktulisahau kusaidia ma kuwajali pia wanyumbani kwetu,ibada njema inaanzia nyumbani.
 

Attachments

  • Screenshot_20240926-173312.jpg
    Screenshot_20240926-173312.jpg
    92.6 KB · Views: 2
usifanye matangazo unapotoa msaada ,usimtangaze uliyemsaidia.
 

Attachments

  • images (89).jpeg
    images (89).jpeg
    8.8 KB · Views: 3
  • images (88).jpeg
    images (88).jpeg
    50.1 KB · Views: 3
  • images (90).jpeg
    images (90).jpeg
    41.4 KB · Views: 3
  • images (93).jpeg
    images (93).jpeg
    53.3 KB · Views: 3
  • images (92).jpeg
    images (92).jpeg
    45.7 KB · Views: 2
Back
Top Bottom