Imefikia hatua Ulaya inataka kuilazimisha China kufanya uhamishaji wa teknolojia Ulaya. How the table has turned!

Hahaha hayo mapicha picha tu, China hawezi ku lead kwenye drone technology halafu aogope kuwekewa vikwazo na marekani!.

Hawa wakiwezeshwa wanaweza, hizo drone wao wameanza kuzitengeneza juzi tu, marekani ni technologia iliyizeeka huko kwao.

Hawa al jazeera walisema HAMAS inawapiga Israel, lakini Dunia nzima walikutana UN wanasema Israel anawamaliza wapalestina.
Halafu leo wakwambie China is leading nawe unakubali?

Nakwambia siku china waki lead dunia hii tutapata shida sanaa.

Sasa hivi wameshindwa kuichukua Taiwan, baba lao kakaa mtu kati, hivi china iwe juu Marekani atatia pua pale kwa ufikiri wako?

Hong Kong tu walisubiri mpaka mkataba wa kikoloni wa uingereza uishe wakapewa, hawakufurukuta.

Hivi unaelewa nchi kuwa mbele kitechnoligia? Inawatishia wote duniani na akiongea mnasikiliza ndio maana yake.

jiulize tena kwanini Marekani akimwambia China sitaki umpe Rusdia silaha au msaada wowote, China anaufyata?

China hanaufahamu uwezo wake na anawafahamu wamarekani, na anafahamu hawezi dhidi ya wamarekani.

Wewe unajifurahisha tu na mipicha picha.

Wachina wana kiburi lakini hawawezi kwa wamarekani.

Marekani anawapa masharti wao na sio kinyume chake.
 
Hawa wanatoa cheap labor tu
China wana manufacturing supply chain ambayo Marekani na nchi za Ulaya hawana.

Hii ndio sababu kuu China imekuwa na lower production cost ukilinganisha na mataifa mengine duniani


"No supply chain in the world is more critical to us than China.
We're not in China for low labor costs....In the United States if we have a meeting of tooling engineers and we might not fill a room. In China, we would fill multiple
football fields."

–Tim Cook (Apple CEO)​
 
ww hujui viwanda vingi vya marekani walioeleka china, mexico, pakistani, vietnam na baadhi ya nchi hizo kwasababu ya cheap labor
China imewekeza zaidi kwenye manufacturing industries ASEAN kuliko Marekani. China ni trade partner mkubwa wa Latin America kuliko Marekani.

Viwanda vingi vilivyo Asia kama India na Pakistan vinategeme critical components na chemical kutoka China
 
Mfano Iphone zinatengenezwa china na India lakini siyo technologia ya wachina ni mikataba ya kazi.
iPhone imewekeza China ili kupata urahisi wa components, hata iPhone India wanaaguza parts kutoka China

Na ukae ukijua iPhone inatengenezwa na components kutoka mataifa mbalimbali kama Japan, Taiwan, China, South Korea n.k
 
Kuwa supplier haimaanishi kuwa advanced kitechnologia.
Unaelewa maana ya critical components? Huwezi kuwa supplier kama hauko na advanced tech. Quality matters.

Marekani inashindwa kuwa na domestic supplier kwa sababu hawana supply chain na skilled personnel

Trump mwenyewe Raisi wa Marekani alikiri kuwa kwa sasa wanahitaji wataalamu waliobobea wakawafundishe Wamarekani

Kama wewe Mmarekani wa Tandahimba utaamua kubishana na Trump endelea kubishana naye


 
Mpaka sasa anategemea vipuri kutoka usa ni mikataba tu, umeona drone za shaheed zina tengenezwa russia kwa chips za kimarekani halafu zina tumika vita ya ukraine.
Ninachojua drones za Ukraine na Russia zinatumia vipuri kutoka China
 
Manufacturing zilio
pelekwa China kutoka nchi zilizoendelea kwa sababu china wanauwezo wa kutoa cheap labor tu.

Siyo kwamba technologia za manufacturing nchi zingine hawana.

Nchi za Afrika hatupati hizo deal kwasababu ya political instability zetu lakini tuna cheap labor kuliko China, India, na bangladesh combined.

Na tungeweza ku vopete nao kwenye manufacturing, kwasababu industrial instalatiins walifanya wenye technologia kwa mikataba maalum.

Kuna kiwanda hapa kwetu kina tengeneza jens za levis lakini haziuzwi hapa kwetu, ni za wenyewe.

Sisi hapa tunapata 3rd class kutoka China huko unakosema wana manufacturing supplies.

China ni watumwa wa nchi za magharibi, kuna bidhaa na wao hawana access nazo licha ya kuzitengeneza kama sisi tu, sasa wana iga nembo na ku duplicate tunaletewa sisi masikini zaidi.

China wana jitafuta, viwanda vya wenyewe vilipopelekwa china siyo kwasababu walikuwa na akili sana, hapana ni cheap labor tu.

Uko ulaya na marekani labor imekuwa gharama sana, sasa wanaangalia sehemu cheap ya kuzalishia ndi china, india, bangladesh, vietnam, nepal n.k

Unawakuza sana hawana chochote hawa.
 
Hawa wachina wanaowekewa vikwazo na USA wawe juu kutechnologia kuliko USA yale macho yange toka nje.
Tangu Marekani aweke vikwazo imemwaathirije China?

Sehemu kubwa ya tech ambazo Marekani ameiwekea China vikwazo kwa sasa wana domestic supplier

Mfano Huawei ilizuiliwa kutumia Google's Android operating system, wamekuja na Harmony OS

Ila Marekani mpaka sasa hajapata domestic supplier wa rare earths tangu Mchina apige pini zisiingie Marekani

Umeona tofauti
 
Mchina na bidhaa zake fake leo hii ashindane na ulaya qe mwenyewe hushangai masimu fake anasuburi iphone atoe mpya origina yeye anakuja na feki yake ya hovyo bidhaa za china hovyo sana.
 
We una leta hadithi tu hapa.
Wachina watakuwa mbele miangi mingi ijayo siyo sasa.
Wakati China inatengeneza midoli, cherehani na baiskeli Marekani haikuwahi kuiwekea vikwazo China

Mara tu China ilipoanza kutengeneza bidhaa za high tech hapo ndipo Marekani ikaanza bans na tariffs.

Jiulize kwa nini iwe sasa na sio miaka ijayo?
 
Ni sahihi kwa sababu Marekani hawana manufacturing ecosystem
Hahaha eco system ipo sema labor imekuwa gharama sana huko kwao.

Wao marekani walizuia hata matumizi ya makaa ya mawe ambayo ndiyo nishati rahisi, walifunga hadi migodi ya makaa ya mawe ili kupunguza polution, china ndiyo nchi inaongoza kwa polution kwasababu hizo walikataa ku sign Kyoto agreements wakidai bado wanajitafuta.

Nchi za magharibi hawakuona ni big deal wakawaacha tu, kwasababu walijua wana watumia kwenye cheap labor.

Nchi za ulaya na marekani polution iko controlled, china wana puyanga tu, halafu ndio useme eti China kuna ecosystem?

Hutaki tu, lakini unaelewa, maxingira ya kazi china huwrzi yalinganisha na maxingira ya kazi ulaya na marekani.

China hawajali afya za watu wao, malipo hata huduma. Kuna high rate ya labor exploitation kwa ujumla.

wewe nahisi ni mchina lakini hutudanganyi kwenye hili.
 
Marekani ndio nchi inaweka vikwazo kwa nchi yoyote duniani including Russia, China hafi europe na wanatulia, hao nfio wawe juu kitechnologia kuliko usa?
Marekani inaweka vikwazo kwa China lakini Mchina anavipuuza tu

Mfano ununuzi wa mafuta kutoka Russia, Iran na Venezuela mataifa ambayo yamezuiwa kufanya biashara na nchi zingine

Bado China inaendelea kununua mafuta Venezuela. Upande wa Iran Mchina kajenga reli kabisa kutoka Iran hadi China kwa ajili ya kusafirisha mafuta tu

China na Russia zimejenga bomba la mafuta na gesi kutoka Russia hadi China

Hivi vikwazo vya Marekani ni kwa mataifa dhaifu kama ya Ulaya
 
Angalia russia kabla ya vita mskampuni kibao ya kimarekani yaliondoka mengine aliyazuia lakini uchumi una dorola.
Nani alikwambia uchumi wa Russia umedorora?

Nchi za Ulaya tangu zianze kushirikiana na Marekani kuiwekea vikwazo Russia ndio uchumi wao unazidi kudorora

Mfano kwa sasa uzalishaji viwandani umeshuka Ujerumani na nchi zingine za Ulaya kwa sababu walikuwa wanategemea cheap energy kutoka Russia

Bado Marekani yenyewe ni mteja mkubwa wa mbolea na uranium kutoka Russia mpaka sasa
 
Mchina na bidhaa zake fake leo hii ashindane na ulaya qe mwenyewe hushangai masimu fake anasuburi iphone atoe mpya origina yeye anakuja na feki yake ya hovyo bidhaa za china hovyo sana.
China ina brands zake za simu kama Huawei, VIVO, Xiaomi, Redmi, Oppo n.k

Kama wewe uliuziwa iPhone fake basi ni ushamba wako
 
Hahaha wewe unajifurahisha tu, hao hauwei walipigwa marufuku kushiriki soko la ulaya, na marekani na kwingine hata Brazil kwasababu ya wizi wa technoligia, wanatuuzia sisi tu huku Afrika.

Vikwazo china hawajawekewa, ila unaona kila siku wanaambiwa ukifanya hivi tutakuwekea vikwazo na hawafanyi, maana yake mkubwa wao marekani ana wamudu.

WANAOGOPA VIKWAXO KAMA UKOMA.

Marekani ina viwanda vingi china na bidhaa nyingi za marekani hutengenezwa china, lakini siyo kwasababu china inawazidi technoligia ni mikataba tu ya kibiashara.

Na kumbuka marekani aliusha sema nia yake siyo kui destabalize china ni kuisaidia China ikue.

CHip za Taiwan, China hana access nazo ziko controlled na marekani, na anauziwa chip za marekani kutoka intel, amd na makampuni mengine, tena siyo zile powerfull.

Juzi tu hspa walikuwa wana uziwa chip za nivdia zenye ubora, marekani akaikataza nivdia kuuza chip zenye uwezo mkubwa na nivdia kaacha mara moja. Kutoka 95 to 0%

China inajitahidi kutengeneza chip zake lakini hawajafikia uwezo huo licha ya kukkopi kopu chip za watu.

Wewe huwezi kuwa na uwezo unawekewa vikwazo, usicheke na yule, usile pale, usicheze hapo.

China ni wachumba tu kwa marekani.
 
China ina nishati za kila aina renewable na non renewable hii ni sababu nyingine kwa nini production cost China ni ndogo uwepo wa cheap energy umeifanya China kuwa world manufacturing powerhouse.

Imagine karibu 40% ya bidhaa duniani zinatoka China. Unafikiri ni nishati kadiri gani inahitajika ili taifa liweze kufanya uzalishaji kwa kiwango hicho?

Ukija CO2 emission per capita utagundua China sio mchafuzi kama Marekani

China peke yake inachangia ukuzi wa uchumi wa dunia kwa karibu 30%
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…