Imejitokeza sintofahamu ya watoto kupotea na kukutwa wakiwa wamefariki huku miili yao ikiwa haina baadhi ya viungo, mamlaka ichuke hatua stahiki

Wizara husika zinasemaje
Wanasiasa nao hasa wanaotegemea kura na majukwaa ya udanganyifu wanasemaje
 
haya matukio yamekua yakijitokeza hasa majira haya ya chaguzi.
Tuyakemee kwa pamoja
Mwanasiasa ambaye amethibitika kwenda kwa waganga ni yule mtemi fulani ambaye anatumia majina ya watu kwenye vyeti vyake (nashangaa kwanini hakutumbuliwa kipindi Cha vyeti feki) Kipindi Cha nyuma alikua na mchepuko wa kipare, Ni mrefu, mpenda sifa na mpenda ugomvi hasa na watu waliomzidi pesa, anapenda kukopakopa na akikataliwa anakua mbogo.
 
Kuna vitu ni aibu kwa nchi wameona wizi wa rasilimali hautoshi mpaka na damu zetu wanataka tena, wanasiasa wa kiafrika ni mashetani kabisa
 
Juzi alipotea baby girl 8yrs old alichukuliwa na boda eti.karudi Leo na chupi mpya.mamake alienda Hadi mochwari aliambiwa kuna watoto watatu maiti zimepokelewa. Katoka mochwari kakutana na mtoto njiani.sijui hata umekuaje maana nimeumia mno
 
Mungu wangu
 
Inasikitisha sana ,binadamu wana tamaa sana.
 
Kusimama mbele ya watu ili wakukubali sio mchezo, inahitajika ushirikina wa hali ya juu. Hata kama hujui kuongea unawekewa maneno mdomoni katika ulimwengu wa roho. Utakuta mtu hata shule hajaenda ila akikohoa tu kila mtu anamsikiliza.
Wewe na wenzako wanaoamini Kama wewe ndio chanzo kikuu cha matukio haya kuwepo.

Kwamba bila ushirikina huwezi kuaminika kwa jamii yako?

Hujui kujieleza ama matendo yako maovu na machafu yamefuta Imani ya jamii juu yako.

Achana na Ushirikina, umeumbwa kamili, unaweza chochote ukiamua, sio mpaka ukaroge!
 
Huwa nashangaa sana watanzania wanavyo jitapa kimataifa kwamba Tanzania ni nchi ya Amani.

Yani hata kwenye Top mia ya nchi zenye Amani duniani, Tanzania haipo na haifai kuwepo.

Hii Amani tunayo hubiriwa ni Amani uchwara.

Nioneshe top 100 ya nchi zenye amani duniani
 
Allah atulinde

Tusubiri taarifa rasmi kutoka kwa vyombo vinavyohusika na mamlaka husika pamoja na ufafanuzi.

Dkt. Gwajima D kwa sababu naona inahusu watoto, je, mna taarifa yoyote kuhusu hili?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…