Imekaaje Rais Samia kwenda na kiti chake kwenye ibada leo tarehe 14.10.2022 mkoani Kagera?

download%20(1).jpg

Ningekuwa Rais ningekuwa kama huyu mtu wa Mungu Jose Pepe Mujica aliyekuwa Rais wa Uruguay
 
Unachagulia watu habari za kujadili? Tatizo unalo wewe bila shaka.
Kama mnajadili mambo yasiyo na maana na hamtaki kuambiwa basi mna matatizo katika vichwa vyenu.

Yani leo mnataka kutumia siku nzima kujadili kiti cha Rais kuingizwa kanisani?
 
Mambo mengine ni madogo na hatutakiwi kuyakuza sana, ila nachokumbuka ni hiki: Miaka ya nyuma mwenzake alijaribu kufanya hivyo kule Iringa kwenye siku ya Nyerere, lakini mwashamu baba askofu Ngalalekumutwa akatia ngumu. Huku Kagera amelegezewa tu, ila kiuhalisia ni kwamba kwenye stoo (Vaults) za hizi dayosisi kunakuwa na viti vyenye thamani kubwa, ambavyo endapo Baba Mtakatifu (The Bishop of Rome) amekuja hupewa akalie. Kama tatizo ni kiti, basi angeweza kupewa akalie hata hicho.....
 
Kiprotokali, Kiusalama na kwa Tukio husika la Kiongozi wa Nchi GENTAMYCINE sijaona tatizo lolote lile la Rais Samia (Muislamu) kuingia Kanisani (Ibadani) pamoja na Kiti (Viti) akiwa na Makamu wa Rais Dk. Philip Mpango katika Nyerere Day ya Jana huko kwa Watani zangu Wapendwa Wahaya Mkoani Kagera (Bukoba)

Ni kweli huyu Mama (Rais) huwa tunamkosoa sana (nami nikiwemo) tukiwa na Lengo la Kumjenga kwakuwa tunampenda ila naanza kuona Sasa kuwa Watanzania tunaanza Kumuonea na kuwa na Nongwa zetu za ama Kiimani (Dini) na Wivu wetu.

Hivi Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere, Hayati Rais Mstaafu Mkapa na Hayati Rais Dk. Magufuli tena Wote wakiwa ni Wakristo Wakatoliki Wenzangu walikuwa hawaingii Misikitini?

Mbona Hayati Rais Dk. Magufuli alikuwa hadi anaingia Misikitini na 'Mamitambo' mengi ya Kiusalama kutoka kwa Watendaji wake na mlikuwa hamsemi chochote na iweje leo iwe Nongwa kwa Rais Samia kufanya hivyo Kanisani?

GENTAMYCINE ni Mtu wa Haki na Ukweli halafu sipendi Unafiki au kuona Mtu asiye na Kosa ama anaonewa au anasakamwa kwa mambo ya Kipumbavu (Kijuha) kutoka kwa Wapuuzi.

Mwacheni Mama (Rais Samia) afanye Kazi na kama ni Kumkosoa basi kuwe ni kwa Tija ili Kumjenga na Kumsaidia na siyo Kumsakama na Kumuonea tu kwa kila Kitu akifanyacho.

Kwako Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan tafadhali nakuomba tuzoee tu Sisi (Miswahili) kwani hatuna Jema wala Shukran hivyo Wewe endelea tu kuchapa Kazi na tambua ya kuwa Wanao Tukuka akina GENTAMYCINE tuko nyuma yako na tunakukubali na hata ukiniona nakupiga Dongo jua nataka tu Kukusahihisha mahala ila sikuchukii kabisa hata Malaika wa Mbinguni wanajua.

Macho na Masikio yote tu ni Sudan!!!
 
Magufuli aliingia msikiti gani na hayo mamitambo ya usalama? Maana nakumbuka mara nyingi aliwakilishwa na Waziri Mkuu wake. Na wakati huo huo yeye mwenyewe alipohudhuria ibada Kanisani, mara zote hakwenda na kiti chake! Badala yake alikaa kwenye madawati ya kawaida kabisa awapo Kanisani kama waumini wengine.

Kwa taarifa yako, hili suala la Marais kuwa na Viti vyao maalum kanisani! Limekuwa likijitokeza zaidi kwa Marais kutoka imani nyingine!

Na kama ulikuwa hufahamu, Askofu Ngararekumtwa wa Jimbo la Iringa enzi za awamu ya nne, na akiwa ni rais wa Baraza la Maaskofu (TEC), alishawahi kumzuia Rais wa wakati huo kuingia na kiti chake Kanisani! Na huyo Rais alilazimika kuahirisha kuhudhuria hilo tukio. Maana kwa Kanisa, hiyo ni dharau.
 
Magufuli aliingia msikiti gani na hayo mamitambo ya usalama? Maana nakumbuka mara nyingi aliwakilishwa na Waziri Mkuu wake. Na wakati huo huo yeye mwenyewe alipohudhuria ibada Kanidani, mara zote hakwenda na kiti chake! Badala yake alikaa kwenye madawati ya kawaida kabisa awapo Kanisani kama waumini wengine.

Wakati mwingine nashindwa kuelewa msingi wa haya malalamiko, mengi mpaka kuhusu viti.

Hivi tunashindania vitu vidogo ili iweje? tangu lini mkristu akawa wa kuhangaikia haya mambo ya ulimwengu? mnaenda kinyume na maandiko!.

Mkristu ameshaambiwa kwenye maandiko, aheshimu mamlaka zilizopo, sasa kama mamlaka zimeamua kuingia na kiti chao shida inatokea wapi? ajabu mnaanza kushindana na mamlaka!.

Tatizo linakuwa kubwa kama chimbuko la jambo huwa ni wanasiasa, hivyo mashabiki wa vyama husika hujikuta wanaingia kwenye malumbano bila kuruhusu bongo zao kutafakari, hivyo kuishia kuchotwa akili na wanasiasa.
 
Wakati Mwalimu alikaa hadi foleni na Marais wengine wanakalia viti vya kanisani kwa adabu, kuna Paka special linasafirisha na kukalia kiti maalum👇🐒🐒

AAq4U0.jpeg
ADPZA.png
YAMVHzi.jpeg
 
Wakati mwingine nashindwa kuelewa msingi wa haya malalamiko, mengi mpaka kuhusu viti.

Hivi tunashindania vitu vidogo ili iweje? tangu lini mkristu akawa wa kuhangaikia haya mambo ya ulimwengu? mnaenda kinyume na maandiko!.

Mkristu ameshaambiwa kwenye maandiko, aheshimu mamlaka zilizopo, sasa kama mamlaka zimeamua kuingia na kiti chao shida inatokea wapi? ajabu mnaanza kushindana na mamlaka!.

Tatizo linakuwa kubwa kama chimbuko la jambo huwa ni wanasiasa, hivyo mashabiki wa vyama husika hujikuta wanaingia kwenye malumbano bila kuruhusu bongo zao kutafakari, hivyo kuishia kuchotwa akili na wanasiasa.
Yaani kiufupi hatutaki mje na hivyo viti vyenu Kanisani kwetu. Kama hamuwezi kuviacha huko kwenye ofisi/magari yenu, basi muache kuingia Kanisani kwetu.

Hongera nyingi kwa Mhashamu Askofu Ngararekumtwa. Kanisa Katoliki hatutaki madharau.
 
Wakati mwingine nashindwa kuelewa msingi wa haya malalamiko, mengi mpaka kuhusu viti.

Hivi tunashindania vitu vidogo ili iweje? tangu lini mkristu akawa wa kuhangaikia haya mambo ya ulimwengu? mnaenda kinyume na maandiko!.

Mkristu ameshaambiwa kwenye maandiko, aheshimu mamlaka zilizopo, sasa kama mamlaka zimeamua kuingia na kiti chao shida inatokea wapi? ajabu mnaanza kushindana na mamlaka!.

Tatizo linakuwa kubwa kama chimbuko la jambo huwa ni wanasiasa, hivyo mashabiki wa vyama husika hujikuta wanaingia kwenye malumbano bila kuruhusu bongo zao kutafakari, hivyo kuishia kuchotwa akili na wanasiasa.
Where do you get time to waste Educating that authentic Moron on this Platform?
 
Magufuli aliingia msikiti gani na hayo mamitambo ya usalama? Maana nakumbuka mara nyingi aliwakilishwa na Waziri Mkuu wake. Na wakati huo huo yeye mwenyewe alipohudhuria ibada Kanidani, mara zote hakwenda na kiti chake! Badala yake alikaa kwenye madawati ya kawaida kabisa awapo Kanisani kama waumini wengine.

Kwa taarifa yako, hili suala la Marais kuwa na Viti vyao maalum kanisani! Limekuwa likijitokeza zaidi kwa Marais kutoka imani nyingine!

Na kama ulikuwa hufahamu, Askofu Ngararekumtwa wa Jimbo la Iringa enzi za awamu ya nne, na akiwa ni rais wa Baraza la Maaskofu (TEC), alishawahi kumzuia Rais wa wakati huo kuingia na kiti chake Kanisani! Na huyo Rais alilazimika kuahirisha kuhudhuria hilo tukio. Maana kwa Kanisa, hiyo ni dharau.
Magufuli kaingia sana tu msikitini mnona

Ova
Screenshot_20221015-101148_YouTube.jpg
 
Wewe popoma jibu hoja! Magufuli alikuwa anaingia na kiti chake Kanisani, au huko msikitini kama alivyofanya huyu mama?

Na unafahamu huo utaratibu wa kuingia na viti maalum vya Urais kwenye makanisa ya Kikatoliki hufanywa na Marais ambao ni Waislam? JK alijaribu kufanya hivi, akazuiliwa na na Askofu wa Jimbo la Iringa na rais wa TEC wa wakati huo!

Jibu hoja! Badala ya kujipendekeza na kuendeleza ule unafiki wako wa miaka nenda.
 
Back
Top Bottom